Asante sana Chadema kwa maamuzi yenu ya leo, nafarijika kuwa bado kipo chama makini chenye msingi imara, hakiyumbi wala hakiyumbishwi!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Mimi pia si Chadema ila namshukuru Jenerali Ulimwengu kwa kusema niliyotaka kuyasema, ni wakati muafaka sasa madaraka yawe mikononi mwa wananchi wenyewe pale pale walipo Kitaifa, Kimkoa, Kiwilaya, Kitarafa na Kimtaa!

Jukumu hilo linaweza kusimamiwa tu na chama imara ambacho kaulimbiu yake ni people's power kilicho tayari kutanguliza maslahi ya nchi na si maslahi ya chama kama CCM...sisi wananchi na si sisi wanachama. Pateni hii burudani kwanza!

Hakika chama cha Chadema kimedhihirisha wazi, pasipo shaka yoyote kuwa wao ndiyo chama pekee hapa nchini chenye demokrasia thabiti.

Hongera Sana chama cha Chadema 👏👏
 
Mimi pia si Chadema ila namshukuru Jenerali Ulimwengu kwa kusema niliyotaka kuyasema, ni wakati muafaka sasa madaraka yawe mikononi mwa wananchi wenyewe pale pale walipo Kitaifa, Kimkoa, Kiwilaya, Kitarafa na Kimtaa!

Jukumu hilo linaweza kusimamiwa tu na chama imara ambacho kaulimbiu yake ni people's power kilicho tayari kutanguliza maslahi ya nchi na si maslahi ya chama kama CCM...sisi wananchi na si sisi wanachama. Pateni hii burudani kwanza!

Kamanda karibu sana ulipotea MAPAMBANO YANAENDEREA
 
Hongera CHADEMA kwa kuonesha busara na ukomavu wa kisiasa katika siasa za Tanzania zilizojaa mikiki mikiki na ghiliba za kila aina....

Pamoja hayo iangaliwe na katiba ili iweke ukomo wa nafasi ya mwenyekiti.....ili kuleta damu changa na kuchochea ari na kasi mpya ndani ya chama....... demokrasia inaanza na wewe kabla hujaidai kwa wengine......
 
Halima na wenzake waende makamani kuweka pingamizi la huu uamuzi wa chama chao.

Sio kwenda mahakamani tu, hata ikibidi wakaishi humo humo mahakamani, ila kwa cdm imefikia mwisho. Huko bungeni wanaweza kuendelea kuwepo maana pia hawakuwa kisheria bali ni kwa maagizo ya Magufuli na Ndugai, na hao wote kwa sasa wamebaki historia.
 
Hongera CHADEMA kwa kuonesha busara na ukomavu wa kisiasa katika siasa za Tanzania zilizojaa mikiki mikiki na ghiliba za kila aina....

Pamoja hayo iangaliwe na katiba ili iweke ukomo wa nafasi ya mwenyekiti.....ili kuleta damu changa na kuchochea ari na kasi mpya ndani ya chama....... demokrasia inaanza na wewe kabla hujaidai kwa wengine......
...Dah!... Demokrasia sio rahisi aisee.
 
Yaani hadi wabunge wa ovyo wa ccm walikuwa wanawashangaa Covid-19. Kongole CDM kwa kuweka sawa rekodi za maamuzi.
Haiwezekani wanachama wafanye umafia mkubwa kama wa Mdee na wenzake wakishirikia na marehemu na Ndugai, then wachukuliwe poa tu!
Uhakika ni kuwa kwa makosa waliyoyafanya hata waende mahakama za ndani na za kimataifa bado watashindwa kesi.

I stand to be corrected!
Tunapotaka mabadiliko lazima tuwe tayari kubadilika!
HONGERENI CHADEMA!!
 
Mzee Halima alikitia Chama unajisi Mkubwa Sana. Kiongozi muandamizi unafikia hatua ya kughushi nyaraka za Chama Ni aibu kubwa.
 
Siasa ni uhuni na kuwahiana, full umakaveli. Wakina Mdee wamecheza vizuri ndiyo wako hapo. Mbowe anacheza vizuri, hadi leo mwenyekiti. CCM wanacheza vizuri, hadi leo wapo madarakani. Ni game tu, usiweke matumaini yako huko.
 
Karibu tena jukwaani mkuu
Asante sana ndugu yangu, JF kwa muda sasa imekuwa kama kokoro inazoa tu...hadi chawa! Ndio maana siku hizi nafanya jitihada kubwa kukaa mbali na JF ila tatizo ni hao chawa, inanibidi kuingia hata kama ni kuwapulizia dawa.

Toka mwaka 2008 najiunga na Jamii Forums nilisema na kusisitiza kuwa adui nambari wani wa taifa letu, Tanzania, ni CCM. Huu msimamo nimekuwa nao hadi leo haujabadilika na kila nikipata nafasi ya kuchangia nakazia hapo hapo.

Nikisema sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa wachache sana wataamini kwani kulingana na mawazo ya chawa, mkosoaji mkuu kama mimi lazima ni Chadema...Chadema hata makao yao sijui yalipo, nasikia tu yako UFIPA.
 
Mimi pia si Chadema ila namshukuru Jenerali Ulimwengu kwa kusema niliyotaka kuyasema, ni wakati muafaka sasa madaraka yawe mikononi mwa wananchi wenyewe pale pale walipo Kitaifa, Kimkoa, Kiwilaya, Kitarafa na Kimtaa!

Jukumu hilo linaweza kusimamiwa tu na chama imara ambacho kaulimbiu yake ni people's power kilicho tayari kutanguliza maslahi ya nchi na si maslahi ya chama kama CCM...sisi wananchi na si sisi wanachama. Pateni hii burudani kwanza!

Nimekubali mzee ulimwengu ni MOJA wa deep state, na niwachache sana
 
Back
Top Bottom