MIAKA 61 YA UHURU: Je, ni kweli wananchi hawaitaki CCM na wamewapuuza wapinzani?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
948
2,857
Heri ya kumbukumbu njema ya Uhuru wa Tanganyika na baadae Tanganyika iliungana na Zanzibar mnamo mwaka 1964 na kuzaliwa Tanzania,Bendera ya Tanganyika ilivyoanza kupepea mwaka 1961 tulishuhudia tunavyoanza kujitegemea,kila nikiusoma utenzi wa tujifunze lugha yetu,kitabu cha 7 najiona mwenye tumaini jipya juu ya nchi yangu na Taifa langu la Tanzania,najiona nina deni la kutimiza maono ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyetaka Tanzania iwe taifa kubwa kama ilivyo Cuba na China,ni miaka sitini imepita toka tupate Uhuru,nchi ya Zimbabwe,Kenya na Rwanda zimesharusha satelaiti zao angani lakini Tanzania tunawaza uchaguzi wa 2025.

Kwanza kabisa na kwa namna ya pekee niwaenzi kwa kuwakumbuka mashujaa wetu waliotangulia mbele ya haki,mlifanya yaliyo mema na sasa mmelala pamoja na Baba zetu,tunawaombea sana,Mtemi Isike kutoka Unyanyembe,Mtemi Mirambo (1840-1884) mtemi wa Wanyamwezi katika magharibi ya Tanzania ya leo,Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855 – 19 July 1898[a]), Wazungu walimuita"conqueror of many lands" nimemkumbuka Mtemi Kimweri ye Nyumbai,nimemkumbuka Mtemi Rumanyika wa Wahaya,nimemkumbuka pia Mtemi Nyungu ya Mawe,Mtemi Kisebengo na Mtemi Kingalu na Mtemi Msumi kutoka Morogoro,kwa namna ya pekee niwakumbuke Hayati Edward Sokoine,Hayati Julius Nyerere,Hayati Abeid Karume,Hayati Rashid Kawawa,Hayati Daktari Omary Ali Juma,Niwakumbuke The Pan Africanist,Martin Delany,Alexander Crummel,Edward Blyden,Dr William Du Bois,Dr Namdi Azikiwe,Marcus Garvey,Kwame Nkrumah,Haile Selassie,Robert Mugabe,Jomo Kenyatta,George Padmore, Julius Nyerere, Nelson Mandela,Oliver Tambo,Thomas Sankara,Patrice Lumumba and Dr John Pombe Magufuli,Mungu awapumzishe kwa amani,

Leo miaka sitini toka Uhuru hatuna umeme tunatumia jenereta asubuhi hadi giza linapoingia,ubwabwa kwa sasa tunauona tu dukani kwa mangi maana kilo moja ya mchele shilingi 3,200 toka shilingi 1,500 mwaka mmoja uliopita maharage imekuwa mboga ya anasa kutoka kuwa mboga ya wanyonge kilo moja ya maharage shilingi 3,500 toka 1,400 mwaka mmoja uliopita,Kwa shida hizo ukijumlisha na makando kando mengine ya kudhihaki waliokufa,makando kando ya ufisadi,makando kando ya wafanyabiashara ndani ya chama,kwa jinsi ilivyo mwaka 2025 chama chochote ili kishinde kinahitajika chama imara chenye sera nzuri, zinazoeleweka na kutekelezeka. Chama hicho kiwe na sura ya kitaifa, kiwe na viongozi wakweli, wenye maono ya kizalendo kwa mfano wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere,Hayati Edward Sokoine na Hayati Daktari John Pombe Magufuli,pia chama kinatakiwa kiwe na misimamo thabiti ya kuikomboa nchi,chama iko kiwe na mifano hai ya utekelezaji wa sera zake kupitia chama husika ili kiweze kuaminika machoni mwa watanzania wengi.

Mwalimu Julius Nyerere alisema,tutamjua kiongozi kwa maneno na matendo yake,sio mtu useme chama chetu kina misingi ya heshima kwa viongozi wastaafu na waliokufa wakati mwenyekiti wa chama ambacho kingekuwa mfano wa heshima anakaa kimya na kufurahi pale kiongozi Marehemu anapotukanwa hadharani,sio mtu useme chama chetu ni cha maendeleo, wakati wanaoendelea katika chama ni mwenyekiti wa chama taifa na genge lake, huku wananchi wakikosa maji na Umeme na bei za vyakula kupanda,sio mtu useme chama chetu kitasimamia utawala bora na haki, huku ndani ya chama chenyewe hakuna anaeweza kuongelea lolote mbele ya mwenyekiti wa chama, viongozi wa chini wanabakia kusifu na kutukuza hadi kukufuru, kiongozi anawageuza Wananchi na wanachama kuwa machawa.

Uchaguzi wa 2025 unahitajika kuchaguliwa mgombea ambae hana makandokando ya uongo, uoga, unafiki na mwenye uwezo wa kweli wa kusimamia sera za chama chake bila kuyumbishwa na mtu yoyote iwe ndani ya chama au nje ya chama,sio kiongozi anakuwa na kauli za kilaghai laghai kwa maslahi yake kisiasa, kiongozi ambaw hajali madhara yatokanayo na ulaghai wake,mtu wa aina hii ni ngumu kuchaguliwa maana watanzania wa sasa sio wale wa 2005 kugawa sahani za wali na maharage,kugawa t-shirt na kofia,Mgombea akiwa hana msimamo thabiti wa kusimamia sera au hoja zake mwenyewe, Mgombea anayesubiri kuletewa hoja na magenge wa waalifu pasipo yeye kujua,

Hakuna uchaguzi uliuokua na wapiga kura wengi kama 2015 hii ilikuwa sababu ya Edward Lowassa kuendesha harakati za mabadiliko kuongoza kundi kubwa la walalahoi waliojaa kwenye mikutano yake mfano wa mafuriko ya maji,matokeo ya kushindwa ya Mh Edward Lowassa yalifanya kundi hilo kubwa la walalahoi kukata tamaa ya kushinda milele maana chance ya 2015 ilikua realistic zaidi so walivunjika moyo kwa kushindwa kwa "rais wa mioyo"Kitu kikubwa alichofanya Rais John Pombe Magufuli ni kuririthi kundi hilo la walalahoi,Hayati Rais John Pombe Magufuli alijaribu,alijitahidi na aliweza kulichulua kundi la walalahoi wa Lowassa na kuwapa ile ladha ya mabadililo ambayo waliamini kwa Mh Edward Lowassa,Kundi la walalahoi sasa likapata mtu wa kuwazungumzia pale Ikulu,mtu huyo aliongea lugha ya wanyonge na kuwaambia mtaji wa masikini ni nguvu zao wenyewe,mtu huyo alikuwa ndiye Rais Magufuli,

-Je ni kweli Wananchi hawaitaki CCM na wamewapuuza Wapinzani!?

Jibu ni kweli kwa sababu zifuatazo;-

Ukiachana na mihemko ya humu JF na Twitter kwa baadhi, ukweli ni kwamba kwa ground,yaani mtaani mtaji wa kura ni walalahoi na wanyonge maana hao matajiri kazi yao kuhonga tu wao hawapigi kura wala hawazunguki kupiga kampeni,CCM wana mtaji wa watu wengi ambao ni tabaka la chini, kwa utafiti tu mdogo kati ya wananchi 10... wananchi 7 wanaamini maono na itikadi za Hayati Rais John Pombe Magufuli huu ni ukweli ukitembelea wananchi kama mama ntilie, bodaboda, machinga ambao hili kundi lilikuwa mtaji wa Chadema,lakini cha ajabu ndani ya CCM mtu huyo mwenye kupendwa na walalahoi ndiye mwenye kupigwa mawe,kwa maana hiyo walalahoi wenye kuamini maono ya Hayati Rais John Pombe Magufuli hawatokipenda chama kinachomtukana na kumrushia mawe shujaa wao,

Lowassa alipata kura milion 6 kutoka kwenye hili kundi la walalahoi now hili kundi limewapotezea Chadema na upinzani kwa ujumla kwa sababu kwanza wanampinga na kukejeri harakati za Hayati Daktari John Pombe Magufuli,kwa jinsi hii kundi la walalahoi Milioni 6 wa Lowassa lililolithiwa na Hayati Rais Magufuli,hawatoipigia kura CCM wala Chadema wala act,kundi hili litapiga kura kwa yule atakae nena na kutenda kama Rais John Pombe Magufuli,Wapinzani Chadema wao wanafurahia na kucheza mdundiko kila pale Marehemu anapodhalilishwa na kubagazwa wanasahau huyo Marehemu ndio alama ya mlalahoi na mnyonge aliyepiga kura ya hasira kumpa Edward Lowassa ili CCM itoke madarakani,kura Milioni sita za walalahoi zilizorithiwa na John Pombe Magufuli kwa kutimiza yale walalahoi hao waliyoyataka na kuyasubiri kwa miaka mingi,kura hizi Milioni sita leo zinachezewa na Chadema,kosa hili watalikumbuka pale kura hizi milioni sita zitapotafuta mtu wa kumpa atakaefanana kwa matendo na Hayati Rais John Pombe Magufuli.

Nimalizie kwa kuyaelezea makundi matatu ya wapiga kura yaliyopo hapa Tanzania kwenye kuamua mustakabali wa nchi kupitia demokrasia ya Uchaguzi,

- Makundi hayo ni

1) Kundi ambalo uwa upande wa chama tawala,lenyewe humpigia kura mtu aliepitishwa na chama chao ili agombee uraisi, ubunge, udiwani nk, haijalishi mgombea ana sifa nzuri au mbaya,kundi hili kwa sababu ya mfumuko wa bei kupanda bei za chakula,na ugumu wa maisha,watapiga kura ya hasira kwa mtu wanaemuamini kuja kuwatoa kwenye shida hizi,tusubiri tuone.
2) Kundi ambalo huwa upande wa vyama vya upinzani,kundi hili nalo pia huwapigia kura watu waliopitishwa na vyama vyao ili wagombee uraisi, ubunge, udiwani nk. Haijalishi wagombea hao wana sifa nzuri au mbaya,kundi hili nalo kwa sababu ya njaa na ugumu wa maisha uliopo sasa,litapiga kura kwa yule wanaemuamini kuja kuwaletea suluhisho la ugumu wa maisha uliopo hivi sasa.
3)Kundi la mwisho hili halina chama au linachama lakini huwa linamchagua mtu kwa kufuata tu sifa za mtu alie katika kinyang'anyiro cha uraisi, ubunge,udiwani nk kundi ndilo lile saba ya kumi lenye kuamini katika maono ya aliyekuwa Rais wa Tanzania,Hayati Daktari John Pombe Magufuli,kwa kundi hili Hayati Rais Magufuli ndio kipimio chao "measuring stick" ya uongozi bora kwa Tanzania ya viwanda, Tanzania ya uchumi wa kati, Tanzania ambayo aliiota Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,

Nimalizie kwa kusema kwamba,kama sisi tunaishi katika nyumba inayonuka mikojo lakini wenzetu wanaishi katika nyumba ambayo nyuma ya dirisha kuna shimo la choo linalotema harufu ya kinyesi,katika chama tawala kuna mafisadi, waongo, wachumia tumbo na wanafiki, na vile vile katika upinzani hivyo basi vyama vyote kuna mafisadi, waongo, wanafiki na wachumia tumbo,tutafanyaje tutaangalia mtu mwenye fimbo ya chuma ambae atawawajibisha chama tawala na upinzani huyu ni yule aliye mfano wa Chuma,Jiwe,nae si mwingine ni Rais John Pombe Magufuli.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Watu wapo kwenye masega
 

Attachments

  • IMG-20221211-WA0317.jpg
    IMG-20221211-WA0317.jpg
    111.7 KB · Views: 8
Mbowe anasema ataendelea kukaa kwenye meza ya maridhiano,anasema alikamatwa siku moja kabla ya maandamano akafungwa kitambaa akapelekwa Bagamoyo na hakuna aliyeandamana, I have a family to feed not a community to impress,ni sawa na kusema sitaki shida tena wacha nipumzike.
 
Back
Top Bottom