Uchaguzi 2020 Askofu na Sheikh wamwaga dua nzito dhidi ya watakaofanya dhulma katika Uchaguzi huu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,501
51,093
Katika mkutano wa Chadema leo Kawe, Askofu Mwamakula na Sheikh Katimba leo wametoa dua nzito sana dhidi ya mtu yeyote atakayetenda dhulma kudhulumu haki za watanzania kwenye kupata viongozi wao halali wa nchi hii.

Askofu Mwamakula amesoma dua nzito ya kuomba Mungu ashushe Malaika wawashughulikie wote watakaojaribu kupora haki za watanzania kuchagua wawatakao. Ametoa mfano wa namna Malaika walipopambana na majeshi ya Ibilisi na kumnyang'anya funguo za kuzimu.

Sheikh Katimba akaomba Mungu amdhalilishe mtu yoyote atakayekula njama za za dhulma ya haki za wananchi, ameomba Mungu amdhalilishe hapahapa duniani na huko Mbinguni

Mimi nasema hawa viongozi wa kitaifa, viongozi wa CCM, VIongozi wa NEC na wote wanaokula njama za kuvuruga uchaguzi MWENYEZI MUNGU ANAONA, LAANA HAZITAWAACHA SALAMA IWAPO MTATEKELEZA UDHALIMU HUU!

Mwaka 2015 Mkuu wa nchi wakati anaapishwa pale uwanja wa Taifa kuwa rais, alisomewa dua na Askofu na Sheikh dua nzito huku akiapa kuwa mtenda haki na kutoonea wala kubagua. Sasa Dua za Mungu huwa haziendi bure, namshauri ajipime aone kama amekiishi hiki kiapo. Viapo mbele ya Mungu ni vizito!

Nimkumbushe tu Rais Magufuli kuwa siku anaapishwa pale Uwanja wa Taifa, Sheikh Mkuu alimsomea dua nzito sana akiambatanisha dua hiyo na aya Nzito kuliko zote kwenye Qu'ran aya ya Mamlaka ya Mungu (Ayatul' Kursiyyu). Hii ni Aya yenye Ulinzi mzito!, Waislamu huitumia aya hii kwenye kujilinda dhidi ya mamlaka za Ibilisi, uchawi, wenye nia mbaya n.k. Na kweli Mungu kamlinda Rais katika Mengi mpaka sasa. Lakini nimkumbushe tu mheshimiwa rais kuwa Qur'an huwa haichezewi chezewi, Mwisho wake siyo Mzuri. Ni bora atende haki la sivyo Mungu hadhihakiwi!, Adhabu yake ni kali!

Maamuzi ni yake atekeleze kiapo chake au akivunje!. Mungu anamuona!
 
Shehe kaongea kwa uchungu Sana nimeona
Baada ya Magufuli kuapishwa pale uwanja wa Taifa mwaka 2015 alisomewa Aya nzito sana na Sheikh Mkuu iitwayo Ayatul Kursiyyu hiyo ni Aya kuu ya ulinzi ndani ya kwenye Qur'an kuliko zote ili Mungu ampe ulinzi akatende haki, sasa ngoja aende nje ya viapo alivyoapa pale uwanja wa Taifa mwaka 2015 aje aone mwisho wake!.
 
Chadema kinatia huruma kutoka kuombewa Dua na masskofu wenye hadhi Kama Kakobe na Gwajima Hadi kuombewa Dua na Askofu mwamakula mwenye kanisa la mfukoni na shehe ubwabwa Katimba
 
Hakuna impact yoyote ya dua wala sala/maombi yanayoweza kufanya chochote. Walipiga dua miaka ya 95 na mpaka 2030 zitapigwa dua..na hakuna kitakacho tokea
 
Chadema kinatia huruma kutoka kuombewa Dua na masskofu wenye hadhi Kama Kakobe na Gwajima Hadi kuombewa Dua na Askofu mwamakula mwenye kanisa la mfukoni na shehe ubwabwa Katimba
Samahani hivi kaakobe na unoboy kifisiemu ni "masskofu" wakubwa? ila kizuri umetofautisha maaskofu na masskofu!!!
Masskofu inatafsirika kama "mass coffin" tumekuelewa
 
Siku ya kupiga kura...Mawakala wa Upinzani kuzuiwa kuingia kwa wakati...ili waingize kura feki kwanza

Hilo linakuja....

Mawakala wa Upinzani siku ya Kura...kufanyiwa kitu mbaya
 
Tumekuwa na chaguzi nyingi chini ya mfumo wa vyama vingi tangu 1995 lakini kamwe hatujawahi kushuhudia uharamia wa kuwapoka wapiga kura haki yao ya Kikatiba ya kuchagua viongozi wao kupitia sanduku la kura.

Mwaka 2019 tulishudia hujuma katiaka mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa zaidi ya asilimia 90 ya wagombea wa vyama vya upinzani kuenguliwa wasigombee.

Hujuma hii ilipelekea vyama vya upinzani kujitoa katika uchaguzi huo feki. Mwaka huu tunashuhudia tena uharamia kama ule wa mwaka wa jana na huu ukiwa umeboreshwa kwa kuongeza matumizi ya vyombo vya dola kama vile Polisi na TAKUKURU katika kutekeleza uharamia huu.

Kwa akili ya kawaida tu ni dhahiri kuwa uharamia huu ni utekelezaji wa azimio la Serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa inairudisha nchi katika enzi ya ujima wa utawala wa chama kimoja. Watanzania kwa mamilioni wamehuzunishwa na uharamia huu na kujiona kama mateka wa kikundi kidogo cha Watanzania wenzetu walioamua kufurahisha matakwa yao hata ikibidi kwa gharama ya damu za Watanzania wenzao.

Kwa vile sisi wahanga wa uharamia huu hatuna majeshi na bunduki kama wao tunamuachia Mwenyezi Mungu awe hakimu wetu.
 
Chadema kinatia huruma kutoka kuombewa Dua na masskofu wenye hadhi Kama Kakobe na Gwajima Hadi kuombewa Dua na Askofu mwamakula mwenye kanisa la mfukoni na shehe ubwabwa Katimba
Ujue kuna maisha baada ya uchaguzi. Usijitoe ufahamu kiasi hiki. Tanzania ni ya Watanzania wote na si ya kikundi kidogo cha watu.
 
Njaa tu hizo hakuna kiongozi wa dini atahangaika na wanasiasa.
Nivemba watapoteana.
Enzi zetu na Mzee wa Kilalacha tulikuwa na Sheikh Mtopea
 
Chadema kinatia huruma kutoka kuombewa Dua na masskofu wenye hadhi Kama Kakobe na Gwajima Hadi kuombewa Dua na Askofu mwamakula mwenye kanisa la mfukoni na shehe ubwabwa Katimba
Ndugu yangu. Mungu haangalii wenye hadhi. Anaweza akamrumia hata yule ambaye hamkutarajia. Rejea mfano wa daudi.
 
Back
Top Bottom