Askofu Anthony Mayalla is no more

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Ninasikitika kuwataarifu Mhashamu Askofu Athony Mayalla wa jimbo la Mwanza amefariki dunia katika Hospital ya Bugando.....!

Habari zaidi zitafuata.
 
Asante Masanilo kwa taarifa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi kiongozi wetu wa kiroho Askofu Mkuu Anthony Mayalla.
 
............................MUNGU, ailaze pema peponi roho yake na wanga wa milele umwangazie astarehe kwa amani.
 
Bwana ametoa, bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe..RIP Arch Bishop Antony Mayala.
 
Jimbo la Mwanza ndio lipi hilo, kanisa gani ndugu? Wengine hatumfahamu, hebu tueleze kidogo Mkuu.

Si lazima ujue kila kitu ......tupo kwenye majonzi sisi wewe unaleta za kuleta....Buricheka....shame on you!
 
Marehemu Askofu Mkuu Anthony Mayalla alikuwa kiongozi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Mwanza
 
Ndugu wana JF wakati Kanisa linajiandaa na mapambano dhifi ya Ufisani wakristo wa Jimbo Katoliki Mwanza wame ondokewa na Askofu wao Mhashamu Mayalaa.Mayala atakumbukwa kwa uchapaji wake wa kazi nakuweka Elimu mbele , namkumbuka kuanzia niko kule Seminary wakati akiendesha majimbo 2 kwa wakati mmoja kabla ya Marehemu Samba. Mapadre wa Jimbo la Mwanza watamkumbuka kwa kuwa karibu nao na kusimamia kazi za kichungaji na maendeleo katika Jimbo la Mwanza .

Pole sana ndugu Pendo .Katika mazishi yake na hasa muda huu tutumie pia neno kufa kufaana maana masikio yote yatakuwa Mwanza msimo na mkazo wa Waraka kwa Nchi nzima uongezewe kasi .

Mungu ampe pumziko la milele .
 
Last edited by a moderator:
Marehemu Askofu Mkuu Anthony Mayalla alikuwa kiongozi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Mwanza
Ahsante Mama Mdogo, sikumfahamu marehemu, wala kanisa lake. Waumini wa Kanisa Katoliki na Tanzania kwa ujumla hili ni pigo; Ajuae Bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu, mgonjwa kuwa salama, leo tunawapa pole. Au hongera, maana ameenda kuliko bora zaidi.

Si lazima ujue kila kitu ...... tupo kwenye majonzi sisi wewe unaleta za kuleta.... Buricheka.... shame on you!
Masanilo,

Si lazima nijue kila kitu, kweli, na haiwezekani kabisa. Nani ajua yote zaidi ya Mwenye Enzi Mungu?

Lakini katika swala kama la kutangaza msiba sikuona ubaya wa kuuliza marehemu askofu wa jimbo la Mwanza alikuwa kanisa gani? Habari za kilio nilidhani tunataarifiana na tusiomjua marehemu tujumuike pamoja katika kipindi hiki kigumu. Sijui wanilaania nini.

 
Last edited:
Raha ya milele mpe Ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani. Amen.
 
askofu anthony mayallah! ooh, too bad. ama kweli ilishaseemwa kila nafsi itaonja mauti, alale pema peponi, mtumishi huyo wa bwana. aamen
 
Mungu Mtakatifu katika Jina la Yesu, ambaye alimuumba Mpendwa wetu Askofu Antony Mayala, hatimaye amemrudisha kwake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen.
 
Back
Top Bottom