Arusha: Masheikh 6 wahukumiwa kunyongwa hadi kifo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

MASHEIKH SITA 6 WAHUKUMIWA KUNYONGWA ARUSHA LEO

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo tarehe 12/12/2023, imewasomea hukumu Masheikh tisa miongoni mwa wale wanaoshikiliwa na Serikali kwa zaidi ya miaka kumi katika Gereza Kuu la Kisonge Mkoani Arusha.

Masheikh hao wanatuhumiwa na Serikali kwa Ugaidi wa kulipua Kanisa Katoliki la Ole sita mkoani Arusha mwaka 2013.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Nkwabi aliwaachia huru Masheikh watatu ingawa mmoja miongoni mwao amerejeshwa jela kwa sababu ya kukabiliwa na tuhuma nyingine.

Walioachiwa huru ni: Abduli Humud Wagoba, Abdurahmani na Amani Mussa Pakasi (ambaye amerejeshwa gerezani).

Aidha Jaji Nkwabi alionesha kuridhishwa na ushahidi wa Polisi kwamba Masheikh sita katika shauri hilo akiwemo imamu mkuu wa Msikiti mashuhuri Masjid Quba Arusha, Sheikh Jaafar Hashim Lema waliripua Kanisa Katoliki na kusababisha madhara makubwa.

Kwa sababu hiyo Jaji Nkwabi aliamua kuwahukumu adhabu kali ya kunyongwa mpaka kufa.

Masheikh hao waliokaa gerezani kwa zaidi ya miaka kumi na hatimaye kuhukumiwa kifo ni:

1. Imam Jaafar Hashima Lema.
2. Yusuf Ali Huta
3. Ramadhani Hamadi Waziri.
4. Abdul Hassa Masta.
5. Kassim Idrisa. Na-
6. Abashari Hassan Omari.

Masheikh hao pamoja na wenzao kumi walio hukumiwa kunyongwa hivi karibuni mkoani Tanga, watanyongwa baada ya Rais Samia Suluhu Hassani kutia saini.

Pia, soma;

Mlipuko mkubwa watokea kwenye Kanisa Katoliki Arusha, watu kadhaa wajeruhiwa
 
Back
Top Bottom