Askari wa usalama barabarani waliopiga picha ya mahaba wakiwa na sare za Polisi wafukuzwa kazi

Sijawahi kuona MTU anafukuzwa bila kufuata utaratibu!! Kama walikuwa wanamakosa mengine ya nyuma hapo saw a kama ndo kosa lao LA kwanza wangeonywa!!
 
Hii tena imetokea huko kenya
76143_01_m_20111227092647.jpg
 
Eh hivi mbona ni vitu vidogo tu hivyo. Wangepewa tu onyo. Chakushangaza askari hao wa barabarani wanakula rushwa kila siku na kila mahali hapo TZ na ni hali ya kuleta hatari kubwa barabarani pale wanapo waachia wavunja sheria kwa kupewa rushwa lakini hao husikii wakifukuzwa kazi




Tunamsubiri Masihi Mwana wa Mungu aje ahukumu ulimwengu kwa haki.

Ninachukia sana dhulma wanayotendewa wanyonge kama kafara kwa wakubwa wa nchi hii.

Hivi kwa nini tuhuma za rushwa kwenye nchi hii sio ishu sana mpaka iwe kwa askari polisi tena wale wadogo tu mana kama ni ufuska hata wakubwa unatajwa ,kama ni rushwa imeanzia juu mpaka chini.

Kukumbatiana watu wakiwa makazini sio jambo zuri lakini kukumbatia wahalifu ni jambo baya zaidi.

Inabidi sasa wale maocCID na maarco wanaokumbatia majambazi na wahalifu nao pia washughulikiwe.Maana hawa ndio mapapa wanaovunja maadili ya polisi lakini wanadunda tu ndani ya polisi.
 
Kamanda a Polisi Mkoani Kagera Henery Mwaibambe ameeleza waandishi wa habari muda mfupi uliopita kuwa, askari hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi.

Kwamba walikuwa wanafanya kazi katika Wilaya ya Misenyi.
==================



Chanzo:Harakatinews

Haja violate constitution
 
Kupigana mabusu ni kulidhalilisha jeshi?watu wanapeana mabusu bila shuruti
 
[FUKUZA WASHENZI WOTE HASA WALE WANAOTUDAI RUSHWA MI WANANIKERA SANA HATA KOSA LA KUKUELEKEZA UKAREKEBISHE WANATAKA PESA ILI WAKAHONGANE VIZURI
demu.jpg
[/QUOTE]
 
Nilikuwa najiuliza hawa walikuwa askari wa wapi.....kumbe misenyi.....sasa kama hakuna magari ya kupiga mabao mlitegemea wangefanya nini.....devils work with idle hands...
 
Huyo afande men anaitwa "MPOKI "
Na mke wake ni mwalimu huyo demu alikuwa anaoshea tu rungu
 
majanga mengne ya kujitakia. sasa kulikuwa na haja gani ya kupiga hizo picha! ok kama lengo ilikuwa ni kuweka kumbukumbu iweje waziweke kwenye mtandao? me nadhani walichoka hii kazi ya upolisi
Huyu mmoja alianza kwa kumrushia mwenzake kwenye whastup,aliyerushiwa kamrushia mwingine,mara ikaenda kwa wa depo ,within few minutes hiyo picha ilikuwa inazunguka whatsup na baadae kidogo ikarushwa jamii forums,nadhani huu wote ni ulimbukeni wa mitandao na madhara ya teknolojia cheap ya mchina.
 
Ebwaba mwaka huu mwezi wa pili kwenye mzani wa Dodoma kama unaanza kuuacha mji nikiwa kwenye gari nikamwona Jamaa yangu tuliachana kitambo sana tangu tumemaliza shule huko mkoa, nikashuka nikamkumbatia akiwa kwenye uniform dah mi sikujua ka hairuhusiwi alitaka kulia

yaani we acha tu PGO noma
 
[FUKUZA WASHENZI WOTE HASA WALE WANAOTUDAI RUSHWA MI WANANIKERA SANA HATA KOSA LA KUKUELEKEZA UKAREKEBISHE WANATAKA PESA ILI WAKAHONGANE VIZURI
demu.jpg
[/QUOTE]

na mimi mnanikera hasa mnapotoa rushwa

wasingeomba kama amtoi
 
Back
Top Bottom