Askofu atabiri Tanzania kupigwa na Rwanda!

Askofu atabiri Tanzania kupigwa na Rwanda!

Status
Not open for further replies.
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!


Huyo Askofu Magumashi baada ya kusema hivyo watu waliendelea kumsikiliza???
 
sasa wewe unafurahia kupigwa? Au unamaanisha nini,

ngoja tupigwe ili siku nyingine tuache unafiki. Jk hana washauri wazuri mara nyingi huwa anaongea bila kutafakari hii siyo mara ya kwanza.
 
ngoja tupigwe ili siku nyingine tuache unafiki. Jk hana washauri wazuri mara nyingi huwa anaongea bila kutafakari hii siyo mara ya kwanza.
Nadhani hujui unachokisema wewe, ulitaka asemaje?
 
naona mnamtetea dhaifu wenu. Ukweli unabaki palepale jk alikchemka. Angeweza kuongea naye private na siyo kama alivyofanya. Kagame amefanya vizuri kumjibu vizuri kavukavu.

Wewe na askofu wako wote akili moja.haya bwana akakuombee
 
Watu wangu walioitwa kwa jina langu wakitubu wakiziacha njia zao mbaya wakinirudia nitaiponya nchi yao.
 
Nchi isito isha vituko. Kila mtu kwakua ana uhuru wa kusema, basi wanaamua kujilopokea. Nafikiri sheria ipitishwe dhidi ya hawa watu wanaopenda kulopoka
 
Huyo si askofu wala lolote ni political opportunist na anacheza na akili za watu kwa kuangalia mwelekeo wa matukio.
Utabiri wake ni wa kijinga, kishetani na wa kulea mimba yake (tumbo). Ni -------- aliyeshindwa kujifunza toka kwa wenzake walioaibika hapo nyuma na anajaribu kupata umaarufu wa bei poa.
Yupo mwenzie aliyekuwa maarufu zaidu yake ambaye baada ya kufutilia kampeni za miaka fulani hapa nchini na kuona mvuto wa watu kwa mgombea aliyekuwa anampenda aliwahi kutabiri kwamba ni lazima mgombea wake toka upinzani angeshinda, na kama asingeshinda basi mungu 'atakuwa' hayupo. Katika uchaguzi ule mgombea wa CCM alimshinda kwa kishindo yule mgombea wa yule 'askofu'.
Mwaka wa jana tu yupo mwingine alijiaibisha kwa kumtabiria Odinga ushindi dhidi ya Kenyatta; yaliyotokea wote tumeyashuhudia. Askofu huyu hana tofauti na waganga wapiga ramli na upo uwezekano wa yeye kutumika kama chombo cha propaganda cha adui.
Tanzania haina shida ya vita na Rwanda kwa sababu za kitoto na kipumbavu za eti kwa nini imemshauri jirani akae meza moja na hasimu wake wamalize migogoro yao bila kumwaga damu ya wananchi wasio na hatia!
Ushauri kama huohuo ulitolewa tena na Rais wa Marekani Barack Obama na hatukumsikia mbabe huyu akimtisha.
Ukweli ni kwamba endapo Dikteta wabKigali ataamua kuivamia Tanzania kwa sababu ya kipuuzi; hata wananchi wake watamgeuka na ndiyo utakuwa mwisho wake. Rwanda inafahamu fika kwamba Tanzania si DRC ambayo imekuwa mhanga wa kila aina ya manyanyaso toka kwa Dikteta huyu mpenda vita na asiyetaka kukosolewa kamwe!
Binafsi sipendi namna nchi yetu inavyoendeshwa humu ndani, naamini tungeweza kufanya vema zaidi tungekuwa na serikali ya chama tofauti na hiki (CCM), lakini hilo likitokea sote tutaungana na kuwa wamoja bila ya kujali u-CCM, CHADEMA, CUF au NCCR.
Ni kawaida yao madikteta duniani pote, wakishalewa mvinyo mkali wa madaraka kuweweseka na kwenda kuangukia ncha za mikuki!
Hitler, Musolini, Iddi Amin na wengine kibao ni mfano; na kwa kweli Iddi Amin amekufa akijilaumu kwa nini alimchokoza jirani aliyelala!
 
Heee! Askofu anaacha kuhubiri dini anakuwa mtabiri. Hii sasa ni balaa.
 
watu mbona wantoa Povu sana? vita si ukubwa wa aridhi, vita ni mbinu
Ila ujue huwezi ingia vitani bila kujua sababu ni nini mie hapo sijapata picha, iddi amini alitaka sehemu ya TZ, Malawi wanataka sehemu ya ziwa, Je Rwanda inataka nini TZ, ujue Warwanda wametoka kwenye vita amabyo matokeo yake bado wanayasikilzia sidhani kama watkuwa tayari kuingia vitani kwa sababu za kijinga, wakati wanafikiria kujijenga
 
mkuu wetu kataka mwenyewe.Kwanza atatue na adumishe amani inayotoweka hapa Tanzania.Sio kwenda na kuongea huko nje kama vile sisi tupo salama.mbona hapa kuna madaktari wa hiari wanaong'oa meno, kucha,kutoboa macho.kuua raia wasio na haki,kwanza atuambie kwa nini alianzisha kikundi cha kigaidi[intarahamwe ya Tanzania] kilicho anza kazi kule igunga.Kikaendelea na kazi Arusha.Toa boriti kwenye jicho lako ,ndio uende ukatoe kibanzi kwa mwenzako.Tanzania amani imetoweka kila mtu ana jua hilo na serikali yako mkuu imekaa kimya sana.Vile vile husiizarau Rwanda hata kidogo.Rwanda wanapata training kutoka USA.Na wana vifaa vya kisasa zaidi ya Tanzania.Tusiangalie idadi ya jeshi, hapana.Angalia vifaa na technology.Tusipoteze muda kuingia kwenye vita.Sisi sasa vivi tuna vita moja tu kuiondoa ccm na kujenga uchumi hatutaki kuingia vitani na kuwa na amdeni kibao.Kila mtu awe balozi na aseme hatutaki vita.Kagame tutaongea nae kama ndugu yetu tu.Tanzania tumerudi nyuma sana.tujifunze faida ya vita ni ipi?.Hawa ccm wanataka kutumia hii mbinu tusifanye uchaguzi 2015.Na kumpa kikwete aendele kuwa kiongozi kwa miaka mingine ya dharura.
 
Hilo ndio Tatizo la maaskofu waliopewa uaskofu sabbu aliweza kufungua kakanisa...sio mara yakwanza kuskia unabii huo wa maaskofu Uchwara...akamuulize shekhe...nini maana na faida ya utabiri/unabii pasipo roho nakweli atamwambia.
 
Mimi huwa napingana na hoja dhaifu za CCM haswa kwenye ufisadi, kusamehe kodi hovyo, kukua deni la taifa bila maendeleo yanayoendana na deni n.k Hizi ni changamoto zetu za ndani, tunarumbana kwa hoja,tunakosoana na pengine kudhauriana lakini mwishowe tunaendelea na safari yetu ya kuijenga Tanzania na kupambana na wanaotaka ibomoke. Linapokuja suala la kimataifa, mguu wetu wa kusimamia ni mmoja tu yaani Tanzania.Huyo Askofu ajichunguze maana hata Sheikh Yahya alisahau kujitabiria kifo chake mwenyewe.Tanzania haina mgogoro na Rwanda ila Mhe.Kikwete ana mgogoro na Kagame hivyo wakigombana wawili wao binafsi, hatujui atapigwa nani lakini ikiwa ni Tanzania Vs Rwanda hata hatuhitaji Sheikh Yahya kutabiri kwamba tunaweza kuichakaza Rwanda ndani ya 48hrs.
 
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!

Huyu askofu namwaminia. Huyu siyo mtu wa njaa. Ni miongoni mwa maaskofu wenye hofu ya Mungu. Lakini nchi bado inayo nafasi ya kutubu. Tabiri za namna hii zilitoka mara tatu zikiionya Burundi ikapuuza. Mungu awape viongozi wetu hekima.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom