Askofu atabiri Tanzania kupigwa na Rwanda!

Status
Not open for further replies.
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!

Hivi nani huwa anawapa uaskofu? Maana siku hizi kila mtu anajiita Askofu!
 
Samahani ndugu zangu Wakiristo nawauliza kitu kimoja kutokana na alivyoandika huyu jamaa " HIVI MUNGU WENU ANA MAPUNGUFU NA UPUMBAVU? " pia nimesikia Lema alikuwapo ndani ya mahubiri.

hapana.ni mungu wake huyo aliyesema hivyo ndio atakuwa --------.ndugu yangu dini yetu ina shida ya kila mtu kutafsiri mambo anavyopenda.this is a big problem in christianity.i have to admit!
 
Ushauri kwa waumini wa kanisa lake,wajitahidi kutoa sadaka mana hiyo ni njia mpya ya kudai sadaka

Hata wakati wa Nuhu walidhihaki hivi hivi, Mungu anaongea na watu leo kama alivyokuwa anaongea nao zamani.
 
Hivi nani huwa anawapa uaskofu? Maana siku hizi kila mtu anajiita Askofu!

Kwa taarifa yako utabiri huu nimeshawahi kumsikia akiusema mwaka 1996, alifundisha somo linaloitwa Kanuni ya kukijaza kikombe cha uovu cha baba zetu.

Yesu aliwaambia waisraeli waliokuwa wanamdhihaki, 'Kijazeni kikombe cha baba zenu ili baada ya hapo iwajie hukumu iliyo ya haki kwenu. Na baada ya Yesu kuondoka duniani walivamiwa wakapigwa na kuchukuliwa utumwani.

Kuna kikombe ambacho kinajazwa na uovu wa tangu mababu, kikijaa uovu MWAFA!!
 
i think we should not ignore this prophecy but take appropriate actions. if he is lying then the word of God is very clear about this " 20 But the prophet that shall speak a word presumptuously in My Name, which I have
not commanded him to speak, or that shall speak in the name of other gods, that same
prophet shall die.
21 And if you say in your heart, How shall we know the word which YHWH has not
spoken?
22 When a prophet speaks in the Name of YHWH: if the thing follow not, nor come to
pass, that is the thing which YHWH has not spoken. The prophet has spoken it
presumptuously: you shall not be afraid of him.
(Deut. 18:20-22 HRV)"

is time for tanzania to repent
 
Tunaweza tukatukana sana na kukejeli sana. Kama ujumbe haukutoka Mungu nothing will hapen. Lakini kama umetoka kwa Mungu utatimia hata kama ni baada ya miaka mingapi. Sikuusikia unabii lakini Kagakee anaweza akawa anatumika ili kutimiza unabii. Kilio cha wanyonge kikifika kwa Mungu huachilia hasira kama hakuna wa kusimama kwa maombi ili kuizuilia. Bila shaka hizi comments zitairahisisha kazi yq Mungu. Tukumbuke vita haina macho. Mungu akiachilia hasira huchukua muda mrefu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mungu wangu nakuomba usituhesabie dhambi hii. Nakuomba utusamehe wote. Amen.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Dah!! ... tulipofikia kunahuzunisha.
Kazi tunayo na hii yote ni siasa za ugomvi na uonevu za ccm na washirika wake dhidi ya wanyonge, hivyo watu wanamakovu ya uonevu yaliyopelekea uzalendo kupotea kabisa , inakuaje unawanyima watu ajira kisa hawana anayewafahamu kwenye majeshi halafu ukizidiwa wanawarudisha wanao nyuma waliokuwa wamewapa vyeo kwenye majeshi kwa upendeleo ili wamtangulize yule wa mtaani waliyemnyima ajira. Hapo hata mimi siwezi kubali
 
Amin alivamia Tanzania na kuchukua sehemu ya nchi, tulipo mpa majibu yake tulitwaa nchi nzima.
Hatutaingia Rwanda hata kidogo tutaibomoa kwa mbali
 
Ninachoweza kusema kwa kifupi tu ni kuwa Mzee Emmanuel Lazaro (Askofu Mkuu Mstaafu wa TAG) ni kati ya viongozi wa dini wanaheshimika sana kwa huduma yao ya kiroho ndani na nje ya nchi. Ni mtu mzima mwenye umri zaidi ya miaka 70 na sijawahi kusikia kashfa katika utumishi wake kwa miaka zaidi ya 30 ambayo nimemfahamu. Tunaweza tusikubaliane na unabii huu aliotoa (maana tunatofautiana sana kwenye mambo ya imani), lakini hatuna pia sababu ya kumtukana, kumdhalilisha na hata kumwita nabii wa uongo au mchungaji wa mshahara kama ambavyo baadhi yetu wanafanya kwenye thread hii. Asanteni kwa kunisikiliza!
Huyu Bishop, aliwahi kutoa UNABII kuhusu Tanzania na Burundi, alizunguka nchi nzima aliitwa IKULU kuelezea hicho alichokuwa anasema ameambiwa na Mungu, akiwa Mbeya Mh Mkuu wa Mkoa Enzi hizo Paul Kimiti , alimwita (Ilikuwa kabla ya kwenda Ikulu) akamwambia yeye (Bishop Lazaro) ni NABII wa uongo na hajatumwa na Mungu aache kuwatia hofu watanzania, Bishop Lazaro akamwambia Mungu ndie aliyekupa nafasi hiyo, na ana uwezo wa kumtoa!! Mh Kimiti alijibu kwamba elimu yake ndiyo iliyompa ukuu wa Mkoa! Nadhani the rest is history!! Kimiti aliyewahi mpaka kuwa Waziri leo si Mkuu wa Mkoa na umaarufu wake kushney!! Huyu Bishop ana Kanisa pale Moshi, hana kashfa yoyote na ana washirika nadhani zaidi ya 4,000!
 
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!
hana lolote.he is just seeking popularity.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom