N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 6,826
- 9,533
Ukweli utafiti nilioufanya kwenye mazingira kadha wa kadha yanayohitaji usafi nimebaini wananchi wengi hapa Tanzania ni wachafu. Hii hasty generalization ni bila kujali ni wasomi au wananchi wa kawaida.
Mfano nimepita kwenye vyoo vya umma, vile vya kulipia, vyoo katika taasisi za elimu ya juu vikiwemo vyuo vikuu vikongwe hapa nchini kwa kweli mazingira ya vyoo ni machafu sana. Utakutana na mikojo au kinyesi pembeni ya tundu au mtu katumia maliwato hajapaswafi. Aidha, nimeenda uwanja wa Taifa Mara kadhaa vyoo ni vichafu mno.
Hata makazini, wakati fulani niliajiriwa Serikalini kwenye ofisi moja yenye reputation kubwa kabisa lakini ile floor ya idara niliyokuwemo haikuwa ajabu kufika toilet kukuta mtu kany'a au kak'ojoa kaacha haja zake hapo, au katumia toilet papers kazichambua kaziacha hapo au kazilowanisha na maji.
Eneo jingine linalothibitisha kwamba wanajamii wetu ni wachafu, ni unaposafiri kwenda mikoani. Barabarani utakutana na taka za chupa tupu, au masalia ya vifungashio vya vyakula vya haraka almaaruf 'take away'.
Eneo jingine linalothibitisha kwamba sisi ni WACHAFU ni namna tunavyoachia 'gereji bubu' kufanya shughuli zao bila mpangilio, kiasi kwamba wanalundika taka mitaani. Mfano ni hapa Dar es salaam kule Tandale, Mwenge jirani na Mwenge Dispensary, Tandika nk pia, Soweto Mbeya miongoni mwa maeneo mengine.
Eneo ambalo wananchi wanajitahidi kwa usafi ni miili yao. Kusema kweli wananchi wengi ni wasafi kwenye miili yao. Ni watu nadhifu na walimbwende haswa. Ukikutana nao kwenye usafiri wa umma ni nadra kukutana na mtu ananuka kikwapa, au kavalia shabishabi. Sasa najiuliza kwanini kwenye mazingira tunakuwa wachafu hivi!? Tatizo liko wapi?
Ukienda nchi kama Rwanda ndio utagundua kwamba sisi ni wachafu sana.
MY TAKE:
Wabunge pitisheni sheria kali ya ulinzi wa mazingira na usafi. Iwe kosa kubwa mtu kuwa na mazingira machafu. Hapa zisiachiwe local governments. Usafi wa mazingira utasaidia sana kupunguza bajeti za afya. Japo mimi sio mtabibu lakini Nina hakika maradhi mengi yanayopeleka watu wetu Hospitali yanahusiana na uchafu. TUBADILIKE.