Kampuni ya DP World ambayo katika Mkataba wa Bandari kati ya Ufalme wa Dubai na Serikali ya Tanzania ndiyo imepewa kuendesha Bandari zote Tanzania Bara (Tanganyika) inatumia faida inayopata katika biashara zake kusaidia misikiti na Waislamu kwa ujumla.
Mwaka huu wakati wa mfungo wa Radhamani, wawakilishi wa DP World walitembelea Mbeya ambako waliahidi kujenga Msikiti wa Masjid Al Jumaa na misaada mbalimbali. Baada ya hapo walisema wanakwenda Zanzibar ambako nako pia watafanya hayo hayo.
Video:
Video hii imerekodiwa kwa lugha ya Kingereza na Kiswahili na ilichukuliwa Mkoani Mbeya! Je, ulijua kuwa Kampuni ya DP ina malengo pia ya kukuza Uislamu mahali popote pale inapokuwa duniani? Je, ulijua kuwa DP World ina malengo ya kidini? Je, unafikiri hii ndiyo sababu Sheikh Mwaipopo alitoa kauli kali ya kutisha na kuonya Waislamu wasihudhurie Mkutano wa Temeke wa 23 Julai 2023 uliolenga kujadili na kuhoji Mkataba wa Bandari unaolalamikiwa sana?
Je, unafikiri kwa nini wawakilishi wa DP World walipofika hawakutembelea Makanisa, viwanja vya michezo, vyuo vikuu badala yake waliamua kutembelea Misikiti na kuahidi kutoa misaada huko? Je, faida watakayopata DP World katika kuendesha Bandari zetu itatokana na Kodi za Waislamu pekee?
Je, unafikiri moja ya sababu za Spika Dkt. Tulia kuutetea Mkataba wa Bandari na kufikia hatua ya kuwaita wanaoupinga kuwa ni 'wapumbavu wasiosha upumbavu wao' ni pamoja na hao DP World kutembelea Mbeya na kuwasidia wapiga kura wake Waislamu kwa kuaahidi kuwajengea Msikiti wa Masjid Al Jumaa?
Usimkarikie Askofu Mwamakula kwa kuandika haya na kuweka video hii hapa, wakasikirikie DP World kwa kuweka malengo yao wazi kuwa wanasaidia misikiti na sio dini nyingine. Pia, walaumu waliovujisha video hii hadi ikamfikia Askofu. Je, ni nani sasa anayeleta udini katika mjadala huu wa Mkataba wa Bandari? Je, ni DP World au wanaoupinga Mkataba wa Bandari?
Je, kuweka hadharani habari hizi ni uchochezi, uhalisia au uzalendo? Je, ni kwa nini viongozi wa Serikali na CCM hawaweki wazi wananchi katika mikutano yao ya hadhara kuwa faida mojawapo ya DP World ni pamoja na kujenga misikiti na kusaidia Uislamu? Je, ni kwa nini hili linafichwa wakati liko wazi hata katika malengo ya DP World? Kama Serikali haikujua malengo hayo, Waarabu hao wangesafiri hadi Mbeya kwa kificho na kuahidi kujenga misikiti nchini?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 26 Julai 2023; 07:55 am.
Habari zaidi, soma: