TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,343
- 3,704
Mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 11, darasa la sita anayefahamika kwa jina la Lightness Mkiindi, mkazi wa Mtaa wa Namayana, Kata ya Ilboru, wilayani Arumeru mkoani Arusha, amefariki dunia akidaiwa kujinyonga
Kwa mujibu wa maelezo ya mama mzazi na bibi wa marehemu, siku ya tukio Januari 29, mtoto huyo hakuenda shule kutokana na kuwepo kwa msiba wa jirani uliokuwa karibu na makazi yao, ambapo familia ilikuwa ikishiriki shughuli za maombolezo. Kabla ya tukio hilo, inaelezwa mtoto alikuwa nyumbani akicheza na wenzake.
Familia imesema walipokea taarifa ya dharura wakati wakiwa msibani, iliyomtaka mama wa mtoto kurejea nyumbani haraka. Alipofika, alikuta mtoto huyo tayari amefariki katika mazingira yanayoashiria alijinyonga kwa kutumia kanga ya kuogea.
"E baba Mungu ninaomba kwa niaba ya familia yangu na jamii nzima pamoja na majirani, Mungu naomba umpe bibi yangu hela pamoja na mama yangu pamoja na baba yangu, bibi yangu apate hela ya marejesho na baba na mama wapate hela ya ada ya shule. Mungu atusaidie, Milele Amina amefanya maajabu jina lake liimidiwe" ameandika mtoto ambaye anadaiwa kujinyonga bafuni.
Chanzo cha tukio hilo bado hakijabainika mara moja, huku tukio hilo likiacha majonzi makubwa kwa familia, ndugu na wakazi wa eneo hilo.