Askofu Bagonza: Sio Kila Wakati tutakuwa na CDF kama Jenerali Mabeyo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,116
49,840
Mjumbe hauwawi,someni wenyewe hapa 👇

---
Askofu wa Dayosisi ya Karagwe KKKT Dkt. Benson Bagonza ameeleza hayo kupitia waraka alioutoa kufuatia yale aliyoeleza CDF mstaafu Jenerali Venance Mabeyo kupitia mahojiano yake na kampuni ya magazeti ya serikali hivi karibuni

Tanzania ingekuwa familia yangu ningeondoa zuio linalozuia kuchapisha habari za kifo, kuugua, mazishi nk) Mungu wetu hajaacha kuja kuvuna kutoka shamba lake la viongozi, alikuja, anaweza kuja na ataendelea kuja, si kila wakati tutakuwa na CDF wa aina hii (kwa wema na ubaya), laweza kutokea kosa mkajikuta mna CDF kama Kalikawe, itakuwaje, kufichaficha chakula humnenepesha panya kuliko paka.

Tuchukulie CDF kasema kweli, aje IGP aseme kweli zaidi, aje DGIS naye aseme asiyoyajua IGP na CDF, baadaye tumsikie daktari wa Mzena naye aje na ya kwake, Mjane achukie aone kwa nini nilifichwa, naye aseme, Padre, Kardinali, dereva, maabara, mwanasheria, ADC, nk nionavyo, CDF kafunua chupa na jini limetoka, tukililazimisha kurudi kwenye chupa, itapasuka, usiri ni kichaka cha maovu.


Chanzo: Jambo Tv

My Take
Jiwe gizani Kwa Maharamia Ambao Walitaka Wasigine Katiba.
 
Kumbe Dr. Mchembe wa Hayati Magufuli ni surgeon, na kama Hayati Magufuli alikuwa akiumwa moyo, basi Dr. Janabi huo ndio ulikuwa uwanja wake.
 
Back
Top Bottom