Askofu Mwamakula: Sisi viongozi wa dini tumesitisha safari ya kwenda Mbweni na kwenda kumuona IGP Sirro!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
BAADA YA WANAWAKE WA CHADEMA KUACHIWA, SISI VIONGOZI WA DINI TUMESITISHA SAFARI YA KWENDA MBWENI NA KWENDA KUMUONA IGP SIRRO!

Jumapili tulitangaza kuwa kama siku ya Jumatatu Jeshi la Polisi lisingeliwaachia viongozi wa CHADEMA 7 na Waandishi wa Habari 2 waliokuwa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Mbweni - Dar es Salaam, sisi Askofu Mwamakula pamoja na viongozi wengine wa dini tungelifika kituoni hapo siku ya Jumanne kwa ajili ya kuwaona. Baadaye tungeliujulisha umma na dunia kwa ujumla.

Baada ya azimio letu, Viongozi wa Dini kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe kuhusu Maadili, Amani na Haki, Askofu William Mwamalanga walitoa tamko kutuunga mkono na kuahidi kuungana pamoja nasi kwenda Mbweni na pia kumuona IGP Simon Sirro. Usiku wa Jumatatu tumepewa taarifa kuwa viongozi hao waliachiwa wote Jumatatu jioni.

Baada ya taarifa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatangaza kusitisha safari yetu pamoja na viongozi wa dini tuliyopanga kwenda Kituo cha Polisi Mbweni siku ya Jumanne. Tunatangaza pia kuahirisha safari ya kumuona IGP Sirro. Tutashauriana kuhusu kupanga siku nyingine ya kuonana na IGP Sirro kuhusiana na mambo yanayoendelea nchini yakiwemo ya kunyanyasa wanaharakati na wanasiasa wa upinzani kunakofanywa na Jeshi la Polisi.

Tunapenda kuwashukuru wote walioshiriki kusambaza ujumbe wetu, walioshiriki kupaza sauti kwa njia mbalimbali na waliokuwa tayari kutuunga mkono kwa kutaka kutusindikiza sisi viongozi wa dini. Pamoja na kutiwa moyo na hatua ya Jeshi la Polisi kutokana na kusikia kelele za umma na kuamua kuwaachia, tunaendelea kutoa wito kwa Jeshi la Polisi kutokuwasumbua kwa lo lote viongozi hao kuhusiana na kukamatwa kwao.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

9823ADA6-EEE9-4AB0-8DF1-6070C5EFAFF9.jpeg
 
Tunapenda kuwashukuru wote walioshiriki kusambaza ujumbe wetu, walioshiriki kupaza sauti kwa njia mbalimbali na waliokuwa tayari kutuunga mkono kwa kutaka kutusindikiza sisi viongozi wa dini.

Pamoja na kutiwa moyo na hatua ya Jeshi la Polisi kutokana na kusikia kelele za umma na kuamua kuwaachia, tunaendelea kutoa wito kwa Jeshi la Polisi kutokuwasumbua kwa lo lote viongozi hao kuhusiana na kukamatwa kwao.
 
Juhudi za baadhi ya Viongozi wa dini katika kupambana na hawa wahuni zinanipa matumaini makubwa sana kuhusu ukombozi wa nchi yetu kutoka kwa hawa majizi na madhalimu wanaofilisi nchi yetu kwa miaka chungu nzima sasa. Mwenyezi Mungu awape maisha marefu afya njema na awabariki sana. 🙏🏾

Tunapenda kuwashukuru wote walioshiriki kusambaza ujumbe wetu, walioshiriki kupaza sauti kwa njia mbalimbali na waliokuwa tayari kutuunga mkono kwa kutaka kutusindikiza sisi viongozi wa dini. Pamoja na kutiwa moyo na hatua ya Jeshi la Polisi kutokana na kusikia kelele za umma na kuamua kuwaachia, tunaendelea kutoa wito kwa Jeshi la Polisi kutokuwasumbua kwa lo lote viongozi hao kuhusiana na kukamatwa kwao.
 
Hawa ndio watakaompigia kura mwanamke mwenzao hapo 2025?

Heshima kwenu akina mama. Historia ya nchi hii itaonyesha kwamba mlitoa mchango wenu katika kuitafuta HAKI.

Himizeni akina mama wenzenu nao waungane nanyi katika ukombozi wa nchi yetu.

Kuhusu viongozi wa dini. Hao wengine wanaokaa kimya juu ya uonevu wa namna hii wao pia watatambuliwa kwa kusaliti taifa lao.

Haiwezekani wakae kimya kana kwamba hawaoni ubaya wowote wanaofanyiwa waumini wao na raia kwa ujumla. Hata kusema neno tu hakuna? Hizi ni dini za kitu gani.
 
Kwa hiyo Polisi waliamua kuwakamata tu kuwaweka rumande na kisha kuwaachia Bila kuwapeleka Mahakamani.
Ifike mahala kuwe na sheria ya kuwabana Hawa Polisi waache tabia yao ya hovyo ya kukamatakamata watu wasiokuwa na hatia
Si huo ndio uonevu wa kusikitisha sana? Na wapuuzi hao hawawezi kfikishwa mahakamani kwa uonevu wa aina hii? Yaani wao wako juu ya sheria, hakuna wa kuwahoji juu ya matendo yao?
Hii ni nchi ya binaadam au wanyama pori?
 
Nayaheshimu sana majeshi yetu lakini nawachukia sana polisi, na ninamchukia zaidi Simon Sirro, but I also pity Madam President.

Hivi ni kwamba Samia hajui kinachofanywa na hawa dhalimu, ni maagizo toka kwake, au ndo kama wanavyosema watu kwamba "...wanaoendesha nchi ni watu wengine"?

No... nimwache Kamanda Sirro; ushenzi wa aina hii usingekuwa unatokea pasipo na baraka za rais wa nchi!! Na wala siamini kwamba SSH anakerwa na udhalimu huu, kwa sababu, kama angekuwa anakerwa, alitakiwa from Day One kutorithi Baraza la Usalama wa Taifa la mtangulizi wake!!

Huwezi kutegemea kitu tofauti toka Baraza la Usalama wa Taifa ambalo miongoni mwa wajumbe wake ni IGP yule yule na TISS DGI yule yule!!

Baraza la Usalama wa Taifa limegeuka kuwa Baraza la Usalama wa CCM... yaani CCM Security Council!
 
Juhudi za baadhi ya Viongozi wa dini katika kupambana na hawa wahuni zinanipa matumaini makubwa sana kuhusu ukombozi wa nchi yetu kutoka kwa hawa majizi na madhalimu wanaofilisi nchi yetu kwa miaka chungu nzima sasa. Mwenyezi Mungu awape maisha marefu afya njema na awabariki sana.
Wanachofanya sasa ni legacy moja kubwa sana huko mbeleni na kumbukizi isiyofutika
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
... ukiona hadi wanawake wamejaa ujasiri; hawajali wala kuogopa kuwekwa ndani kwa sababu ya kutetea HAKI hayo ni maandishi ukutani CCM mjipange.

Hakuna namna ya kuzuia mabadiliko maana chachu ile kidogo tonge zima lachachuka sasa. Mtafunga wangapi? Hakuna namna ni sote kuishi pamoja kama watanzania vinginevyo ubaguzi wa kichama utaliangamiza taifa.
 
Kwa hiyo Polisi waliamua kuwakamata tu kuwaweka rumande na kisha kuwaachia Bila kuwapeleka Mahakamani.
Ifike mahala kuwe na sheria ya kuwabana Hawa Polisi waache tabia yao ya hovyo ya kukamatakamata watu wasiokuwa na hatia
Hiyo sheria itajileta ?
 
Kwasasa tumeanza kupata hamasa ya kuandamana maana hasira zinazidi kuongezeka maana ukichaa unakaribia 'every body is mad and that the degree of madness is measured when angry'
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hawa ndio watakaompigia kura mwanamke mwenzao hapo 2025?

Heshima kwenu akina mama. Historia ya nchi hii itaonyesha kwamba mlitoa mchango wenu katika kuitafuta HAKI.

Himizeni akina mama wenzenu nao waungane nanyi katika ukombozi wa nchi yetu.

Kuhusu viongozi wa dini. Hao wengine wanaokaa kimya juu ya uonevu wa namna hii wao pia watatambuliwa kwa kusaliti taifa lao.

Haiwezekani wakae kimya kana kwamba hawaoni ubaya wowote wanaofanyiwa waumini wao na raia kwa ujumla. Hata kusema neno tu hakuna? Hizi ni dini za kitu gani.
Acha uwongo wako, mtu mzima ovyoo sana wenzenu kina maria sarungi wana tengeneza michuzi hawa sura zimewapa ukaa jua!
msidanganyike
 
Back
Top Bottom