kevin strootman
JF-Expert Member
- Nov 26, 2017
- 1,077
- 1,728
Ni takribani siku 4 tangu kupoteza maisha kwa binti aliyefahamika kwa jina la Rachel William aliyefariki dunia kwa kukosa huduma baada ya kufika katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwaajili ya kujifungua na kushindwa kupatiwa huduma hiyo bila kutoa kiasi cha fedha alichoambiwa na daktari.
Tukio hilo limetokea Disemba 28, 2023 katika hospitali ya wilaya ya Kahama ambapo marehemu alifika hospitalini hapo kwaajili ya kujifungua ndipo aliambiwa atoe fedha ili apatiwe huduma.
Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo kiongozi wa familia Mwanambalu Shinje anaeleza kuwa kutokana na kumpoteza binti na kichanga kwa uzembe uliofanywa na watoa huduma kama familia waliamua kutofanya mazishi ya marehemu hao.
Akitoa salamu za pole Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amesikitishwa kutokea kwa tukio hilo huku mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ameishauri serikali kuwachukulia hatua watumishi waliojihusisha na tukio hilo.
Akizungumza kwa njia ya simu Kaimu mkurugenzi manispaa ya Kahama Clemency Mkusu Anaeleza hatua zilizochukuliwa baada ya kubaini tukio hilo ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa waliobainika kujihusisha na kitendo hicho.
NB: Kwenye hii Dunia hasa ukiwa unaishi Tanzania Fanya juu chini usikose pesa, pesa ndio itakufanya uishi, Fanya unavyoweza iba, tumia ndagu Yani we Fanya unavyojua ila usikose hela.
View attachment 2859671