Askofu Shao amgeuka Magufuli, asema mizengwe kwenye uchaguzi mdogo ni ishara serikali haielewi maana ya demokrasia

YEHODAYA hivyo ni vibwagizo tu katika ujumbe sio ujumbe wa ibada, endelea tu kwenda church
iwe kibwagizo or whatever ieleweke kanisani watu wa vyama vyote na wasio na vyama ambao ndio wengi huenda na wanapoenda hawafuati vibwagizo vya kisiasa wanakotoka majumbani kwao wamevipata vya kutosha hadi kuboa wanataka vitu tofauti nje ya siasa inaudhi sana.
 
Askofu Shao aliwahi kumsifia Magufuli hadi kumfananisha na Rais wa Zimbabwe aliyeondoka madarakani Robert Mugabe

Askofu Shao amfananisha Rais Magufuli na Robert Mugabe wa Zimbabwe... ataka watanzania tumuunge mkono!

Lakini kwenye leo kwenye ibada ya Krismas iliyofanyika leo Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Zanzibar Mhashamu Augustino Shao amesema ipo haja kwa serikali kuelewa dhana ya demokrasia kutokana na mchango wake katika maendeleo ya taifa

Amesema mizengwe iliyofanyika kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani huko bara ni ishara kuwa serikali haielewi maana ya demokrasia, yaani kutofautiana

Pia amekemea watu wanaoiibia serikali na kusema hiyo ni dhambi kubwa
View attachment 658971

Ndo nani huyo?
 
hilo ni tamko la misa ya kitaifa kutoka baraza la maaskofu katoliki Tanzania kama sikosei ukweli lazima usemwe na watu wote wenye mapenzi mema na tanzania na siyo kumuhadaa kwa kumuita mzalendo
 
iwe kibwagizo or whatever ieleweke kanisani watu wa vyama vyote na wasio na vyama ambao ndio wengi huenda na wanapoenda hawafuati vibwagizo vya kisiasa wanakotoka majumbani kwao wamevipata vya kutosha hadi kuboa wanataka vitu tofauti nje ya siasa inaudhi sana.
Siasa ipo kila mahali chief.

Uwezo wa raia kuamini na kufanya ibada ni maamuzi ya kisiasa.

Leo bunge likisema nchi yetu inaanza kufuata misingi ya kijamaa na kupiga vita dini na kuabudu yatakua ni maamuzi ya kisiasa ndiyo yameamua hivyo.

Hoja yangu ni kua, kiongozi wa dini kuongelea siasa anakua hajacheza nje ya uwanja.
 
hilo ni tamko la misa ya kitaifa kutoka baraza la maaskofu katoliki Tanzania kama sikosei ukweli lazima usemwe na watu wote wenye mapenzi mema na tanzania na siyo kumuhadaa kwa kumuita mzalendo
Askofu mzima hajui jinsi ya kukosoa muumini wa kanisa lisilo lake? Alitakiwa awasilishe malalamiko kwa Askofu pengo halafu pengo angempa feedback baada ya kuongea na muumini wake.Hivi hawa maaskofu woropokaji wasiojua protocol walipataje uaskofu kanisani kuna rushwa.hawa maaskofu nawaomba waombe wapewe semina na Kanisa LA Tanzania Assemblies of God yaani TAG wako vizuri kwenye mambo ya protocol za kikanisa.Katoliki,Lutheran, akina kakobe,Gwajima na maaskofu wote waropokaji washinikizwe kuhudhuria hata kwa viboko na makanisa yao hiyo semina.Kama hela za kuattend hawana naomba TAG idhamini bure tafadhali
 
Hawa maaskofu so boring.mitaani unasikiliza siasa unasema ngoja nibadili mkao nimechoka siasa ngoja niende kanisani unafika kanisani unakutana na siasa tena .stupid

Tena hao viongozi wa dini wamechelewa sana kuongea na tunawalaumu sana kwa hilo. Ule unyama uliofanyika juzi kwa kukata watu mapanga huku umma ukishuhudia nilishangaa sana viongozi wa dini kukaa kimya. Inafikia mahali mpaka DC na RC anaingilia uchaguzi eti ili Magufuli afurahi na kuonyesha anapendwa. Hao viongozi wa dini wameamua kuonyesha ukweli na hiki kitendo cha wapinzani kususia uchaguzi kimewaamsha wengi kwenye usingizi mzito.
 
Askofu mzima hajui jinsi ya kukosoa muumini wa kanisa lisilo lake? Alitakiwa awasilishe malalamiko kwa Askofu pengo halafu pengo angempa feedback baada ya kuongea na muumini wake.Hivi hawara maaskofu woropokaji wasiojua protocol walipataje uaskofu kanisani kuna rushwa.hawawa masskofu nawaomba waombe wapewe semina na Kanisa LA Tanzania Assemblies of God yaani TAG wako vizuri kwenye mambo ya protocol za kikanisa.Katoliki,Lutheran, akina kakobe,Gwajima na maaskofu wote waropokaji washinikizwe kuhudhuria hata kwa viboko na makanisa yao hiyo semina.Kama hela za kuattend hawana naomba TAG idhamini bure tafadhali

Inaonekana hujui utaratibu wa kanisa katoliki, Pengo ni kardinali na sio boss wa maaskofu wakatoliki Tanzania. Hata kama ingekuwa hivyo huyo Pengo ndio aambiwe ili afunike unyama unaoendelea nchini? Hao viongozi wa dini wamevumilia wameona huko tunakoenda sio kwema, nchi inatawaliwa kinyama huku sheria zikikiukwa. Na bado kuna jumbe za viongozi wengi wa dini zitaripotiwa leo na kesho. Huu unyama unafanyika wazi kiasi hiki ni ngumu viongozi wa dini kukaa kimya.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom