Askofu Anthony Mayalla is no more

Askofu Anthony Mayalla is no more

Jina la bwana lihimidiwe....bwana ametwaa Amina.
Pumnzika kwa amani Askofu Mayalla.
 
Ninasikitika kuwataarifu Mhashamu Askofu Athony Mayalla wa jimbo la Mwanza amefariki dunia katika Hospital ya Bugando.....!

Habari zaidi zitafuata.
Bwana ametoa na bwana ametwaa..Jina lake lizidi kutukuzwa.
Namuombea mapumziko mema yenye amani.Amen
 
Lunyungu,

Asante kwa habari hii ya msiba wa mhashamu Askofu wetu mpendwa Anthony Mayala. Kwa sisi waseminari huyu mzee ametufanyia mengi sana. Nilimuona kwa mara ya kwanza wakati akitembelea parokia yetu early 1980s. Huyu mzee nitamkumbuka sana kwa kutoa nafasi kwetu watoto wa wakulima tukapata nafasi ya kusoma. Hakika bila ya juhudi za watu kama hawa sijui kama wengi wetu (hoi poloi) tungepata nafasi za kusoma-ukichukulia kwamba vijijini kwetu hatukuijua serikali zaidi ya wamisionari na watu kama akina Askofu Mayala. Alijitahidi sana kujenga huduma za kijamii. Kwa wote walioguswa na maisha yako watakukumbuka.

Kama binadamu mwingine yeyote alikuwa na mapungufu yake. Lakini naamini ni Mwernyezi Mungu pekee mwenye uwezo wa kumuhukumu kama kazi aliyompa aliifanya kwa ukamilifu na uaminifu.

Baba Askofu upumzike kwa amani. Tulikupenda lakini Muumba wako alikupenda zaidi. Jina la bwana litukuzwe.

Masanja,
 
RIP Askofu Mayala, utakumbukwa kwa hekima na busara zako katika uongozi mzima wa RC.
 
Masanha jambo hili mni zito lakini Mayala alikuja kunipa kipaimara ( Confirmation) na akasema atapenda kuniona niko Seminary , baada ya Ibada aliniombea baraka na kunishika kimwani na kweli nikatinga Seminary .Huyu mzee alikuwa mwelewa alipenda wasomi.Jimbo la Mwanza nina imani lina ongoza sana kwa kuwa na mapadre wasomi maana alifika kote Duniani kuulizia kama anaweza kusomesha mapadre huko.Kazi za injili ujenzi wa zahanati , mashule na misaada hakika the man worked hard .Again apumzike kwa amani .
 
Pole kwa waumini wote wa kanisa katoliki na kwa watz wote kwa kuondokewa na mtu muhimu. Mungu amlaze mahali pema peponi. Vizuri vinaondoka tunabaki na nini?
 
Habari hizi nimezipokea kwa mshtuko mkubwa sana. Nimepata nafasi ya kufanya kazi chini ya Askofu Mkuu Mayalla katika Idara ya Afya na vile vile alinipa heshima ya pekee mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu kuliwakilisha Jimbo hilo kwenye nafasi muhimu wakati ule. Ni kwa ajili yake nikaguswa na siasa za Tanzania kwa namna ya pekee.

Ninatoa pole kwa waumini wa Jimbo la Mwanza, wakazi wote wa Mwanza, masista wa Kawekamo, parokia ambazo nilibahatika kufanya nao kazi Bugando, Kirumba, Nyakato, Nyakahoja, Magu na kwingine kwa msiba huu mzito.

Ninaona nilipata neema ya pekee kuweza kumfahamu Askofu Mayalla.

Mungu aiweke roho yake pema peponi Amina.

Ad Majorem, Dei Gloriam!

ASK
OFU MAYALLA AFARIDI DUNIA
Kutoka mwanakijiji.com

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Mwanza Mhashamu Antony Mayalla amefariki duniani. Hadi tunaingia mitamboni hatujajua bado chanzo cha kifo chake. Askofu Mayalla alizaliwa tarehe 23 Aprili, 1940 huko Mwabagole, Kwimba mkoani Mwanza. Baada ya masomo ya msingi na Sekondari na baadaye Useminari alipewa daraja takatifu la Upadrisho tarehe 20 Disemba mwaka 1970.

Aliteuliwa kuwa Askofu wa Musoma mwaka 1979 (miaka tisa tu baada ya upadrisho) na kuwa miongoni mwa maaskofu vijana wa Kanisa Katoliki akiwa na miaka 39 tu. Alisimikwa kuwa Askofu wa Jimbo la Musoma tarehe 22 Aprili, 1979 na Muadhama Kardinali Laurean Rugambwa akishirikiana na Maaskofu James Rubin M.Mafr. na Askofu Renatus Butibubage aliyekuwa Askofu wa Mwanza wa wakati huo. Kufuatia kujiuzulu kwa Askofu Butibubage mwaka 1987, Baba Mtakatifu Yohanne Paulo wa Pili alimteua Askofu Mayalla wa Musoma kuliongoza Jimbo Kuu la Mwanza kama Askofu wake Mkuu Novemba mwaka huo.

Alisimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mwanza 28 Februari, 1988 na hivyo kuanza utawala wa Utume wake wa kiaskofu.

Baada ya kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Askofu Mayalla alisimamia kwa kiasi kikubwa uhamishaji wa Makao Makuu ya Askofu kutoka Bugando kwenda kilima kingine cha Kawekamo maili chache toka Uwanja wa ndege wa Mwanza.

Askofu Mayalla ameweza kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kichungaji jimboni mwake huku akiongoza kwa kupata waseminari na mapadre wapya, kufungua seminari ya kwanza ya Wasichana Jimboni na vile vile kuendelea kufungua vituo vya afya, shule za sekondari na programu mbalimbali za Afya. Jimbo la Mwanza chini ya Askofu Mayalla limendelea kutoa mojawapo ya mafunzo ambayo kwa muda mrefu yalikuwa yanatolewa Mwanza tu nayo ni yale ya Clinical Pastoral Education ambayo yalikuwa yanahusisha watu wa dini mbalimbali kujifunza jinsi ya kuhudumia wagonjwa.

Wengi watamkumbuka katika maadhimisho ya Misa ya Papa Yohanne Paulo wa 2 kwenye viwanja vya Kawekamo Mwanza na pia katika misa ya kumuaga marehemu Baba wa Taifa huko Butiama ambayo yeye aliiongoza.

Mipango ya mazishi itajulikana baadaye.

Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi, Amina
 
Last edited:
Miongoni mwa legacy alizoacha ukiachia hospitali ya Bugando, ni mmoja waliokuwemo kwenye jopo la tafsiri ya Biblia takatifu kwa lugha ya Kisukuma na ujenzi wa Parokia ya Bujora iliokuwa ikiendesha misa kwa lugha ya Kisukuma.
RIP MHASHAMU ASKOFU ANTHONY MAYALLA.
 
Asante Lunyungu kwa post hii. Masanilo alishatoka na breaking news yake dakika 42 kabla ya post yako. Nashauri umuombe mod aiunganishe ili tuendelee na eulogy moja for this great man
RIP Bishop Mayalla.
 
Back
Top Bottom