Askari Wanyamapori kizimbani kwa kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania hasara ya Shilingi 2,231,000

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Askari Wanyamapori Bw. Ibrahim Silas Mtaki, Mfanyabiashara wa mbao Bw. Roden Esches Mwalongo na Mjasiriamali Bi. Lilian John Jombe, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa shtaka la kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania hasara ya kiasi cha Shilingi 2,231,000/=

Akisoma mashtaka hayo katika Kesi na. ECO 14/2023 mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo Mhe. Edward Uphoro, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Bi. Restituta Kessy akisaidiana na Bi. Husna
Kyoba na Bi. Lissa Gwakisa Kasongwa alisema makosa hayo ni Kinyume na Aya ya 10 ya Jedwali la kwanza na Kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Mshtakiwa wa kwanza Bw. Ibrahim Silasi Mtaki na Mshtakiwa wa tatu Bi. Lilian John Jombe walisomewa mashtaka yao ambapo mshtakiwa wa kwanza alikana na Mshtakiwa wa tatu alikiri na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Mshtakiwa wa pili hakufika mahakamani kwa sababu za ugonjwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 13, 2023 ambapo washtakiwa watasomewa hoja za awali.
 
Natumaini watapewa adhabu ya kufagia maeneo ya hospital ya Mwananyamala.
 
Mshtakiwa wa kwanza Bw. Ibrahim Silasi Mtaki na Mshtakiwa wa tatu Bi. Lilian John Jombe walisomewa mashtaka yao ambapo mshtakiwa wa kwanza alikana na Mshtakiwa wa tatu alikiri na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Mshtakiwa wa tatu, imekuaje ukubali kizembe hivyo hasara yenyewe ni 2.2mil tu...

Hao watu huwa hawana huruma na dagaa, wanakuchapa mvua ukatumikie hadi miaka ya kambale wakwepa kodi...
 
Nimekimbia kufungua Uzi nikizani ni 2 point something billions na Sio tumilion mbili twa Tanzania,Nimekasirika kuona waiba kuku ndio wanaozidi ng'ang'aniwa na Sio wezi wa Ng'ombe.
 
Nchi ya Ajabu na maajabu yake.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Si wazichange tu wawalipe?
Ile mijizi ya kwenye ripoti ya CAG ipo tu inadunda
 
Askari Wanyamapori Bw. Ibrahim Silas Mtaki, Mfanyabiashara wa mbao Bw. Roden Esches Mwalongo na Mjasiriamali Bi. Lilian John Jombe, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa shtaka la kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania hasara ya kiasi cha Shilingi 2,231,000/=

Akisoma mashtaka hayo katika Kesi na. ECO 14/2023 mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo Mhe. Edward Uphoro, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Bi. Restituta Kessy akisaidiana na Bi. Husna
Kyoba na Bi. Lissa Gwakisa Kasongwa alisema makosa hayo ni Kinyume na Aya ya 10 ya Jedwali la kwanza na Kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Mshtakiwa wa kwanza Bw. Ibrahim Silasi Mtaki na Mshtakiwa wa tatu Bi. Lilian John Jombe walisomewa mashtaka yao ambapo mshtakiwa wa kwanza alikana na Mshtakiwa wa tatu alikiri na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Mshtakiwa wa pili hakufika mahakamani kwa sababu za ugonjwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 13, 2023 ambapo washtakiwa watasomewa hoja za awali.
Kamateni na hao papa waliotajwa kwenye ripoti ya CAG kwa kuisababishia serikali hasara ya billions badala ya kukamata vidagaa wa milion 2. What is a shame?
 
Nimekimbia kufungua Uzi nikizani ni 2 point something billions na Sio tumilion mbili twa Tanzania,Nimekasirika kuona waiba kuku ndio wanaozidi ng'ang'aniwa na Sio wezi wa Ng'ombe.
Nchi hii vihela vidogo wanakomaalia sana ila mabilion kimyaa

Ova
 
Back
Top Bottom