Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,988
- 22,379
Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena .
Sawa ila kwa sasa wacheni ujuaji.Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Katiba mpya ndio suluhisho la Matatizo mengi ya nchi yetu. Sio matatizo yote, narudia kusema matatizo mengi. Maana katiba ni muongozo tu kama ilivyo Qur an au bible.Katiba mpya ndio kaburi la chama chakavu
Eti kuingilia dirishani...!!! Dar..!! this is JF banaa...Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Usipofuata biblia, utaishia tu kutengwa na kanisa... USIPOFUATA KATIBA.. GEREZA LINAWEZA LIKAKUHUSUKatiba mpya ndio suluhisho la Matatizo mengi ya nchi yetu. Sio matatizo yote, narudia kusema matatizo mengi. Maana katiba ni muongozo tu kama ilivyo Qur an au bible.
Leo Qur an ipo na waislam hawaofuati, bible ipo na wakristo hawaifuati ni kipi kinachokuonyesha watanzania watakuja kuifuata katiba mpya???
Kwahiyo katiba mpya tunaitaka maana itatusaidia kupunguza matatizo mengi yanayotusibu Watanzania.
Kwani rasimu si ipo?Katiba mpya au iliyoboreshwa ni nzuri Sana
Lakini je hao waandishi wa katiba mpya ni wakina Nani?
Tusije kukuta tunaleta vitu vya ajabu
Halafu sasa ana kimbelembele. Yaani maoni mabovu kabisa ndio maoni ya kwanza!Kwa maoni haya ni wazi kuwa umevurugwa kama wale wasiotaka kuamini awamu ya tano imekwisha na sasa tuko awamu ya sita.
Pole eeh.
Zote zipoIpi?
Zilikua version 2
Katiba mpya ndio suluhisho la Matatizo mengi ya nchi yetu. Sio matatizo yote, narudia kusema matatizo mengi. Maana katiba ni muongozo tu kama ilivyo Qur an au bible.
Leo Qur an ipo na waislam hawaofuati, bible ipo na wakristo hawaifuati ni kipi kinachokuonyesha watanzania watakuja kuifuata katiba mpya???
Kwahiyo katiba mpya tunaitaka maana itatusaidia kupunguza matatizo mengi yanayotusibu Watanzania.
Mkuu umeongea kwa hasira mno hata kama ndo ukweli!Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Katiba mpya inaweza kuandikwa lakini ikawa mbovuuuu kuliko hata iliyopo sasa hivi.Kwa heshima naomba nkuvulie kofia niliyovaa wakati huu naandika huu uzi.
Wakati historia inaandikwa juu ya upatikanaji wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Maxence Melo tutamtambua kama prominent figure wa kwanza kabisa kutoka hadharani na kumuomba Mheshimiwa Rais Mama yetu kipenzi Samia Suluhu Hassan kutupatia katiba mpya. Mkurugenzi huyu mtendaji wa Jamii Forums alilitoa ombi hili maalumu kwa Mheshimiwa raisi alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 hivi karibuni juu ya masuala mbali mbali.
View attachment 1809190
Najua wapo wengi ambao wanatamani kupatikana kwa katiba mpya na wamekuwa wakilipigia kelele suala hili kwa muda mrefu sana, kwa mfano viongozi mbali mbali wa vyama vya upinzani na wanaharakati wa haki za kibinaadamu kadhaa. Lakini Maxence Melo yeye sio kiongozi wa chama cha upinzani wala sio mwanaharakati wa haki za binaadam, yeye ni mdau mkubwa wa sekta ya TEHAMA na hili ndilo lililonifanya kuandika uzi huu wa kumbukumbu maana kwa wadau wengi wa habari katika zama hizi wamekumbwa na uoga wa hali ya juu kiasi kwamba wanashindwa kutoka front na kutoa/ kuongelea mambo ya msingi kama haya.
Mheshimiwa Rais wa Awamu ya sita Mama yetu Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mtu msikivu, mwelewa, mkarimu, Muogopa Mungu haswa, mkweli, mpole, mwenye huruma, mwenye upendo wa kweli na sio wa maigizo, mnyenyekevu na mzalendo. Hili linanifanya mimi binafsi kuamini kwamba Mama hatotoka madarakani In Shaa Allah mpaka ahakikishe ametuachia katiba mpya.
Mtu yoyote mwenye mapenzi ya dhati na ya kweli kwa nchi hii ataelewa kwamba katiba tuliyonayo sasa ina dosari kubwa sana na za msingi ambazo hata jitihada gani zichukuliwe basi ni vigumu sana kupiga hatua. Hivyo basi, jambo la kwanza kabisa kulifanya ili nchi yetu hii ipige hatua za dhati za maendeleo ni kuhakikisha kwamba tunapata katiba mpya itakayokidhi mahitaji ya sasa.
Kwako mheshimiwa rais, mimi binafsi naomba kutilia nguvu hoja ya Maxence Melo kwamba huu ndio wakati sahihi wa kuliendea jambo hili. Usisubiri muda uende zaidi Mama. Hii ndio legacy yako Mama na hakika nchi hii itakukumbuka for hundred and thousand years to come. Wasiolitakia mema taifa letu wasikutishe wala kukurudisha nyuma katika adhma hii. Tunatambua ulituambia tusubiri kidogo, lakini mama hakuna ajuae kesho yake.
Waswahili walisema ngoja ngoja huumiza matumbo, na chelewa chelewa ukute mwana si wako. Muda ni sasa Mama yetu kipenzi. Nenda ukaandike historia, nenda ukawakomboe kiukweli wanyonge wa nchii hii.
Kwa wananchi: Tunaendelea kusisitiza kwamba, Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
Viva Mama Samia! Muda ni sasa!
Unafikiri uchaguzi ni kama kununua nyanya sokoni!?Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Halafu sasa ana kimbelembele. Yaani maoni mabovu kabisa ndio maoni ya kwanza!