Askofu atabiri Tanzania kupigwa na Rwanda!

Status
Not open for further replies.
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!

Angetabiri kabla ya hii sintofahamu kati ya Kikwete na Kagame angalau ningepoteza muda wangu kumsikiliza... Attention seeker!!
 
Ukisoma Mathayo 24:6 inasema
Nanyi mtasikia habari za vita na tetesi za vita........taifa moja litatoka kupigana na taifa jingine...........
 
manabii wa uongo hawako kanisani hata kwenye siasa chadema ni manabii wa uongo. take it from me.
Utabiri utumbo tu huo. "Mwisho wa dunia ukikaribia watatokea manabii wa uongo nao watadanganya wengi"


-Wameshatokea wengi,
-Na wengi mnadanganyika.
 
Hakuna Jipya ndani yake 2mezoea Maaskofu kama hao kuwepo duniani.uchovu unampelekea kuota ndoto kwetu anasema njozi.
 
Huyu nadahni ni mmoja wa wale majasusi wa kagame,Ameanza kucheza na vichwa vya watu kwa kutumia mbinu za kivita kumaliza vita kabla ya kuanza.Ila tuwe makini hawa jamaa wako wengi nchini.
Je tufanyenje.
 
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!

tuwe makini na alichokisema Rev. Mtikila kuhusu kagame! huwezijua kagame kajiandaa kiasi gani na anaungwa mkono na akina nani, hatujui. ila kwasababu watz pamoja na viongozi wetu tumezoea kuchukulia mambo ya msingi kirahisi rahisi; lets wait and see!
 
Kwenye thread kama hii, kama huna busara na uvumilivu unaweza ukajikuta umejiingiza katika utata na muumba wako. Kukaa kimya kama unachocomment huna uhakika nayo ni vizuri zaidi.

Mungu iponye nchi yetu na maadui wa aina yoyote ile.
 
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!

Hawa sasa si watumishi wa Mungu tena Wanamtumikia Lowasa. Hawaaminiki tena.
 
Kunahitajika nidhamu katika masuala yanyohusu usalama wa nchi, kila neno lipimwe uzito wake kabla ya kulitamka.
 
Ninachoweza kusema kwa kifupi tu ni kuwa Mzee Emmanuel Lazaro (Askofu Mkuu Mstaafu wa TAG) ni kati ya viongozi wa dini wanaheshimika sana kwa huduma yao ya kiroho ndani na nje ya nchi. Ni mtu mzima mwenye umri zaidi ya miaka 70 na sijawahi kusikia kashfa katika utumishi wake kwa miaka zaidi ya 30 ambayo nimemfahamu. Tunaweza tusikubaliane na unabii huu aliotoa (maana tunatofautiana sana kwenye mambo ya imani), lakini hatuna pia sababu ya kumtukana, kumdhalilisha na hata kumwita nabii wa uongo au mchungaji wa mshahara kama ambavyo baadhi yetu wanafanya kwenye thread hii. Asanteni kwa kunisikiliza!
 
I will wait for you jk at the right time and i will hit you. The days of jk are numbered! Amuuliza melkior ndadaye na habirmana walitunguliwaje. Myarwanda mwembamba mrefu si wa kuchukulia vrahs hvyo. He is the beast. Jk ajiangalie na uvasco dagama wake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom