Kila basi la abiria kupaki na kupakia abiria kwenye kituo chake pia ni chanzo cha ajali

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,148
7,724
Katika Jiji la DSM Mabasi yaendayo mikoani kupaki na kupakia abiria kwenye vituo vyao badala ya kupaki na kupakia katika kituo cha Mabasi cha MAGUFULI hilo pia linachangua ajali za barabarani.

Inashangaza Mamlaka husika kama LATRA kuacha kila basi kupaki na kupakia abiria kwenye vituo vyao badala ya kutumia Stendi maalum ya MAGUFULI.

Tunaziomba Mamlaka zipige marufuku kwa basi za abiria kupaki na kupakia abiria nje ya stendi ya magufuli. Basi zote za abiria zipakie abiria kwenye stendi ya Magufuli ili ziweze kukaguliwa na wakaguzi wa Magari.

Matajiri wa mabasi hawapo juu ya sheria, lazima sheria zifuatwe.
 
Unatembea na V8 ndo maana una hicho kiburi. Hivi unajua gharama ya kutoka magufuli kwenda gongo la mboto? Au kwenda kigamboni?

Siku moja naomba utolewe kwenye V8 utembee kwa miguu kuvuka tu ile barabara ya Moro road upande gari pale mbezi kwa kuingilia dirishani halafu utajielewa.
 
Kwahiyo Tanzania mabasi yasipita kituo cha Magufuli ndiyo yanayopata ajali! Huu ni ujinga, hatuwezi kulazimisha basi linalotoka Kigoma kwenda Mwanza lije Dar es Salaam lianzie safari Magufuli! Tutakuwa wendawazimu kama mwandishi wa Post hii.
 
Katika Jiji la DSM Mabasi yaendayo mikoani kupaki na kupakia abiria kwenye vituo vyao badala ya kupaki na kupakia katika kituo cha Mabasi cha MAGUFULI hilo pia linachqngia ajali za barabarani.

Inashangaza Mamlaka husika kama LATRA kuacha kila basi kupaki na kupakia abiria kwenye vituo vyao badala ya kutumia Stendi maalum ya MAGUFULI.

tunaziomba Mamlaka zipige marufuku kwa basi za abiria kupaki na kupakia abiria nje ya stendi ya magufuli.
Basi zote za abiria zipakie abiria kwenye stendi ya maguli ili ziweze kukaguliwa na wakaguzi wa Magari.

Matajiri wa mabasi hawapo juu ya sheria, lazima sheria zifuatwe.
Kwaiyo stand ya magufuli ina uchawi wa kizui ajali? Au unauza maji hapo stand unaona hayatoki?
 
Wakipaki kwny vituo vyao huwa wanatoboa matairi?
Kikubwa hata wakipandia wapi bus lazima lipite Magufuli au 88...
Labda ana maana Gari zinazo pakilia stend kuu huwa zinakaguliwa na Askari kujiridhisha kama gari imefanyiwa service kabla haijatoka. Tofaut na zile zinazo pakilia kwenye stend zao binafsi. Nilivyo muelewa mtoa mada
 
Lakini sisi mfano huku Dom iwe isiwe bus likipakia popote linatakiwa liiingie stand kuu na trafic ndo analiruhusu...yani ule muda uliondikwa bus linaondoka lazima liondokee stand kuu...
 
Siku zetu wanadamu ziko mikononi mwa Muumba wetu( Mwenyezi Mungu) Haijalishi gari limepakia wapi, limekaguliwa au halijakaguliwa, ajali haizuiliwi kwa kuwa Bus limefanyiwa Service au kwa sababu ya kukaguliwa bali ni mkono wa Mungu tu utukingao na hatari zote.

Hivyo kuanzia Safari Magufuli si kinga ya ajali ndugu yangu
 
Ulichoandika hakina mashiko. Ulijiuliza kabla hujaandika?
Bus la ester kupakiza abiria mbagala wanaosafiri na bus hilo kwenda moshi kunasababisha ajali?

Kwahiyo awaache abiria wake kule mbagala, wapande daladala waje wapandie Magufuli mbezi ndio ajali hakuna?!!!

Wewe jamaa
 
Katika Jiji la DSM Mabasi yaendayo mikoani kupaki na kupakia abiria kwenye vituo vyao badala ya kupaki na kupakia katika kituo cha Mabasi cha MAGUFULI hilo pia linachangua ajali za barabarani.

Inashangaza Mamlaka husika kama LATRA kuacha kila basi kupaki na kupakia abiria kwenye vituo vyao badala ya kutumia Stendi maalum ya MAGUFULI.

Tunaziomba Mamlaka zipige marufuku kwa basi za abiria kupaki na kupakia abiria nje ya stendi ya magufuli. Basi zote za abiria zipakie abiria kwenye stendi ya Magufuli ili ziweze kukaguliwa na wakaguzi wa Magari.

Matajiri wa mabasi hawapo juu ya sheria, lazima sheria zifuatwe.
Mimi naona uko sahihi kwenye kipengele kimoja tu cha mabasi kushusha abiria kwenye stendi kuu. Mabasi yote yangeanza na kuhitimisha safari zao kwenye hizo stendi kuu! Na baada ya hapo, basi ndiyo liende sasa kwenye ofisi zake huku likiwa na mizigo pekee. Na lengo hapa ni kuzisaidia tu hizo stendi kuwa active muda wote.

Ila kabla ya kufikia hatua hiyo, serikali inatakiwa pia kuimarisha miundombinu. Yaani usafiri wa kumfikisha abiria stendi kuu uwe ni wa uhakika! Wa haraka! Na upatikane ndani ya masaa yote 24.

Kwenye kusababisha ajali, nadhani hakuna uhusiano.
 
Katika Jiji la DSM Mabasi yaendayo mikoani kupaki na kupakia abiria kwenye vituo vyao badala ya kupaki na kupakia katika kituo cha Mabasi cha MAGUFULI hilo pia linachangua ajali za barabarani.

Inashangaza Mamlaka husika kama LATRA kuacha kila basi kupaki na kupakia abiria kwenye vituo vyao badala ya kutumia Stendi maalum ya MAGUFULI.

Tunaziomba Mamlaka zipige marufuku kwa basi za abiria kupaki na kupakia abiria nje ya stendi ya magufuli. Basi zote za abiria zipakie abiria kwenye stendi ya Magufuli ili ziweze kukaguliwa na wakaguzi wa Magari.

Matajiri wa mabasi hawapo juu ya sheria, lazima sheria zifuatwe.
Hebu fafanua zaidi mkuu.
Kupakia nje ya kituo kikuu kunachangiaje ajali?
 
Mimi naona uko sahihi kabisa kwenye kipengele kimoja tu cha mabasi kushusha abiria kwenye stendi kuu. Mabasi yote yangeanza na kuhitimisha safari zao kwenye hizo stendi kuu! Na baada ya hapo, basi ndiyo liende sasa kwenye ofisi zake huku likiwa na mizigo pekee.

Ila kabla ya kufikia hatua hiyo, serikali inatakiwa pia kuimarisha miundombinu. Yaani usafiri wa kumfikisha abiria stendi kuu uwe ni wa uhakika! Wa haraka! Na upatikane ndani ya masaa yote 24.

Kwenye kusababisha ajali, nadhani hakuna uhusiano.
Kwa nini hamtaki kuweka maslahi yenu wazi? Manataka kutumia kichaka cha ajali kwa lengo la kutafuta ulaji? Kwani basi likitoka na abiria kituo cha magufuli na kuwaacha linakoishia kunaletaje ajali? Uza bolt na Uber zako kama umekosa abiria kwa kutegemea wanaoshushwa Magufuli
 
Siku zetu wanadamu ziko mikononi mwa Muumba wetu( Mwenyezi Mungu) Haijalishi gari limepakia wapi, limekaguliwa au halijakaguliwa, ajali haizuiliwi kwa kuwa Bus limefanyiwa Service au kwa sababu ya kukaguliwa bali ni mkono wa Mungu tu utukingao na hatari zote.

Hivyo kuanzia Safari Magufuli si kinga ya ajali ndugu yangu
Una imani ya kipumbavu mnoo
 
Back
Top Bottom