Askari waliopambana na Hamza wapewa zawadi

Askari polisi 11 waliomdhibiti na kumuuwa gaidi Hamza pale Selender bridge wamepewa vyeti vya kutambua ujasiri na uzalendo wao uliotukuka.

Mungu ni mwema wakati wote!
Kwanini post hii imewekwa "Jukwa la siasa"?
 
Askari polisi 11 waliomdhibiti na kumuuwa gaidi Hamza pale Selender bridge wamepewa vyeti vya kutambua ujasiri na uzalendo wao uliotukuka.

Mungu ni mwema wakati wote!
Jambo la heri. Ndio uzuri wa tukio kuwa mubashara na wazi mbele ya wananchi. Sijui ndio mwanzo na haitakuwa mwisho? Mara nyingi tunaletewa PR za polisi kurushiana risasi na majambazi hatari na kufanikiwa kuwaua wote lakini mashujaa hawatajwi wala vyeti havitolewi.
 
Kamanda muliro mchana huu amewatunukia zawadi za vyeti na pesa kwa mashujaa wetu wa jeshi la polisi waliojitoa mhanga kupambana na Hamnza wakafanikiwa kumuuwa

Katika ukurasa wa instagram wa millard ayo ameripoti tukio hilo lakini chakushangaza badala ya wananchi kupongeza jeshi letu wameonekana kuweka emoji za kucheka na kuwadhihaki mashujaa wetu kuwa hawakustahili kupewa zawadi eti walikuwa hawana shabaha
Nakumbuka nilisema zile risasi walizommiminia zilikuwa na nia ya kujenga hoja kuwa marehemu alikuwa anawakimbia ila walifanikiwa kumpiga risasi na kumuua.
 
Nilichokishuhudia siku ile ya Hamza nikijumlisha na nilichokiona siku soko la Kariakoo linaungua naona kuna umuhimu kujifunza martial arts na mazoezi ya mbio kwaajili ya kujilinda mwenyewe tu
.

Bongo hata ukijamb utasikia sababu ni serikali ya mitozo

wakuu ukiwa maskin tabuu
 
Hakuna zawadi ingewafaa kama kuwapeleka kozi ya mafunzo ya namna bora ya kupambana na wahalifu
Na ilitakiwa hivyo ila kwa sababu kila mtu anataka kula akiwa afisi ya serikali ndiyo haya tunayo shuhudia.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ametoa zawadi ikiwemo fedha na vyeti kwa maaskari polisi walioshiriki katika tukio la kupambana na Hamza aliyezua taharuki karibu na zilipo ofisi za ubalozi wa Ufaransa Dar es Salaam Agosti 25 mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 20, 2021, na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro.

"Askari hawa (Waliopambana na Hamza) miongoni mwao walikuwa ni Askari 11, ambao kwa mamlaka za kisheria za uendeshaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP amewapa zawadi ya vyeti vya ujasiri na zawadi ya pesa kwa kadri alivyoona inafaa," amesema Kamanda Muliro
Yaani Askali kikosi kizima Cha Askali zaidi ya 30,kupambana na Raia mwenye siraha,mkapiga risasi zaidi ya 20!mkamkosa,mnapewa zawadi?!!
Sasa hao raia wangekuwa 10 kama wale wa Westgate! Dar si ingechimbika.
 
Back
Top Bottom