Katekista Katoliki ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua Mlei

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411

ONYO: Mauaji haya ya watumishi wa madhabahuni yasihusishwe na dini yeyote ile, huu ni utashi wa mtu, japo sijasikia huko TAG wakiuana ama kubaka watoto>

Mahakama kuu kanda ya Iringa iliyofanya kikao chake mkoani Njombe imemhukumu kunyongwa hadi kufa Daniel Philipo Mwelango miaka (42),katekista na mkazi wa Makambako baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la mauaji ya kukusudia ya Nickson Elias Myamba (43) mkazi wa makambako mtaa wa Kahawa aliyekuwa katibu wa baraza la walei kanisa la Katoliki kigango cha Parokia ya Makambako.

Akisoma hukumu hiyo Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Iringa Said Kalunde amesema mshtakiwa alitekeleza mauaji hayo 8/2/2022 mtaa wa Bwawani katika duka la kanisa Katoliki kigango cha Makambako.

Jaji Kalunde amesema siku ya tukio mshitakiwa alifanya maandalizi kwa kuandaa Panga,Chuma pamoja na mifuko minne ya Kinganjaa,mifuko miwili ilikuwa kwa ajili ya kuzuia damu isisambe na miwili mingine kwa ajili kuhifadhi mwili wa marehemu.

Baada ya hapo akampiga na chuma kwenye kisogo baada ya kuona ameanguka chini na kufariki alimkata vipande viwili na kuvipaki katika mifuko ya kinganjaa ili iwe rahisi kubeba mwili huo na kwenda kuutupa mbali,baada ya kuona mke wa marehemu anapiga simu mara kwa mara kwenye simu ya Maherehemu pamoja mwenyekiti wa kigango alishindwa kuubeba mwili huo na kuamua kuondoka huku akiwa amelibeba panga na kwenda kulitumbukiza katika shimo la choo cha shule ya msingi Makambako na chuma alichotumia kumpiga nacho alikificha kwenye gata karibu na duka na yeye kutorokea Dar es Saalam.

Aidha Mh.Jaji amebainisha kuwa licha ya mshitakiwa kukiri kufanya kosa hilo kuwa hakukusudia,Mahakama kupitia upande wa mashtaka imejiridhisha pasina shaka juu ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo,Mahakama hiyo imemkuta mshitakiwa na hatia ya mauaji.

Jaji Kalunde amesema Kosa lililofanywa na mshitakiwa huyo ni Kinyume na kifungu cha sheria namba 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Kesi hii ya mauaji namba 74 ya mwaka 2022 kwa upande wa utetezi imesimamiwa na wakili Alex Mgani na kwa upande wa serikali imesimamiwa na wakili Magdalena Hyasint Whero ambaye aliiomba mahakama itoe adhabu kali dhidi mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine kwa wengine.

Pia soma
 
Mahakamani Kuu Kanda ya Iringa ambayo imefanya kikao mkoani Njombe, Desemba 11, 2023 imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Daniel Philipo Mwelango (43) ambaye alikuwa Katekista wa Kanisa katoliki #Makambako mkazi wa Makambako kwa kosa la mauaji baada ya kukutwa na hatia.

Mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo Februari 8, 2022 kwa kumuua Daniel Elias Myamba (43) mkazi wa mtaa wa Kahawa Makambako kesi Na MC 74/2022 katika mtaa wa Bwawani mjini Makamabako.

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Jaji Said Kalunde.

Akisoma hukumu hiyo Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Iringa amesema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote kwamba mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo.

Jaji Kalunde amesema siku ya tukio mshitakiwa alifanya maandalizi kwa kuandaa Panga,Chuma pamoja na mifuko minne ya Kinganjaa,mifuko miwili ilikuwa kwa ajili ya kuzuia damu isisambe na miwili mingine kwa ajili kuhifadhi mwili wa marehemu.

Baada ya hapo akampiga na chuma kwenye kisogo baada ya kuona ameanguka chini na kufariki alimkata vipande viwili na kuvipaki katika mifuko ya kinganjaa ili iwe rahisi kubeba mwili huo na kwenda kuutupa mbali, baada ya kuona mke wa marehemu anapiga simu mara kwa mara kwenye simu ya Marehemu pamoja Mwenyekiti wa Kigango alishindwa kuubeba mwili huo na kuamua kuondoka huku akiwa amelibeba panga na kwenda kulitumbukiza katika shimo la choo cha Shule ya Msingi Makambako na chuma alichotumia kumpiga nacho alikificha kwenye gata karibu na duka na yeye kutorokea Dar es Saalam.
 
Duh sababu ya unyama huo ni nini?

Aise,tukio utafikiri zile movie za wrong turn

Ova
 
Back
Top Bottom