Askofu Shao amgeuka Magufuli, asema mizengwe kwenye uchaguzi mdogo ni ishara serikali haielewi maana ya demokrasia

Mimi Hii kitu democracy sitaki kuisikia kabisa hiyo democrasia ndiyo iliyosababisha celtel kuchukuliwa,escro,migodi kubinafisishwa wizi chungu mzima


Magufuli naomba ukaze hivyo hivyo maana hata haya makanisa yanatunyonya tu sisi wananchi wa chini ilitakiwa waridishiwe kodi
 
Askofu Shao aliwahi kumsifia Magufuli hadi kumfananisha na Rais wa Zimbabwe aliyeondoka madarakani Robert Mugabe

Askofu Shao amfananisha Rais Magufuli na Robert Mugabe wa Zimbabwe... ataka watanzania tumuunge mkono!



Lakini kwenye leo kwenye ibada ya Krismas iliyofanyika leo Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Zanzibar Mhashamu Augustino Shao amesema ipo haja kwa serikali kuelewa dhana ya demokrasia kutokana na mchango wake katika maendeleo ya taifa

Amesema mizengwe iliyofanyika kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani huko bara ni ishara kuwa serikali haielewi maana ya demokrasia, yaani kutofautiana

Pia amekemea watu wanaoiibia serikali na kusema hiyo ni dhambi kubwa
View attachment 658971

Hata hiyo kumfananisha na Mugabe ilikuwa siyo sifa bali kejeli...sema Magu alivyo mweupe akaibeba ilivyo, na akina Msigwa wa Ikulu kwa ujinga wa level flan nao pia wakainukuu na kuiripoti kama ilivyo, neno kwa neno!
 
Magufuli ni rais wa nchi, ni zaidi ya mkazi wa Dar. Kama ni hivyo basi Magufuli asingezunguka nchi nzima angebaki Dar tu. Inaonekana unashindwa kuvumilia kusikia ukweli. Huu unyama mnaendeleza kwa kuwa viongozi wa dini wamekaa kimya hivyo mnaona kila unyama na kuvunja sheria mnakofanya mko sawa.
Usichanganye uumini na uraisi Magufuli kwa viongozi wa dini ni muumini wakichanganya na siasa itawachanganya wakiwa viongozi wa kirioho watakuwa wazingatie protocol za kidini sio kisiasa sababu ni viongozi wa kidini sio kisiasa.Ku maaproach Magufuli kwa angle ya kidini anatakiwa kuzingatia protocol ya kidini kama wewe kiongozi wa dini lakini kama wewe wa kisiasa ruksa kupitia angle ya kisiasa .Hawa maaskofu wakosoaji wa Magufuli kisiasa wakati wao viongozi wa dini hawajielewi na Uaskofu wao walipewa kimekosa labda walihonga
 
Hawa maaskofu so boring.mitaani unasikiliza siasa unasema ngoja nibadili mkao nimechoka siasa ngoja niende kanisani unafika kanisani unakutana na siasa tena .stupid
Yaani...hata mimi mpenzi wa Simba, siku Simba imefungwa huwa hata sitaki kusikiliza kipindi cha michezo na kusoma magazeti ya michezo. Lakini siku Simba ikishinda, weee, nitataka kusikiliza michezo redio hii, kisha nitataka kujua wengine wameisimuliaje habari hiyo. nitataka kuwasiliana na watu mbalimbali ili kujua magoli yalifungwaje. Pole sana maana ulitarajia Magufuli atasifiwa. Jamaa kampa za uso, tena mbele ya vyombo vya habari. Waaaoooo, sijui Pengo atajisikiaje??
 
Huelewi wewe unachoongea.

Chini ya sheria ya Kanisa Katoliki, Canon Law, kuna mambo ambayo askofu wa jimbo moja hawezi kuyafanya katika jimbo jingine. Mambo hayo ni ya kiutawala tu na siyo mambo ya kiroho. Kanisa katoliki ni moja tu, na ni familia moja inayofuata imani moja. Maaskofu wote ni mapadre. Maaskofu hawawekwi wakfu. Daraja la upadre ndilo linalotoa mwongozo wa mafudisho ya kiroho. Hakuna Askofu wa Kanisa Katoliki ambaye anayweza kuleta mafundisho ya kiwendawazimu ya kusema kuwa kwa nini unamuonya muumini wa jimbo langu kuacha uovu.

Kanisa linakamilika kwa kutumia karama zilizomo ndani ya kanisa. Wengine ni waombaji wazuri lakini ni dhaifu wa kukemea. Wengine wana karama ya uponyaji lakini hawajui kuomba. Wengine ni manabii lakini siyo walimu wazuri, n.k. Karama hizo za viongozi ndizo zinazolijenga na kulikamilisha Kanisa.

Inaelekea unapungukiwa sana na uelewa wa muundo wa Kanisa Katoliki, mafundisho yake, elimu ya biblia na sheria ya Kanisa Katoliki. Muundo wa TAG ni tofauti kabisa na Kanisa Katoliki. TAG kila kanisa linajitegemea wakati Kanisa Katoliki lote ni familia moja iliyo chini ya Mama Kanisa mmoja. Mipaka ya majimbo ni mipaka ya kiutawala lakini siyo mipaka ya mafundisho au imani.
Kama ni hivyo kunahitaji Reformation kanisa katoliki tena kubwa yaani INA maana padre wa patokia au Askofu askofu wa jimbo aweza toa tamko LA katoliki LA dunia akiwa parokia yake au jimbo badala ya papa? Kuna tatizo
 
Usichanganye uumini na uraisi Magufuli kwa viongozi wa dini ni muumini wakichanganya na siasa itawachanganya wakiwa viongozi wa kirioho watakuwa wazingatie protocol za kidini sio kisiasa sababu ni viongozi wa kidini sio kisiasa.Ku maaproach Magufuli kwa angle ya kidini anatakiwa kuzingatia protocol ya kidini kama wewe kiongozi wa dini lakini kama wewe wa kisiasa ruksa kupitia angle ya kisiasa .Hawa maaskofu wakosoaji wa Magufuli kisiasa wakati wao viongozi wa dini hawajielewi na Uaskofu wao walipewa kimekosa labda walihonga

Hapa hao maaskofu wameongea ukweli na wala hawana sababu ya kusibiri hizo taratibu unazotaka kuzisema wewe. Kwani huo ukatili unafanyika kwa kufuata taratibu? Ukiona wameamua kuongea waziwazi ujue wameshaonya nyuma ya pazia wakapuuzwa, hivyo namna pekee ni kunawa mikono mbele ya umma. Na kwa hili wako sahihi.
 
Kama ni hivyo kunahitaji Reformation kanisa katoliki tena kubwa yaani INA maana padre wa patokia au Askofu aweza toa tamko LA katoliki LA dunia akiwa parokia yake badala ya papa? Kuna tatizo

Kwa hiyo kanisa katoliki lifanye reform ili kumridhisha rais wa Tanzania.!!? Unachekesha kweli wewe. Huu uvunjifu wa sheria uko wazi hata kama watu wanaoogopa kusema. Sheria za katoliki haziwezi kubadilishwa ili ziweze kufunika uovu. Uovu hauhitaji protocal kuukemea.
 
Askofu mzima hajui jinsi ya kukosoa muumini wa kanisa lisilo lake? Alitakiwa awasilishe malalamiko kwa Askofu pengo halafu pengo angempa feedback baada ya kuongea na muumini wake.Hivi hawa maaskofu woropokaji wasiojua protocol walipataje uaskofu kanisani kuna rushwa.hawa maaskofu nawaomba waombe wapewe semina na Kanisa LA Tanzania Assemblies of God yaani TAG wako vizuri kwenye mambo ya protocol za kikanisa.Katoliki,Lutheran, akina kakobe,Gwajima na maaskofu wote waropokaji washinikizwe kuhudhuria hata kwa viboko na makanisa yao hiyo semina.Kama hela za kuattend hawana naomba TAG idhamini bure tafadhali
mzee naona dawa imekuingia vizuri, dawa yoyote huwa si tamu iwe vidonge au sindano ispoleta kizunguzungu itakuletea kichefuchefu lakini ndio dawa cha msingi upote maladhi yako.
 
Wakuu kuna haja ya kuwaandikia hawa Viongozi wawili wa dini kwa kupongeza misimamo yao dhidi ya uchwara ili wajue kwamba kuna Watanzania wengi sana ambao tunawaunga mkono kwenye kauli zao dhidi ya utawala huu dhalimu na wa mabavu.
 
Hapa hao maaskofu wameongea ukweli na wala hawana sababu ya kusibiri hizo taratibu unazotaka kuzisema wewe. Kwani huo ukatili unafanyika kwa kufuata taratibu? Ukiona wameamua kuongea waziwazi ujue wameshaonya nyuma ya pazia wakapuuzwa, hivyo namna pekee ni kunawa mikono mbele ya umma. Na kwa hili wako sahihi.
Hawa Maaskofu wawili wameibariki Krismasi yangu nina furaha moyoni kulisema hili lijamaa.

Huu ndio uchungaji na ucha Mungu, usipokemea maovu unayoyaona wazi wazi maana yake unayaunga mkono. Huu ndio utumishi uliofanywa na Nabii Daniel, Eliya, Isaya, Yohana. Ni kuwachana live hata kama wamebeba mitutu na mabomu.
 
Back
Top Bottom