Arusha: Mtoto aliyetoroka kwao amepatikana na kueleza kilichotokea

Arusha: Mtoto aliyetoroka kwao amepatikana na kueleza kilichotokea

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
6,897
Reaction score
14,221
Kufuatia tukio la mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Murieti Jijini Arusha, aitwae Daniel Jeremia (15), kutoweka nyumbani kwao January 26, 2026, nakuacha ujumbe unaosema kuwa anamuonea mama yake huruma kwa namna anavyomuhangaikia maishani, hatimaye leo January 31, amepatikana na kusema alikuwa anafanya kazi za kubeba mizigo maeneo ya stendi na sokoni ili siku moja arejee kumsaidia mama yake aliyemuacha akiwa anaumwa.

"Niliondoka mama alikuwa anaumwa, tulikuwa hatuna hela ndani ikabidi aende tu hivyo hivyo kazini tu, hicho kitendo kikaniuma, anateseka kisa mimi, nilikuwa nimeenda tu pale stendi nilikuwa nabeba tu mizigo, nalala hapo hapoo, ningerudi tu nikishapata ela yakumsaidia mamaa" Mtoto Daniel akizungumza na mwandishi wa GADI TV kupitia simu ya mama yake huku akiwa analia.

Mama mzazi wa mtoto huyo amekiambia chombo cha habari "GADI TV" mwanae amepatikana baada mtu mmoja kumuona maeneo karibu na Kituo Kikuu cha Polisi Jijini humo na kisha kufananisha picha zilizokuwa mtandaoni, na alipohojiwa alikiri kuwa ni yeye.
1769865781291.jpg

Source: GADI TV
 
Huku kuna wanasiasa wanatapanya mabilioni ya walipa kodi bila huruma
Maisha ya watu wote hayawezi kuwa sawa.

Jambo la msingi ni kila mtu kuweka bidii katika eneo lake na kumtanguliza Mungu.
 
Maisha ya watu wote hayawezi kuwa sawa.

Jambo la msingi ni kila mtu kuweka bidii katika eneo lake na kumtanguliza Mungu.
Vipaumbele vyetu ni vipi? Kulipa mamalioni kwenye magoli ?
Kutuma watu Vatican kwa gharama za walipa kodi kusafisha uchafu usiosafishika?
 
Maisha ya watu wote hayawezi kuwa sawa.

Jambo la msingi ni kila mtu kuweka bidii katika eneo lake na kumtanguliza Mungu.
Maisha ya watu wote hayawezi kuwa sawa lakini yanaweza kuwa na unafuu, matokeo ya utafutaji na upataji yalingane na bidii ya mtu.
 
Back
Top Bottom