Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Kabla nawe hujageuka mchawi, tazama video niliyokuwekea halafu usiwe mgumu wa kuelewa.
Aliyeruhusiwa kuota tena ni binti wa Kitanzania, popote pale alipo. Nazungumzia binti yeyote ambaye sasa ameruhusiwa kurudi shule (Kuota tena) kupambania ndoto yake baada ya kukukosea na kupata ujauzito. MFANO MZURI NI HUYO ANAYEONGEA HAPO KWENYE VIDEO.
Wachawi ni wale watu wote ambao wanajipa kazi ya Mungu kuhukumu, na kusema kwamba hawa mabinti hawana haki ya kurudi shuleni kupambania ndoto zao.
Rais Samia anawaruhusu hawa mabinti kuota tena kwani hizo mimba walizopata halijawahi kuwa tamanio lao, wengine wamezipata kwa kubwaka au kurubuniwa, ama ufinyu tu wa kuwaza mbali jambo ambalo sidhani kama linawafanya wakose haki ya kujiuliza tena na kupambania ndoto zao.
Ni uchawi wa hali ya juu kutaka binti kama huyo wa kwenye video hapo chini aendelee kujiona maisha yake yamefika mwisho, anyimwe kabisa nafasi ya kupambani tena ndoto zake. Ni uchawi kwa sababu hao wanaofanya hivyo pia wana madhaifu yao, wamewahi kukosea lakini wanapata nafasi ya kurekebisha.
ARUDI SHULE, Asante kwa Rais Samia kwa kuruhusu binti huyu aote tena.
KWAKO BINTI UTAYERUDI SHULE : Waoneshe uwezo wako, usikubali kurubuniwa tena, usikubali kukata tamaa.