Wewe hata kujitambua hujitambui. Njaa mbaya sana! Angalia ulivyopoteza utu wako na kudharaulika kila kona Nchini.
Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka, Yakafuata Mashirika, Sasa ni Zamu ya Media Ina-suffer!
Mimi mwenyewe na kale kajikampuni kangu ka PPR, ambapo tulibamba sana tenda za serikali, mwanzo tulikuwa na wafanyakazi 20, tukipangisha jengo la NHC pale Mtaa wa Mkwepu kwa kodi ya pango kwa mwezi, ya zaidi ya mshahara wa DC, sasa hakuna tena tenders za serikali, serikali inatangaza moja kwa moja na TBC, mwaka huu pia tenda zangu za kutangaza Maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane zimefutwa, hivyo tumepunguza wafanyakazi 15!, tumebaki 5!. Na Mtaa wa Mkwepu hapakaliki hivyo tumehama, tumehamia jengo la Posta House kwenye kajichumba.