MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Katika dunia hii kila kitu kina mwanzo na mwisho.
Mwanzo wa suala lolote hujenga msingi ambao unakuwa ni rejeo kwa kizazi na kizazi bila kujali kama ni mzuri au mbaya.
Historia yetu inabainisha wakoloni walikuwa na dhana ya kuwa Watanzania hatuna uwezo wa kujiongoza/kujitawala. Hii dhana ilitumika vizuri kwa muda mrefu ili kuhakikisha hatupati uhuru wetu na kujitawala.
Kwa nchini mwetu, uongozi wa Rais Nyerere ulifuta dhana hiyo na kuweka msingi na rejeo ambalo mpaka sasa linatumika katika kupima uongozi na uzalendo wa Rais nchini.
Kutokana na mfumo dume kutamalaki nchini, dhana ya wanawake kushika uongozi wa juu imekuwa ikipingwa sana na waumini wa mfumo dume nchini lakini dhana hii ilipata mtihani baada ya Rais Samia kushika nafasi ya juu ya uongozi wa kurithi nchini.
Urais wa Rais Samia ulikuwa na fursa ya kuifuta hii dhana ya mfumo dume lakini kutokana na hulka za uongozi za Rais Samia ambazo zimeonyesha wazi kuwa hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi unafanya wanaopigia chapuo dhana ya mfumo dume nchini wanaonekana wako sahihi na kwa msingi huo ameua ndoto za wasichana na wanawake wengine nchini wanaofikiria kushika uongozi wa juu kabisa serikalini kwa sababu hawataaminiwa tena nchini.
Kwa sasa itachukua miongo mingi kwa wanawake nchini kuja kuaminiwa na umma kushika tena nafasi ya Urais nchini kwa sababu ya rejea ya uongozi mbovu wa Rais Samia.
Nimesikia baadhi ya wanawake wameanza kuwalaumu wanaume kuwa ndio chanzo cha kushindwa kwa uongozi wa Rais Samia. Mmojawapo aliyetia lawama hizo kwa wanaume ni Mama Gertrude Mongella.
Angalia video;
Kuna baadhi pia wanasema eti anashauliwa vibaya au eti kuna “genge” la washauri linataka asifanikiwe. Ukijiuliza, kwani hilo “genge” au kundi aliyeliweka katika nafasi za kumshauri ni nani? Kwa mantiki hii tukubali kuwa Rais Samia hajui anachokifanya au ni kama “remote control” na kuna mtu/watu wengine wanaitumia!
Yaani Rais Samia anavurunda halafu lawama wanabebeshwa wanaume.
Kuendelea kuwabebesha lawama wanaume au viongozi wengine haimsafishi Rais Samia bali inazidi kuonyesha kuwa hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi. Hii pia inaonyesha ni Rais kivuli!
Katiba yetu katika Ibara ya 33 na Ibara ya 36 imempa Rais madaraka makubwa na uwezo wa kuajiri na kufukuza mtumishi yeyote wa serikali bila kuhojiwa au kuwajibika kwa mtu/taasisi yoyote nchini. Hii ina maana kuwa lolote linalofanyika serikalini linakuwa na baraka/limekubaliwa na Rais kama hajakanusha.
Kwa miongo mingi ijayo wanawake nchini watakuwa wanapimwa kwa kutumia kigezo cha uongozi mbovu wa Rais Samia.
Wanawake ni vema kwa sasa watambue “mchawi” wao katika kuaminiwa na jamii kubwa kuanzia sasa ni Rais Samia na sio wapenda mfumo dume kwa sababu toka Rais Samia apate Urais amejitahidi kuufungamanisha Urais wake na jinsia ya kike huku akijiita Mama na kutaka watanzania wamuone kama Mama.