BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Tofauti za dini zilishindwa kutugawa. Serikali haina dini na hakuna anayelazimishwa kuwa na dini. Tofauti za makabila zilishindwa kuligawa Taifa. Makabila madogo yana fursa sawa kama makabila makubwa. Faida ya makabila ni kutambika na kufanya fujo katika misiba ya watani.
Tofauti ya rangi ya ngozi ya mwili haikuligawa Taifa. Baada wa kupata uhuru, baadhi ya waliokuwa wanaitwa wakoloni waliteuliwa kuwa mawaziri. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja. Tofauti za vipato hazikuligawa Taifa. Tajiri na maskini wanaweza kunyea ndoo moja huko mahabusu. Utajiri ni wa mtu lakini umaskini ni wa Taifa. Aliyewapa hawa ndiye kawanyima wale.
Tofauti za kiitikadi zinaligawa na kulisambaratisha Taifa letu. Kwanini?
1. Tofauti za kiitikadi zaweza kukutia hatiani au kukuweka huru.
2. Tofauti za kiitikadi zaweza kukupa au kukunyima maji ya bomba, barabara, HOSPITALI na
Shule.
3. Tofauti za kiitikadi zaweza kumpa uongozi kichaa na kumnyima Profesa kazi hiyo. Chama kinakuwa bora kuliko mtu. Hatuko salama.
4. Chama kinakuwa na nguvu kuliko Muumba. Mmoja amependekeza akishinda atabadili jina la nchi liwe la chama chake! Mitume hawasikilizwi lakini makada wanashangiliwa. Ukame ukija tusitafutane.
Viongozi wa dini ombeeni na kugawa baraka kwa rangi zote. Wanyambo walisema "Lisha mbwa wote washibe kwa usawa na bila upendeleo maana hujui ni yupi atakayewinda vizuri na kupata mawindo". Na watani wangu wa Tarime husema, "Asiyetembelea kwa mtemi huwa ananungunika eti mtemi ni bahili".
Baba Askofu Bagonza.