Rais Samia amewezesha wasichana zaidi ya 6,000 kurejea shuleni

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya sekondari kwa njia mbadala (SEQUIP) umefanikiwa kusajili wasichana 3,616 kwa mwaka 2023 na 3,333 kwa mwaka 2022 wenye umri kati ya miaka 13 hadi 21.

Wasichana hawa wanatarajia kurudi shule kuendelea na elimu ya sekondari baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wanafunzi waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kurudi shuleni ikiwemo wale waliopata ujauzito shuleni.

Maamuzi hayo ya Rais Samia Suluhu yametoa fursa kwa mabinti hawa kutimiza ndoto zao za kielimu lakini kupunguza utofauti kati ya wanawake na wanaume kwenye taaluma au fani mbalimbali.

Sio tu ni faraja kwa wanafunzi waliopata nafasi ya kurudi shule lakini wazazi wa mabinti hawa wamepata matumaini mapya juu ya binti zao.

Ndani ya miaka miwili ya Rais Samia Suluhu madarakani tunashuhudia mabadiliko kwenye sera, sheria lakini sekta mbalimbali kwa maendeleo ya watanzania na ujenzi wa Taifa bora.

FqWuaZIWwAMoAnp
 
Back
Top Bottom