Arusha: Wananchi walia na kituo cha mabasi makubwa ya abiria ya kwenda mikoani

Arusha ipo over rated sana.

Lakini pia serikali imefeli kabisa kuujenga huu mji.

Ilipaswa kabisa uweze kutoa ushindani na jiji la Nairobi.

Lakini umebakia kuwa jiji la hovyo,hata ukipita pale East Africa Hq, AICC ile barabara inatia aibu.

Ndio maana leo google,microsoft na int offices nyingi zinawekwa nairobi.
Arusha hata miaka 50 ijayo haiwezi fikia Nairobi, wala huwezi shindanisha Dar na Nairobi.
 
Arusha ndio mnataka kuifananisha na Mwanza kweli?

Arusha inapambana na miji kama Musoma, Geita, Katoro, nk. Kahama sasa sio level za Arusha tena.

Soon senta kama Kagongwa ama Runzewe zinaipita Arusha.
Kahama stand kubwa imebanana Sana, japo wanasema zipo stand ndogo tatu za mikoa jirani.

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Kuna miji inastahili kuwa na stand zaidi ya moja ila Halmashauri hawajaliona hilo, ile ya Arusha ((kama ndio ile ile nayoijua mie ukitokea Sheikh Amri Abeid kwenda Jogoo House maana nilitoka Arusha kitambo) inatakiwa ibaki pale pale na ikajengwa nyingine na ile ikawa ni ya kupita tu hasa magari yanapoingia usiku yaani yanashusha stand hizo za mbali alafu yanamalizia hapo yanaenda ku-park na kujaza mafuta vivyo hivyo asubuhi wakati yanaenda stand kuu yanapita pale yanakula vichwa alafu linaenda stand kuu ila hasara yake abiria wa pale ni kama hisani maana kama gari linaondoka saa 12 alfajiri basi pale linapita mapema zaidi maana safari inahesabiwa kuanzia stand kuu.

Mwanza waliliona hili kitambo sana zaidi ya miaka 15 kwa kuwa na stand ya Nyegezi na Buzuruga yaani hapo gari zinazotokea Nairobi au Musoma zinaishia Buzuruga ila kama zipo zinazounganisha Dar zinashusha hapo na kula vichwa kisha zinakwenda Nyegezi na zinaendelea na safari na gari zikiingia usiku hata jioni zinashusha Nyegezi alafu zinawasogeza abiria Natta (mjini kati) na zingine mpaka Buzuruga. Na katika utaratibu huu wa kujenga stand mpya na zote zinajengwa ila hii ya Buzuruga wametafuta eneo lingine na imeshakamilika bado kuizindua ambapo hii ya zamani inaweza ikatafutiwa matumizi mengine hata kuwa ya daladala au magari ya kwenda vijijini / wilayani.

Mikoa ya Dar, Mwanza, Arusha na Dodoma zinahitaji stand kuu zaidi ya moja, wenzao Mwanza walishaonyesha mfano tangu kitambo na sasa wanakamilisha stand kubwa 2
Sijui kama wale Wameru na Waarusha kindaki ndaki watakuelewa. Nilijaribu kuwaeleza nikaambulia matusi...

Mkuu una akili kubwa sana!👏👏
 
Hapoa Arusha wanaweza wakafanya mpango wakahamisha hayo makaburi nyuma ya stendi Ndogo kisha eneo lote mpaka huku stendi ndogo likiwa stendi kubwa ya mabasi.Yaani kuanzia hapo stadium kote kunakuwa ni STAND.Inawezekana kabisa
Stendi zipelekwe nje ya mji zikasaidie kukuza maeneo ya pembezoni.
Miji mingine ilipata hii akili 20 years ago...
 
Wananchi jijini Arusha pamoja na abiria wanaotumia stand kubwa ya mabasi wamailalamikia uongozi wa jiji la Arusha kuwa wameshindwa kuwaletea mabadiliko kwa kuwajengea stand nyingine mpya ya kisasa tofauti na iliyopo sasa ambayo ipo tangu kabla ya uhuru hadi sasa.

Kutokana na udogo wa kituo hicho cha Mabasi umefanya baadhi ya makampuni kushusha na Kupakia abiria katika sehemu mbalimbali na wengine katika ofisi zao zilizopo sehemu tofauti tofauti jijini hapo na hivyo kuleta usumbufu kwa abiria na wageni kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Mfano gari za kwenda Namanga kuna ambazo zinapaki stand kubwa na. Nyingine nje ya uwanja wa mpira wa. Abeid karume.

Magari ya Kwenda Dar es Salaam kuna machache yanapaki ndani ya kituo hicho, mengine stand ndogo na. Mengine yamekuwa yakipakiza na kushusha abiria katika ofisi zao

Za kwenda karatu nazo kuna ambazo zinapaki ndani ya kituo na nyingine mbali na kituo hicho maeneo ya Sabena

Kituo hicho kikubwa cha mabasi hakina sehemu ya kusubiri abiria wala Wasindikizaji.

Hakuna sehemu ya kuwakinga na Mvua wala jua.

Na. Pia Usalama ni mdogo usiku na. Mchana kutokana na miundombinu ya kituo hicho cha mabasi na hivyo Kuwa na. Idadi kubwa ya vibaka, wezi, wavutaji wa madawa yote na vijana wa mitaani ambao ni tishio kwa wageni na abiria.

Wananchi wa jiji la Arusha wamekuwa wakilalamika miaka Nenda miaka rudi lakini hawaoni mabadiliko yoyote hadi sasa,kituo cha mabasi kilichopo hakiendani na hadhi ya jiji kwani jiji hili limekuwa likipokea wageni wengi ndani Na Nje ya nchi hivyo kituo hicho ambacho hakina uwezo hata wa kupaki mabasi (10)kumi kwa wakati mmoja, kinaharibu taswira ya jiji.
uwanja wa Abeid Karume ndio upi huo?wakazi gani hao wa Arusha wameyasema hayo
 
Hata hivyo Arusha ni mji mkubwa wenye eneo finyu angalau sasa hivi watakuwa wameongeza mipaka ya jiji na mbaya zaidi kule maeneo mengi yanamilikiwa na watu tangu enzi hizo na wanajua thamani ya ardhi hivyo hata serikali inapata wakati mgumu wa kupata maeneo ya shughuli za maendeleo zaidi ya kwenda pembezoni nako lazima walipe fidia ndefu
Kusema kuwa serikali inashindwa kupata maeneo ni kukiri kuwa udhaifu wa serikali. Mbona serikali ikitaka kufanya miradi kama ya barabara, umeme au maji chap chap wanafidia watu na kutekeleza miradi husika??

Iko hivi: Kinachotokea Arusha ni mgongano wa maslahi na fear of the unknown.
Unakuta viongozi wafanya maamuzi wamewekeza kwenye majengo na biashara nyingi zilizosongamana pale mjini.

Wazawa nao wanahofia mizunguko ikihama maisha yatakuwaje.

Tusishau vile vile historia mbaya ya Arusha uliotokana na ile mitandao ya uhalifu! Japo mambo yamebadilika lakini watu bado wana hofu! Kuna maeneo ikifika saa 12 na nusu jioni tayari hata usafiri unaanza kusua sua, maduka yashatiwa kufuli... Watu wana hofu!

Kwa mji unaojinasibu kuwa ni lango na kitovu cha utalii, serikali ya Jiji/mkoa inatakiwa iwaze ndani na nje ya boksi. Kinachoendelea sasa pale Arusha ni kero na aibu!

Kongole kwa A to Z, Braeburn, Bansal, Lenagro, Nida, Auwasa, n.k walioamua kujiwekeza kule nje ya mji.
 
Mjini kupoa pia ni maendeleo. Kwa sasa ule mji wa Arusha unatia kichefu chefu
shida kubwa ya tanzania ni planning. serikali imewaachia watu waendeleze miji kiholela, miji ikikua (kiholela) ndipo inajifnaya kuanza kujali
 
Ili mji wa Arusha upanuke na ukue kwa haraka wahusika wazingatie yafuatayo:
1. Ondoa stendi na masoko yale pale mjini kati.
2. Stendi mabasi ya kutoka Dodoma road inatakiwa iwe Kisongo. Weka soko huko.
3. Stendi mabasi kutoka Moshi road iwe USA au Chekereni. Weka soko huko.
4. Stendi magari kutoka Nairobi iwe Ngaramtoni ya Juu. Weka soko huko.
5. Stendi magari kutoka Simanjiro/Kiteto iwe Oljoro. Weka soko huko.

NB: Lakini msije mkalalamika kuwa stendi na masoko yako mbali!
🤣🤣 Hizo Zitakuwa stand au vituo vya daladala
 
Back
Top Bottom