Askari wa usalama barabarani waliopiga picha ya mahaba wakiwa na sare za Polisi wafukuzwa kazi

HarakatiNews

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
218
185
Kamanda a Polisi Mkoani Kagera Henery Mwaibambe ameeleza waandishi wa habari muda mfupi uliopita kuwa, askari hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi.


Kamanda Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788, PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme, wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Misenyi, mkoani Kagera.
==================

IMG-20141008-WA0023.jpg

JESHI la Polisi mkoani Kagera limewafukuza kazi askari wake watatu kwa kulifedhehesha jeshi hilo kutokana na kitendo cha kupiga picha inayowaonyesha wawili kati yao wakinyonyana ndimi wakiwa kazini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, alisema kitendo kilichofanywa na askari hao kimeshusha hadhi ya jeshi.

Aliwataja askari hao waliofukuzwa ni F.7788 PC Mpaji Mwasumbi, G 2122 PC Fadhili Linga na WP.8898 Veronica Mdeme ambao wote ni wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Misenyi.

Alisema PC Mpaji na WP Veronica walipiga picha inayokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi wakiwa kazini, huku PC Fadhili akiingia matatani kwa kuwapiga picha hiyo chafu askari wenzake na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda Mwaibambe alisema picha hiyo ilianza kuonekana katika mitandao mbalimbali ya kijamii mapema wiki hii.

Alisema askari PC Fadhili alipiga picha hiyo mwaka 2012 kwa kutumia simu yake ya kiganjani na kuitunza, lakini wiki hii aliamua kuisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume na kazi yake.

"Napenda kuthibitisha kuwa picha hii iliyoonekana kwenye mitandao ya kijamii ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa kabisa.

"Maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari wetu wanafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi na si vinginevyo.

"Jeshi halikubaliani na vitendo hivi, ikitokea askari kwenda kinyume lazima achukuliwe hatua kali," alisema Kamanda Mwaibambe.

Taarifa zaidi kutoka mkoani Kagera, zinaeleza baada ya kusambazwa kwa picha hiyo na kuonekana katika mitandao ya kijamii, WP Veronica alianguka ghafla na kupoteza fahamu kwa mshtuko wa tukio hilo.

Kutokana na hali hiyo, majirani waliokuwa karibu na nyumbani kwake walilazimika kumpatia msaada na kumkimbiza hospitali kwa matibabu, ambako aliruhusiwa juzi jioni kabla ya kutiwa mbaroni.

DAR ES SALAAM

Wakati hayo yakiendelea, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewahamisha askari wake, WP 5863 Quine na WP 3548 Koplo Maeda kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ilala kwa kukiuka maadili ya kazi.

Taarifa ya ndani ya Oktoba 2, mwaka huu ya Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Dar es Salaam iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, imesema askari hao walisimamisha gari dogo na baada ya dereva kujitetea, waliendelea kutafuta makosa hali iliyosababisha abiria aliyekuwa mgonjwa kufariki.

Kutokana na tukio hilo, makamanda wa polisi wa wilaya zote za Mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam wametakiwa kuwakumbusha askari wao kuepuka kutolazimisha kutafuta makosa ambayo hayana madhara.

"Makosa ambayo hayana madhara katika kusababisha ajali mfano ni vifaa vya kuzimia moto, rangi, kadi kutoandika anuani, motor vehicle, leseni chini ya siku 30 na kadhalika," lilisomeka agizo hilo kwa makamanda hao wa polisi.


CHANZO: Mtanzania

Ilivyokuwa:
Jeshi la Polisi: Hili tukio lina ukweli ndani yake au ni kuchafuana tuu?
 
majeshi si lelemama kukumbatiwa tu na ndugu yako labda hamkuonana muda mrefu ukiwa ndani ya magwanda ni hatari tosha sembuse mahaba!!!!
 
Naona sasa hivi wananchi tunatakiwa kuwa makini kubaini kama wanahamishwa kikazi katika mikoa mingine au la!

Naomba kuwasilisha.
 
Mi naona kama wameonewa...
Mbona wenye vyeo wana vituko zaidi ya hawa dagaa na hata warning hawapewi...

Walitakiwa wapewe onyo...lakini kuwafukuza kazi...
Kuna picha ngapi za waheshimiwa tena za aibu zaidi na hamna wanachofanywa zaidi ya stori kuwa ni za kutengenezwa...

That's not fair...
 
Ngoja tukafaidi vizuri kuda dadeki... chezea "conjugal right" wewe.
N a nakala yao ya kufukuzwa hii hapa

MeinKempf ... Sijui labda umekosea...lakini hiyo unayoita hati ya kufukuzwa kazi 'haisemi' lolote kuhusu kufukuzwa kazi bali kufanyiwa 'rotation' kwenye vitengo vingine vya jeshi la Polisi. Pili kosa liliandikwa kwenye hiyo hati ni kukamata gari lisilo na kosa mpaka kupelekea abiria kuchelewa matibabhu na kufariki...acha uongo kwa kuweka document zisizohusika na tukio!
 
Last edited by a moderator:
Na cha ajabu mwanake anaonekana ni Mke wa mtu,angalia pete ya Ndoa! Siuji hili dume ila kwa muonekano umri huo lazima ni mtu na familia yake.
 
Eh hivi mbona ni vitu vidogo tu hivyo. Wangepewa tu onyo. Chakushangaza askari hao wa barabarani wanakula rushwa kila siku na kila mahali hapo TZ na ni hali ya kuleta hatari kubwa barabarani pale wanapo waachia wavunja sheria kwa kupewa rushwa lakini hao husikii wakifukuzwa kazi
 
Nikiichunguza hiyo pete ya mdada ni ya ndoa kabisa!
Sasa kazi hana...na huenda kwa bwanake kibarua cha kumhudumia nako kikaota nyasi!
Hii ni stori ya FROM HERO TO ZERO!:A S wink:
Kweli kabisa na inawezekana huyu hapo anayembusu ndo mumewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom