KWELI Asali ni hatari kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Asali ni chakula kinachotumika kama dawa ya magonjwa mengi. Hutibu vidonda, kikohozi, huondoa sumu mwilini, ni chanzo bora cha nishati pia hutumika kwa kazi nyingi za urembo.

8308ECCE-50FE-453E-B8DC-7310CC3FB5ED.jpeg

Ukipita mtandaoni utaona baadhi ya makala zikiweka marufuku ya kuwapatia watoto wachanga asali. Jambo hili linaleta ukakasi mkubwa wa jamii kwa kuwa asai imekuwepo kwa miaka mingi, na karibia kila jamii huitumia.

Katazo hili lina ukweli gani kisayansi?
 
Tunachokijua
Asali ni chakula chenye manufaa makubwa sana kwa afya ya binadamu. Viambato vikubwa viwili vya asali ni maji na sukari.

Kwa mujibu wa USDA, pamoja na uwepo wa virutubisho vingine, asali huwa na nishati ya kutosha, protini, wanga, madini ya chuma, calcium, magnesium, phosphorus, zinc, copper, fluoride na selenium.

Asali hufaa kwa watoto?
JamiiForums imebaini ni ukweli kuwa asali haifai kutolewa kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kwa kuwa mfumo wao wa kinga, pamoja na ule wa chakula huwa bado haujakomaa vizuri.

Chakula hiki huwa na asilimia kubwa ya kubeba bakteria wabaya jamii ya Clostridium botulinum ambao kwa umri huo, mtoto huwa hawezi kuwaharibu akiwala.

Husababisha tatizo hatari lisilo onekana mara kwa mara linaloitwa Infant botulism ambalo huwa na dalili za choo kigumu, kuweweseka, kifafa, changamoto za kupumua zinazosababishwa na kupooza kwa mfumo wa hewa na hatimaye kifo ikiwa msaada wa haraka hautatolewa.

Kwa kuwa tatizo hili halionekani mara kwa mara, pia kwa kuwa ni ngumu kujua asali iliyo salama na isiyo salama kwa kutazama, Kituo Cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa Cha Marekani (CDC) hushauri watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja wasipewe asali kama sehemu ya kuwakinga.

Aidha, mazingira ya uvunwaji wake, uhifadhi na usafirishaji hayawezi kueleweka kirahisi kwa mtumiaji.

Ushauri
Watoto wenye umri zaidi ya mwaka mmoja, watu wazima, wanawake wajawazito pamoja na wazee wanaweza kutumia asali kwani miili yao huwa imekomaa vya kutosha kupambana na bakteria hawa.
Someone's zuri Sana kwa kweli.Wengi tulikuwa hatulijui hili kwa hiyo umetusaidia Sana mkuu tutachukua tahadhari mapema.
 
Asali ni chakula kinachotumika kama dawa ya magonjwa mengi. Hutibu vidonda, kikohozi, huondoa sumu mwilini, ni chanzo bora cha nishati pia hutumika kwa kazi nyingi za urembo.

View attachment 2422162

Ukipita mtandaoni utaona baadhi ya makala zikiweka marufuku ya kuwapatia watoto wachanga asali. Jambo hili linaleta ukakasi mkubwa wa jamii kwa kuwa asai imekuwepo kwa miaka mingi, na karibia kila jamii huitumia.

Katazo hili lina ukweli gani kisayansi?
Asante Kwa somo zuri, ndio nimejuwa Leo🙏🙏🙏
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom