Napinga Masheikh sita wa Kiislamu kupewa adhabu ya kunyongwa hadi kufa

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,102
2,717
Nimepita pale mahakamani jana nikamuona yule mama Analia,nikauliza,"Huyu analia nini?". Najua jambo kama lile siyo ajabu, lakini bado nikauliza,"Huyu analia nini?" Nikaambiwa,unajua, hii ni mahakama na yule mama ukimuona analia, basi, labda itakuwa mtoto wake amehukumiwa kifungo.

Wakamwambia yule mama unaweza kwenda ndani ukawaone kabla hawajaondolewa, lakini ukifika kule usilie.
Halafu mtu mmoja akasema, hapana, hawezi kwenda, yule askari hujamuona anafukuza watu?

Hii hukumu, unasema watu wachache wameuawa,na wachache tena,wamejeruhiwa. Haya mambo ya Kanisa kushambuliwa au Msikiti kuchomwa moto,haya mambo viongozi wa dini wanaweza kukutana, wakajadili.
Dini yetu ni moja, Abrahamic Faith.

Kuna sababu gani ya kuwafunga Masheikh ambao wameshakaa miaka kumi jela?

Kuhusu hukumu ya masheikh soma > Arusha: Masheikh 6 wahukumiwa kunyongwa hadi kifo
 
Nimepita pale mahakamani jana nikamuona yule mama Analia,nikauliza,"Huyu analia nini?".
Najua jambo kama lile siyo ajabu,lakini bado nokauliza,"Huyu analia nini?"

Kuna sababu gani ya kuwafunga Masheikh ambao wameshakaa miaka kumi jela?

Mashehe dini imewatoa akili wakaanza ugaidi,adhabu inawastahili kwa matendo ovu waliyofanya,uiicheka na magaidi utavuna maovu mengi.
 
Heading kunyongwa, body kufungwa!!

Kama wametenda jinai, na ushahidi upo, kuhukumiwa ni halali. Tena wao viongozi wa dini walitakiwa kuwa mfano katika kutenda mema.
Huyo ndio mtoto wa Nyerere. Mzee alituachia watoto vilaza sana. Huyu alifukuzwa pale Butiama kwa Mama na DC kwani anamsumbua Mama.
 
Kama nchi ingekuwa inaongozwa na sheria za kanisa, naamini kabisa hao mashekhe wangesamehewa na kuachiwa huru.

Bahati mbaya nchi inaongozwa na sheria zake, na kwa mujibu wa sheria hizo, hukumu waliyopewa hao mashekhe imetokana na ushahidi uliotolewa dhidi yao na mahakama kujiridhisha.

Haya mambo hayataki hisia, naamini kabisa hata wewe umekuja na huu mtazamo wako kwasababu ya kumuona huyo mama anayelia mahakamani.

Umesahau wapo wengine waliolia siku ile waliyopata taarifa za misiba ya ndugu zao waliokufa kwa mabomu kazi ya mikono ya hao mashekhe, na siku waliyowazika.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Endapo kama haujaridhika na Hukumu iliyotolewa basi kata rufaa ili kuwatetea.

Ukweli ni kwamba suala la matukio ya Makanisa kuvamiwa, kushambuliwa au kuchomwa Moto yamekuwa yakijirudia mara kwa mara hapa nchini Tanzania. Hukumu hii itakuwa ni fundisho kubwa kwa wahusika wa matukio ya namna hii.
 
Back
Top Bottom