Askofu atabiri Tanzania kupigwa na Rwanda!

Status
Not open for further replies.
Ushauri kwa waumini wa kanisa lake,wajitahidi kutoa sadaka mana hiyo ni njia mpya ya kudai sadaka
 
Kama Askofu mwenyewe ndiye huyu wala sishangai.

YEYE HUYU HAPA

2.jpg
 
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!

Da! Kagame atakuwa ametusaidia sana...kuwaondoa mafisadi wa CCM!!
 
Mi najua kama nchi isipoacha ufisadi, rushwa na utawala mbovu na kumrudia Mungu kuna siku tutakung'utwa na jeshi kuchukua madaraka.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Unajua kumezuka aina fulani ya uchizi kwenye hizi dini na hao wanaojiita viongozi wanapenda sana ile situation.......ya kutaka kuaminiwa kuwa wao ndio wenye maono kuhusu nini kinaendelea taking advantage of circumstances/situations/environments........wanajua kabisa wafuasi wao hawako well informed....so they take advantage of that as well.......ili mradi tu watu waendelee kuwaamini.....hizi dini zetu zimepoteza muelekeo kwa kweli....kwani wameachiwa watu wasio na akili/ELIMU kuongoza.....na tunakoelekea ni hatari endapo tunaruhusu kauli za kipuuzi namna hii zi-surface.......persons should be responsible for what they say........
 
Kifuatacho ni yeye kumtimua aende ishi uko Rwanda.
Huwezi sema maneno ya uchonganishi kama hayo nikijua fika lengo ni kupata umaarufu!
 
Angesema tunashinda ungeamini? mbona mnapinga msichokijua? kama ni la Mungu hakuna awezaye kuzuia lakini kama ni la kwake pia Titania. hakuna sababu ya kuanza kutukana au kudharau.
 
Alilosema Askofu sio Jambo la kustaajabisha.Utabiri ulikuwepo tangu Enzi za Baba wa Imani-IBRAHIMU.Cha Msingi ni kumwomba atusaidie njia ya kuepuka Kichapo.Hata ukitafakari kwa Makini tu bila hata Utabiri utagundua Tanzania sio Salama.Vyama vimeamua kujitafutia Ulinzi binafsi baada ya Serikali kushindwa kuwalinda,Mipaka ipo wazi kwa kila Mhamiaji Haramu kama ana Rushwa ya Kuhonga,Wasomali,Wanyarwanda,Wakenya na Waganda wamejipenyeza na kushika nafasi Nyeti Serikalini na kwenye Vyama.Kwa ujumla Nchi haina umoja na Mshikamano aliotuachia Mwalimu.Katika Mazingira kama hayo ndipo unapoona umuhimu wa kutopuuza Utabiri wa Baba Askofu.
 
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!

kichaa sio lazima aokote makopo
 
Angesema tunashinda ungeamini? mbona mnapinga msichokijua? kama ni la Mungu hakuna awezaye kuzuia lakini kama ni la kwake pia Titania. hakuna sababu ya kuanza kutukana au kudharau.

Support! Chukua 5

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Napata Hasira sana niwaonapo wachungasanaji njaa na wapuuzi kama hawa.... Hakika wanaruzalilisha wakristo.
mkuu huyo sio Mkristo ni Freemasons.askofu gani hicho cheo kajipa mwenyewe!
 
naamini katika mungu na siamini katika manabii mamluki kikubwa mungu ibariki tanzania mungu tubariki sisi watanzania amen.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom