Arusha: Rais Samia akishiriki Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 7, 2026

Arusha: Rais Samia akishiriki Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 7, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Arusha: Rais Samia akishiriki Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Machi 7, 2026


Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akichukua nafasi ya Rais wa Kenya, William Ruto, ambaye amemaliza muda wake wa uongozi wa mwaka mmoja.

Tukio hilo la makabidhiano ya vitendea kazi limefanyika leo, Machi 7, 2026, wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa EAC unaofanyika jijini Arusha.

Hii ni mara ya nne kwa Rais Museveni kushika wadhifa huo wa juu tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo, jambo linalomfanya kuwa mmoja wa viongozi wenye uzoefu mkubwa zaidi katika masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki.

Mara tu baada ya kupokea kijiti, Rais Museveni ameanza rasmi majukumu yake kwa kuongoza vikao vya Mkutano huo wa 25 wa Wakuu wa Nchi, ambapo ajenda kuu ni pamoja na usalama wa kikanda, biashara, na uzinduzi wa mifumo mipya ya forodha

Balozi Stephen Patrick Mbundi Ateuliwa kuwa Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Balozi Stephen Patrick Mbundi, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi wake, alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje akisimamia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kuanzia Bunge lijalo, Wabunge wa EAC kulipwa mishahafa na nchi zao

Katika hatua kubwa ya kupunguza matumizi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Wakuu wa Nchi wamepitisha uamuzi kuwa kuanzia Bunge lijalo la jumuiya hiyo (EALA), mishahara ya wabunge wa bunge hilo itagharamiwa na mataifa wanayotoka badala ya jumuiya.

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa EAC, William Ruto amebainisha hayo leo, Machi 7, 2026, jijini Arusha, wakati wa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), akieleza kuwa mishahara hiyo kwa sasa inachukua takriban 30% ya bajeti yote ya jumuiya.

Chini ya utaratibu huu mpya, EAC itabakiwa na jukumu la kulipa posho pekee pale wabunge hao wanapokuwa katika shughuli za kikazi za jumuiya, hali itakayookoa rasilimali nyingi kuelekezwa kwenye miradi ya kimaendeleo.

“Hatua hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa mzigo kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili tuweze kutumia rasilimali nyingi zaidi katika kuhakikisha tuna Jumuiya yenye ufanisi. Ni posho za wabunge pekee ndizo zitalipwa na EAC wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao, lakini mishahara italipwa na nchi zao binafsi”, ameeleza Ruto.

Kutokana na jumuiya kukua hadi kufikia nchi nane, mfumo wa awali wa kuhitaji makubaliano ya wote ulikuwa unachelewesha ufanisi. Sasa, maamuzi yatatolewa kwa makubaliano au kwa kura za 65% ya wanachama.

Ruto amesema kuwa mabadiliko haya ni muhimu kwa sababu sheria zilizoanzisha jumuiya hiyo ziliandikwa wakati kukiwa na nchi tatu pekee, hivyo hazikukidhi mahitaji ya sasa ambapo jumuiya inaendelea kutanuka.
 
Tunasikia Raisi Kajificha kizimkazi imekuaje tena?
 
Huenda wafanye yafuatayo:

1) Ethiopia should be invited to join the East African Community.

2) Lengthen the runway of Arusha Kisongo airport, to 4,000 metres. This will enable big planes that carry leaders to land in Arusha Kisongo.

3) Lengthen the runway of KIA airport to 4,000 metres. These two airports will greatly boost diplomatic infrastructure.

4) Create one single currency to cover the entire EAC and SADC area. This single currency should co-exist with national currencies, do not abolish the national currencies. The central bank for this single currency should be in Arusha.

5) Make the whole main road from Holili (on the Tanzanian-Kenyan border, via Moshi and Arusha) until Makuyuni (when the main road branches to Babati and to Ngorongoro gate), to become a double road.

6) Build a SGR rail from Nairobi to Arusha to Dodoma.

7) Make Arusha city a hub for international organisations like the EAC, SADC, AU, AfCFTA, UN, World Bank, IMF etc. And improve the infrastructure of Arusha city. Including tarmacking the road that goes into the AICC estate area, off Njiro Road.

8) The Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) should become the Eastern and Southern African Management University (ESAMU).

9) Tarmac the road from Ngorongoro park gate to Serengeti park gate to Musoma lake Victoria beach. This will boost tourism.

10) Change the labour laws in the EAC member states and in the EAC secretariat to be pro-young and also to accommodate Gen Zs.

Make the labour laws to allow for 50% part-time employment in the government civil service, and in the entire public sector (including in Universities and Colleges) and also in the corporate private sector. Also make the labour laws to allow for short-term contracts that range from 1 month to 12 months, whether full-time or part-time (50%), in the government civil service, in the public sector (including in Universities and Colleges), in public corporations, and in the corporate private sector.

Make internship programmes, graduate trainee programmes, graduate management trainee programmes (that employ young people with absolutely no work experience), mandatory, in the civil service, in the public sector, in public corporations, and in the corporate private sector.

Compulsory retirement age, in the government civil service, in the public sector (including in Universities and Colleges), in public corporations, and in the corporate private sector, should be increased from 60 years to 70 years. So as to accommodate young people, Gen Zs and Gen Xs, who are not yet successful in life.
 
Yaani jana nimejua tuna nchi la kijinga kweli 😔 Nimetoka Manyara kwenda Tanga yaani mimi wa kukaa road siku nzima?! Eti kuna msafara wa Viongozi! 😔
 
Back
Top Bottom