gollocko
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 2,945
- 2,283
Hebu tafadhari sana hebu njoo unipe habari hii ya Padre Karugendo, huyu mzee nilikuwa nashangaa kujiita Padre lakini ukimchallange kwenye Habari za Kanisa alikuwa hataki kusikia am anaonekana yuko mabali sana.
Ni muumini mzuri sana wa Mwl Nyerere, kama unataka mkosane anadika au sema jambo baya kuhusu Nyerere. Kuna watu walikuwa wakimuhusisha na uraia wa Rwanda na kwamba amekuwa akidaiwa ni moja kati ya Mashushu wa Kagame nchini petu. Ni mpingaji mzuri sana wa hii serikali ya Mh Jakaya akiandikia gazeti la Raia Mwema na Mara Chache Mwananchi. Kitu ambacho nilikuwa sijui ni kwamba kumbe amewahi kuwa Padre wa Kanisa Catholic na ati alifukuzwa....!!!
Je ni nini kosa/Chanzo, kwanini hataki kujihusisha na masuala ya kanisa, je mpaka sasa ni muumini wa kanisa gani?.... Mkuu gollocko mara apatapo notification hii tafadhari kwa haraka jongea hapa utoe ufafanuzi au kwa mkuu yeyote anayemjua huyu Bwana P. Karugendo msaada tafadhari...
BACK TANGANYIKA
Mkuu Respect, Padri Privatus Karugendo alikuwa Padri toka mwaka 1981 mpaka 2009 pale Papa alipomvua daraja hilo la upadri, iansemekana alikuwa na ugomvi na askofu wa jimbo la Rulenge Sevelin Niwemugenzi hasa katika matumizi ya huduma ya uponyaji ambayo walikuwa wameianzisha kanisani hapo na askofu aliyekuwa kabla ya huyo Niwemugenzi na ndipo suala lake(Karugendo) la kuunga mkono matumizi ya kondomu kwa wanandoa lilipofika kwa Kadinali Pengo, hii ilipelekea Karugendo kusimamishwa kuhudumu altareni ili uchunguzi ufanyike, aliposimamishwa alimuandikia barua Papa kujieleza ambayo ilitafsiliwa kama ni kukata rufaa na hivyo kuonyesha utovu wa nidhamu. Na vilevile wakati kasimamishwa alipata kuoa na kupata watoto hivyo ikambidi Papa kumvua daraja la upadri hiyo mwaka 2009. Kama unavyojua Upadri ni sakramenti ukishapigwa muhuli wake haufutiki, hivyo Karugendo anasakramenti ya upadri lakini hawezi kupanda tena altareni.