Assume: Muungano umevunjika

Dawa ya Muungano ni kuuvunja tu. MUUNGANO! Hauna faida. Wananchi wa Zanz hawautaki. Viongozi wa Zanz wanautaka, sio kwa sababu wanaupenda, bali kwa sababu unawapa vyeo na mafedha ya kumwaga. Angalia, kutoka Zanz kwa sasa (ka-sehemu kenye watu laki 8, mara tano ya mkoa wa Mwanza wenye watu takribani milioni 4) kuna Makamu wa Rais wa Muungano, kuna Mawaziri 7 na manaibu kadhaa, mabalozi lukuki, makatibu wakuu wa wizara, majaji, wabunge 80 nk; huku MWANZA kuna waziri mmoja tu, wabunge 10. Usawa uko wapi? HAKUNA, MUUNGANO UVUNJWE.

Alafu, Zanz hawachangii fedha za kuendesha Muungano huo, wao wanavuna tu mapesa.n Ni mafisadi hawa. Vunja MUUNGANO PLEASE
 
Dawa ya Muungano ni kuuvunja tu. MUUNGANO! Hauna faida. Wananchi wa Zanz hawautaki. Viongozi wa Zanz wanautaka, sio kwa sababu wanaupenda, bali kwa sababu unawapa vyeo na mafedha ya kumwaga. Angalia, kutoka Zanz kwa sasa (ka-sehemu kenye watu laki 8, mara tano ya mkoa wa Mwanza wenye watu takribani milioni 4) kuna Makamu wa Rais wa Muungano, kuna Mawaziri 7 na manaibu kadhaa, mabalozi lukuki, makatibu wakuu wa wizara, majaji, wabunge 80 nk; huku MWANZA kuna waziri mmoja tu, wabunge 10. Usawa uko wapi? HAKUNA, MUUNGANO UVUNJWE.

Alafu, Zanz hawachangii fedha za kuendesha Muungano huo, wao wanavuna tu mapesa.n Ni mafisadi hawa. Vunja MUUNGANO PLEASE
vunja pleaseeeeeeeeeee
 
Mi nashindwa kuelewa huu muungano ni wa sababu zipi kwa sasa! Mana sababu zilizofanya tuungane miaka ya 64 sasa hivi hazipo. Ni bora uvunjwe na itangazwe duniani kote, ili wabara turudishiwe Tanganyika yetu. Wazanzibari walioko Tanganyika wote warudi kwao watuachie ardhi yetu na watanganyika walioko zanzibar warudi.
 
Mi nashindwa kuelewa huu muungano ni wa sababu zipi kwa sasa! Mana sababu zilizofanya tuungane miaka ya 64 sasa hivi hazipo. Ni bora uvunjwe na itangazwe duniani kote, ili wabara turudishiwe Tanganyika yetu. Wazanzibari walioko Tanganyika wote warudi kwao watuachie ardhi yetu na watanganyika walioko zanzibar warudi.
wao hata wakibaki sio shida ila watangannyika wenzetu warudishwe tu huku
 
Mm naungana mtoa mada kwamba bado watanganyika mnakuwa
wazito kuelewa ni kwamba ili amani ya muungano ipatikane bac kuwe na serikali3 na gharama zitapungua kwani wizara ni zilezile ila tu ambazo zìnashughulikia mambo ya muungano zitakuwa za muungano na za Tanganyika zitabakia kuwa za tanganyika na za Zanzibar pia zitabakia kuwa za zanzibar hivyo
gharama zitakuwa hizozo ila kwa muda huu ucfikirie kuwepo kwa serikali 1 ikiwa 2 watoto wa wazanzibar
 
Nazidi kuwashauri mrudishe Utaifa wenu wa Tanganyika.

Kwani hata mwanamke akiolewa na kisha kuachika basi anarudia lile jina lake la zamani.

KARIB TANGANYIKA
 
Kwanza kabisa Tanganyika haikuondolewa kwa ridhaa ya wananchi
Hili ni tatizo kubwa katika katiba
Tanganyika irudi kwanza ili tuweze kujadili katiba
Katiba ya zanzibar, Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Muungano
Tuangalie sasa kama tunaweza kuongeza nchi nyingine kama:
Burundi
Rwanda
Congo
Uganda
Kenya
Sudan kusin NK

Tasijidanganye na muungano wa mchezo wa kuigiza wa serikali mbili na katiba mbili
Hauna uhai
haukui
Utakufa.:pound:
 
Lula wa Ndali-Mwananzela

NAANDIKA makala hii nikiwa na moyo mzito na machozi. Ninaupenda Muungano wetu na ni tunu ambayo naamini inastahili kutetewa hata kwa damu. Lakini siamini kama unastahili tena kutetewa na mtu yeyote bali tujiandae kuuvunja yaishe.

Kwa vile Muungano wetu unaelekea kuvunjwa au kuvunjika na kwa vile hauna watetezi tena zaidi ya wale ambao wanauangalia kwa misingi ya kisheria ni wazi basi Muungano wetu unaelekea kuvunjika au kuvunjwa.

Dalili zote zilizopo sasa zinaonyesha kuwa vile ambavyo tulikuwa tunaviita "kero" vimegeuka kuwa "sababu" tosha ya kuvunja Muungano kwani kero zikizidi huwa sababu.


Kwa vile Muungano wetu umefikia mahali ambapo hauteteeki wala kuokoleka (kama kilivyo chama fulani) ni wazi basi kujiandaa kama Taifa kuelekea hatimaya Muungano wetu.

Tukumbuke kuwa Muungano ulianzishwa na watu na ni watu wenyewe wenye uwezo wa kuuvunja. Hatuwezi kuutetea Muungano kwa misingi ya kiuchumi na maslahi tu. Muungano wetu haukujengwa kwa misingi ya kiuchumi au maslahi fulani, ulijengwa kutokana na tunu ya kuungana kwenyewe na kuwa na Taifa moja.


Leo hii Muungano huu unahojiwa kwa sababu za kiuchumi na kwa vile hizo ndizo fikra zake basi utavunjika kwa sababu hizo hizo.

Tukio la hivi juzi ambao vijana wa Kitanzania wamewachomea vijana wengine wa Kitanzania vibanda vyao vya biashara ati kwa "kuchoshwa na Muungano" na viongozi wetu wanaendelea kuishi katika pepo yao kana kwamba ni jambo la kutokujali, imenisikitisha. Imenisikitisha kwa sababu watawala wetu wanafikiria Muungano utavunjwa kwa sababu ya mambo makubwa, la hasha.


Baada ya kuchomeana vibanda kitakachofuata ni mauaji ya kundi la watu. Kwa vile tayari tuna watu ambao wana "ujasiri" kama tunaweza kuuita hivyo, wa kutumia silaha kuwadhuru watu wengine kwa sababu za kisiasa ni wazi kuwa mauaji hayatokuwa mbali sana. Tutaamka siku moja tutasikia huko Zanzibar vijana wetu kadhaa "wenye asili ya Bara" wamekutwa wameuawa na ujumbe umewekwa kuwa "hatuutaki Muungano".

Na kwa kadiri watawala wetu bado wanasuasua kuona uzito wa tukio hili vijana wa Bara nao wakisikia wenzao wametendewa hivyo, watalipiza kisasi huku Bara na mara moja tutaanza kuona kile ambacho tumekuwa tukikiona kwenye filamu tu.

Tutaona "watu wenye asili ya Visiwani" wakianza kupanda boti na meli kurudi "kwao" na wale Wamasai na Wachagga walioko Zanzibar wakianza kufunga virago na kupanda meli kurudi Bara.


Tayari kumekuwa na matukio ya nyumba za ibada za Wakristu kuchomwa moto na biashara zao kutiwa kiberiti. Hatujaona Rais wa nchi yetu akilizungumzia wala Rais wa Zanzibar wote wanaona mambo haya ni "isolated incidents" yaani mambo madogo tu yanayokuzwa bila "sababu".

Kwa sisi tulijifunza historia ya mambo ya utaifa tunajua jinsi gani hisia za utaifa zinaweza kuzaa mambo makubwa zaidi. Nimemuoana Shehe Basalleh akisema wazi kuwa kama Muungano uvunjwe "turudi kwetu" akimaanisha Zanzibar. Tanzania Bara si kwake.


Kwa hiyo ndugu zangu Muungano umeshaanza kuvunjika na inawezekana umeshafika mbali sana kwenye kuvunjika kwani kabla ya kuvunjika kisheria unatakiwa uvunjike katika mioyo ya watu kwanza.

Tayari kuna sababu nyingi ambazo zimetolewa za kwanini tusiendelee kuungana na kama nilivyosema hapo juu hakuna watetezi wa Muungano waliobakia, ni wazi kuwa Muungano uliopo sasa umebakia wa kiuchumi na si kisiasa na tunu.


Wakongwe kama kina Nassoro Moyo ambao tulitarajia kuwa watetezi wa Muungano wanawatia moyo hawa wanaotaka kuvunja Muungano. Nimeona mahali ambapo msomi mmoja ninayemheshimu sana wa Zanzibar akiwalalamikia "wa Bara" kwanini wanang'ang'ania Muungano wakati "Zanzibar hawautaki". Na yeye mwenyewe ana ndugu wamejazana Bara kila kona!


Sasa kwanini tufike kote huko? Hivi ni kweli watu wa Bara tunaung'ang'ania Muungano hivyo? Hivyo nimeamua kujitolea kutoa mwongozo wa wazi na wa bure ili tuweze kuvunja Muungano bila kuchomeana vibanda na ili hatimaye Muungano ukishavunjika nchi zetu mbili zisiwe maadui.


Ninachoogopa ni kuwa japo wengine wanafikiria kwa kutumia hiana wataweza kuvunja Muungano na wakabakia rafiki wakati watu wameumizana. Kwa mtindo ambao unaelekea sasa Muungano ukivunjika hakutakuwa na undugu tena kati ya Bara na Zanzibar, na utakuwa ni uhasama wa aina fulani.

Zanzibar kama nchi ndogo haitoweza kuwa katika hisia ya usalama na Bara haitoacha kuona Zanzibar inaweka ushirikiano wa kiusalama na nchi nyingine yoyote ambayo itatishia usalama wa Tanzania Bara. Sababu zile zile za miaka ile zitarudi tena.

Sasa kwanini tufike huko? Kwanini tusiamue kuuvunja Muungano wetu vizuri na baadaye kubakia kuwa ni marafiki wa damu. Kama Wamarekani na Waingereza walipigana vita na Marekani ikavunja Muungano wake wa damu (wenyewe wanawaita Waingereza mabinamu zao) lakini leo hakuna nchi zenye uhusiano "maalumu" kama Wamarekani na Waingereza.

Waingereza watakufa kwa ajili ya Wamarekani na Wamarekani vivyo hivyo kwa ajili ya Waingereza. Lakini si nchi moja. Je, yawezekana kuwa na uhusiano kama huo kati ya Zanzibar na Tanzania Bara (ambayo naamini itabakia na jina la Tanzania)?

Hawa wanaochoma vibanda na kuvumiliwa wanataka kufanya iwe ngumu kabisa na uhasama wa pekee kati ya watu wa Visiwani na watu wa Bara huko mbele. Kama haya yanayofanyika sasa yanaonekana kama ni mambo madogo yatakapotokea makubwa itakuwa tumechelewa kabisa kuokoa uhusiano wetu. Mwisho tutabakia katika hali ya utete kama ilivyo Ireland ya Kaskazini na Uingereza.


Ufuatao basi ni utangulizi wa bure wa jinsi gani tunaweza kuvunja Muungano wetu bila ulazima wa kuchomeana vibanda!

Wawakilishi wakutane na wananchi wawasikilize Wabunge wa Bara na na Wawakilishi wa Zanzibar waende kukutana na wapiga kura wao na kuwauliza maoni yao kama Muungano uendelee kuwapo au uvunjike. Sijasema wawaulize suala la kero au mabadiliko gani wanayataka la hasha, liwe swali moja na jepesi tu, je, Muungano wa aina yoyote kati ya Tanganyika na Zanzibar uwepo?


Tukubaliane kwenye kanuni kwanza kabla hatujaamua marekebisho gani. Kama kikanuni wananchi hawataki Muungano wa aina yoyote basi hatua ya pili ifikiwe.

Hili swali halihitaji kamati wala kura ya maoni, inahitaji Wabunge na Wawakilishi wakutane na wapiga kura wao na wawasikilize na wakishawasikiliza warudi Bungeni na katika Baraza la Wawakilishi kutoa azimio kwa minajili ya sauti za wananchi.


Kama wananchi wanasema Muungano wa aina yoyote usiwepo (iwe serikali moja, mbili au tatu) basi hatua za kuuvunja ziendelee. Baraza la Wawakilishi waje na azimio la pamoja la kutangaza msimamo wao wa kutaka Zanzibar ijitoe kwenye Muungano na vile vile Bunge la Muungano nalo lifanye hivyo.


hapa ndipo tume ya pamoja iundwe ambayo itatekeleza taratibu zifuatazo.

Tarehe ya kuvunja Muungano iwekwe kama marabaza yote mawili ambayo yanawakilisha wananchi wetu yatachukua hatua hiyo basi hapo ipangwe tarehe ambayo Muungano huu utavunjwa. Kwa mfano tukakubaliana kuwa ifipako Julai 1, 2012 Tanzania iliyoungana haitokuwepo basi wananchi wa pande mbili waanze kujiandaa kuelekea nchi mbili.
Masuala ya haki mbalimbali yaamuliwe.

Mojawapo ya mambo ambayo yatahitaji kuamuriwa kabla ya Muungano kuvunjika ni haki mbalimbali za pande hizi mbili. Mambo hayo yatahitaji kujibu swali la "nani anapata nini na kwanini". Kwa mfano, madeni ya Zanzibar kwa TANESCO yatalipwa na nani na kwa msingi gani? Hili likizungumzwa pamoja na wafadhili Zanzibar inaweza kupatiwa msaada wa kulipa madeni fulani. Lakini wakati huo huo Bara yaweza kujikuta inahitaji kufanya mambo fulani kusaidia Zanzibar kujianzishia ilipo.


Uzuri ni kuwa Zanzibar tayari ina vyombo vyake vingi ambavyo itakuwa rahisi tu kuvibadili na kuwa vya Zanzibar kamili. Hivyo, Zanzibar haitoanzia kwenye sifuri kwani si nchi mpya inayoanza bali kurudi kwa nchi ya awali. Wazanzibari wenyewe wataamua wanataka kurudia Zanzibar ipi.


Hivyo maswali mbalimbali yatahitaji kuamuliwa mapema kuanzia suala la mapato, madeni, usalama, rasilimali n.k. Maswali haya yatahusisha bila ya shaka mambo ambayo yatakuwa na moto sana kwa pande zote mbili lakini kwa kushirikiana na kwa uwazi mambo yanaweza kupatiwa ufumbuzi.

Hofu yangu ni kuwa baadhi ya mambo hayo hayo ndiyo yamekuwa sababu ya "kero" na sijui tutakapovunja Muungano huu tutayatatua vipi bila kusababisha uhasama na vurugu za kudai "haki".

Baada ya Muungano huu kuvunjika maswali ya mahusiano mapya

Kwa vile ukweli ni kuwa kinachovunjwa ni mahusiano ya Muungano wetu bado ukweli ni kuwa tukiamka asubuhi baada ya tarehe ya kuvunjika Muungano Zanzibar itakuwa iko pale pale na Bara itakuwa pale pale na Bahari ya Hindi itaendelea kututenganisha.

Lakini huo utakuwa ni mwanzo wa mahusiano mapya kati yetu. Hivyo, Wazanzibar wataamka na furaha ya kuipata nchi yao ambayo wanaona imemezwa na Tanganyika na Watanzania (kama watakavyobakia kuitwa) wataamka wakiwa na furaha ya kuona hatimaye manung'uniko ya upande mmoja yatakuwa yamekoma.


Sehemu zote mbili zitaamka zikiwa na matatizo yale yale ya wananchi wao! Watu wa pande zote mbili watagundua kuwa matatizo yao hayakutokana na Muungano na hapo ndipo watakapojua kuwa bado hata wakivunja Muungano itabidi bado washughulikie matatizo yale yale, vita ile ile dhidi ya magonjwa, ujinga na umasikini.

Bado wataamka na kukuta bado ajira ni tatizo kubwa na maisha ya watu wao bado ni duni. Watakuwa kama wale waandamanaji wa Misri ambao walifikiria wakimng'oa "adui" wao Hosni Mubarak ndio utakuwa mwisho wa matatizo yao. Baada ya Mubarak kuondoka wamejikuta bado wana matatizo yale yale japo wamepata matumaini.


Ndugu zangu hata tukiuvunja Muungano kesho au keshokutwa matatizo ya watu wa Zanzibar na wale wa Bara yatabakia kuwa ni matatizo yao japo kwa wakati huo haiwezekani kumlaumu "mwingine".

Wazanzibari kwa mara nyingine tena watarudi kuwalaumu watawala wao wenyewe na si ‘wakoloni Watanganyika' waliowachomea vibanda miaka michache nyuma. Hili si geni kwa Zanzibar kwani kabla ya Mapinduzi waliwalaumu watawala wao wenyewe.

Katika barua ambayo imeenezwa sana kwenye mitandao ya wazee kutoka Zanzibar waliomuandikia Rais Jakaya Kikwete hoja zao walisema hivi "haitakuwa ajabu kama itafikia pahala ama Wazanzibari, Watanganyika, au wote kwa pamoja kama watakataa Muungano. Maamuzi yao yaheshimiwe na tuachane na Muungano kwa salama na amani.

"Hii haitakua aibu kwetu kwani ni jambo la kawaida kwa mataifa yaliyoungana na hatamaye kugawanyika ili kila mmoja ashike ubao wake na aendelee na safari katika jahazi lake. Zipo nchi nyingi zilizowahi kupita katika mkondo kama huu wa Muungano na leo hii wameshasahau kama walikuwa wamoja."

Mimi nakubaliana na wazee hawa. Tuna mambo mengi yanayowasumbua watu wetu, tuna safari ndefu ya kuelekea ujenzi wa Taifa la kisasa na tuna matatizo mengi kabisa yanayotusumbua kwa muda mrefu, suala la Muungano halitakiwi kuwa mojawapo.


Kwa sababu Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka karibu 50 wameshindwa kutatua matatizo haya au hata kutuongoza na hasa kwa vile hakuna mwana CCM anayeweza kusimama na kuutetea Muungano kwa kanuni na tunu ni wazi njia bora na ya ukweli ni kuishia kuuvunja vizuri.

Badala ya kuuacha ulipuke na kutuvuruga tutumie uwezo wetu tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu kuandaa njia ya kuelekea kuuvunja huu Muungano.

Ninasema hivi kama mwanafunzi mzuri sana wa Mwalimu Julius Nyerere na ambaye ninaamini katika Afrika iliyoungana. Lakini kama wazee wetu walioutumikia Muungnao huu kama kina Moyo na Salim Ahmed Salim hawawezi kuutetea sisi wengine tuendelee kuutetea kwa ajili gani?


Kama Kikwete na kina John Malecela, Kingunge Ngombale na wengine wao hawawezi kusimama kuutetea kwanini sisi wengine tuutetee? Wameshindwa kuutetea tangu mwanzo na hawawezi kuutetea kama Nyerere alivyoutetea kwa hoja! Hakuna anayeweza kuutetea kati yao na akabakia mkweli kwa nafsi yake.

Tuuvunje Muungano tuanze mahusiano mapya! Wenye kupata wapate, wenye kukosa wakose. Lakini tunapofikia watu wanaanza kuchomeana mali zao basi tujue ni utangulizi wa watu kuondoleana roho zao. Na tutalaaniwa kama tutafika huko wakati tulikuwa na uwezo wa kuachana na kubakia marafiki wa kudumu na kama watu hawataki hata urafiki basi na tuwe maadui.
 

Attachments

  • KATUNI168.jpg
    KATUNI168.jpg
    21.6 KB · Views: 35
Mzee Mwanakijiji-Umewaficha watu wazima ukawafumbulia watoto wadogo nini mbona sijakupata sawa sawa? Nilitegemea zaidi
 
watoto wa KIJAMAAA wataja lalamika kwa mawimbi na hakuna atakaye kuja kujibu hoja zaidi ya kukutukana binafsi na kukushambuia kama wewe

Pili kutakuwa na mambo ya kuletewa maneno ya MFU/MZOGA liyekufa miaka kadhaa iliyopita as if wengine hawana akili za kufikiria
Sidhani ni uungwana kumuita marehemu yeyote yule "mzoga." Kama huwezi kujirekebisha lugha nitapeleka malalamiko kwa mods.
 


Written by Nassor20 // 12/05/2011 // Habari // No comments

Upinzani kushinda Bara nitabu kama hawato anzisha vuguvugu la kurudisha Tanganyika.

Muungano ukivunjika Wabara watajitambulisha kwa jina gani? Watanzania au
watanganyika?



Wazanzibar tusidanganyane kuwa Tanganyika kuna vyama vingi vya upinzani na
dini tafauti, mimi naungana na wale wenyekusema kuwa Watanganyika wote ni ccm na
lengo lao wote ni moja.



Wewe angalia mfano mdogo tu? Wazanzibar wanapo zungumzia kero za Muungano
watanganyika wote huwa kitu kimmoja na husahau tafauti za dini zao na itikadi za
vyama vyao.



Na jambo hili huwakasirisha sana utazani Zanzibar ilikuwa ni nchi yao
Watanganyika? na kusema Zanzibar ina nchi kamili na Raisi wake? sisi hatuna hata
nchi? ok nyiyi hamuna hata nchi? kwa nini munashindwa kuidai nchi yenu ya
Tanganyika ambayo Nyerere kaiuza kwenye utashi wa itikadi za chama cha ccm na
ilani ya ccm ndio imekuwa Tanganyika.



Nyiyi Watanganyika kwa vile hamuna nchi kama munavyo sema? ilikuwa muwe
wamwanzo kudai nchi yenu Tanganyika kwa vile ina historia ya Bibi zenu na Babu
zenu? mimi hushangazwa na watu hawa? hivi karibuni walikubali jinchi lao liwe na
Guverner lakini tu Zanzibar wasiikose, jee hamuoni haya kupenda wasio wapenda?
au ndio ukaona vijanajike vya Bara hupenda kuolewa na Wazanzibar kuna siri kani
mpaka mukaparadia sana Wazanzibar wawaowe?.



Watanganyika kama kweli munataka kuiuwa ccm na upinzani ushinde huko mupate
Tanganyika yenu basi piganieni kurudishwa kwa Tanganyika ambayo Nyerere na ccm
yake wameiuwa kuliko kupotezwa muelekeo wa kuiparatikia Zanzibar lazima iwemo
kwenye Muungano wakati Wazanzibar hawataki tena.



Mutakuja kuazirika vibaya kama hamukuchangamka kudai Tanganyika yenu, hivi
sasa ccm hushinda ushaguzi kwa sababu wameshawastukizia kuwa hamuna lenu jambo
ni nguvu ya kuzungumza tu mbele ya action muko 0, ndio ukaona ktk ushaguzi nguvu
zote za kijeshi hupelekwa Zanzibar na nyiyi huonekana watu poa tu mukisha
kuambiwa Wazanzibar wanataka kuvunja Muungano nyiyi huwa kimya?.
 
Back
Top Bottom