Arusha halisi ilivyo na watu wake

Arusha halisi ilivyo na watu wake

Chuki zako kwa Arusha dhahiri kabisa..

Hivi kwenye huu uzi wewe kimekuchukiza kipi?? Tumekuombeni msifie mji wetu?? Tumesema wapi ni lazima nyie msifie mji wetu?? Ni vibaya sisi kuamua kusifia mji wetu?? Tumeomba wapi validation ya ninyi ku approve mji wetu ni mzuri kama tunavyousifia??

Naomba unijibu hayo maswali...
Chuki imetoka wapi? Mimi nimeuliza tu kwanini mnatumia nguvu? Acheni watu waje wajionee.
 
Kwa kiasi kikubwa katoa taarifa chanya sahihi japo ina kasoro chache.Upande wa pili wa Shilingi Arusha ina mambo mengi ya hovyo usiyowezaa kuyapata popote Tanzania.Maeneo kama Unga LTD onyesha ilivyo,Arusha ni baadhi ya maeneo machache yaliyopo Tanzania unayoweza kunyang'anywa chochote mchana kweupe,ukapigwa na kisu risasi na wenyeji wanaona ni jambo la kawaida.Arusha kuna eneo ambalo ukiamua kuwa mzinzi unauliza tu ni wapi napata malaya,unaonyeshwa na kununua kirahisi kuliko unavyoweza kununua nyanya Iringa,Mbeya au Lushoto.

Mapungufu ya Arusha ni mapungufu yetu tuyaondoe.

Ila kwa hali ya hewa na mandhari ni moja kati ya maeneo unayofurahia uumbaji wa MUNGU.Ni moja kati ya maeneo unayoona fahari kuzaliwa Tanzania na kuwashangaa wanaotamani wangezaliwa mbwa Ulaya au Marekani.
Unachokiona pale Shivaz Mrina kiko kila mkoa wa nchi hii... Hakuna Mkoa ambako huwezi kununua malaya kwa pesa yako tena wakiwa wamejikusanya eneo moja wewe unachagua unayemtaka...

Kuhusu uhalifu uliousema, kupigwa risasi hadharani au kuchomwa kisu na kufariki hadharani hizo ni lazima ziwe ni published news, sasa tuwekee hao watu walioporwa kwa kupigwa risasi hapa Arusha.. Tuwekee hata link tu tujionee..
 
Chuki imetoka wapi? Mimi nimeuliza tu kwanini mnatumia nguvu? Acheni watu waje wajionee.
Tumeomba mtu yeyote aje ajionee na a prove tunachokisema??

Kitu pekee ambacho Wakenya wanatushinda Watanzania kwenye Utalii ni hicho.. Wenzetu wanajitangaza sana huko duniani sisi tumekaa kama mazoba tukijidanganya watakuja tu... Sisi tunavyosifia na kuweka vitu mbalimbali vya kusifia mkoa wetu utajuaje ndio itakuwa nyenzo ya kushawishi watu waje kutembelea Arusha??
 
Kila jambo unataka ushahidi "link",waulize wakazi wa Arusha.Ukiambiwa Mbeya walichuna ngozi ya binadamu,kupigwa nondo utataka pia "link".Sina ushahidi huo ndugu ila ninayoyasema yapo Arusha.Maana hata unywaji wa gongo utataka ushahidi.Ukizikataa kasoro zilizopo hutapaboresha.
 
Kila sehemu kuna matatizo yake ,changamoto za Arusha sana ziko kwenye shilingi kuisaka kila mtu mjanja ukiwa mshamba unalizwa peupe ,hata hao wa visu ,silaha ni wana mambo yao ya kipesa sio unatembea mtu anakuvamia hiyo hapana kabisaaaa
 
Mkuu, Mwanza juzi watu wamechinjwa msikitini imeripotiwa, Tanga pia iliripotiwa.. Majambazi wameua kwenye vibanda vya Mpesa huko Kilwa imeripotiwa, Majambazi kuvamia watu na kuua Geita na Shinyanga inaripotiwa, Majambazi wanaotumia bodaboda kuua na kupora pesa Dar inaripotiwa... Lakini Arusha mtu kupigwa risasi mchana kweupe mbele ya hadhara ya watu tukio lisiripotiwe?? Give me a space man....
 
Si ndio hapo mkuu, uporaji mdogo mdogo upo kila mahali dunia hii... Ila ninachompinga mimi na hapo anasema eti mtu anapigwa risasi mchana kweupe na watu hawasaidii ni kawaida kutokea Arusha...
 
Mkuu, Mwanza juzi watu wamechinjwa msikitini imeripotiwa, Tanga pia iliripotiwa.. Majambazi wameua kwenye vibanda vya Mpesa huko Kilwa imeripotiwa, Majambazi kuvamia watu na kuua Geita na Shinyanga inaripotiwa, Majambazi wanaotumia bodaboda kuua na kupora pesa Dar inaripotiwa... Lakini Arusha mtu kupigwa risasi mchana kweupe mbele ya hadhara ya watu tukio lisiripotiwe?? Give me a space man....
Unayaongelea ya leo tu au maisha ya kila siku ya jamii husika? Ningekuwa hakimu kama wew ningeomba ushahidi wa hayo pia.Ninaangalia je hatua zimechukuliwa kuyatatua?

Wapenda sana kiingereza,mie sikiwezi.Inafaa kutochanganya lugha maana Kiswaglish hakijawa rasmi.
 
Serengeti haipo Arusha,na mleta mada hoja yake kuu anauzungumzia mkoa wa Arusha,sasa suala la kuzungumzia vitu vilivyo karibu mkoa wako na kuvifanya ndio advantage ya mkoa wako hiyo ni irrelevant na hoja yenyewe na yeye mwenyewe mwanzo kabisa amesema hana lengo la kuulinganisha mkoa wa Arusha na mkoa mwingine,so alichopaswa kuzungumzia yeye ni mkoa wa Arusha tu,kama kuwa karibu na Serengeti basi mwanza wako karibu zaidi kuliko Arusha,yeye alipaswa kuzungumzia ni vile vilivyomo Arusha na uzuri wa Arusha tu na maeneo yake kama vile karatu,kwa mrombo,oljoro ,ikidinga, maji ya chai,usa river,ngulelo,ngaramtoni.kisongo,monduli,muriet,majengo,mbauda ,njiro,moshono,kijenge,tengeru,na kwingineko
soma habari yote kasema karibu
 
Kuna mjapani alijenga hoja kuwa tunawezaje kujenga uzalendo kwa taifa bila ya kuwa na uzalendo kwa kijiji chako, kata yako , wilaya na mkoa wako? hili nalo linafikirisha, hapa hakumaanisha ukabila ila pale unapoishi, tujitolee kuendeleza maeneo yetu na tujivunia na kushindana na maeneo mengine , hapo tutakuwa tunajenge uzalendo kuanzia chini.
 
kennedy_school.jpg

89403008.jpg

89402819.jpg

Mnaweza kudhani hiyo ni Hotel ya kitalii kumbe ni shule ya St. Constantine International Burka hapo ndio tulipofikia mabilioneea wa Arusha
Baba tuwekee na Precious blood na Henry Gorgaty
 
Unayaongelea ya leo tu au maisha ya kila siku ya jamii husika? Ningekuwa hakimu kama wew ningeomba ushahidi wa hayo pia.Ninaangalia je hatua zimechukuliwa kuyatatua?

Wapenda sana kiingereza,mie sikiwezi.Inafaa kutochanganya lugha maana Kiswaglish hakijawa rasmi.
Ukishaona mtu anahama kwenye hoja na kukimbilia vitu visivyohusika ujue ameshindwa kutetea hoja yake...

Ukiona mtu badala ya kujibu maswali, yeye anarudisha swali kwa swali ujue pia hoja zimemshinda..

Kama utataka kuendelea, Plz naomba pia uniwekee hapa hata matukio ya ujambazi wa silaha yaliyotokea Arusha kwa mwaka huu..
 
Habari zenu wadau.

Kwanza naomba niseme huu uzi hauna lengo la kuilinganisha Arusha na mkoa wowote Tanzania pia nataka huu uzi utumike kama reference kwa threads zote zitakazouongelea mji wa Arusha.

Dhumuni la kuuanzisha uzi huu ni kutokana na wimbi kubwa la members huku kuusema mji wa Arusha kwa namana tofauti ambazo pengine kutokana na kuwa sio wakazi wa Arusha wanaweza wasiwe sahihi sana.

MAMBO YA KIPEKEE KUHUSU MKOA WA ARUSHA.

1. Hati rasmi za uhuru wa Tanzania zilitiwa sahihi hapa na Uingereza mwaka 1961.

2. Azimio la Arusha la kujitegemea lilipitshwa mjini hapa karibu na maeneo ya mnara wa saa.

3. Makubaliano ya Arusha accords ya kusitisha vita nchini Rwanda yalipitishwa mjini Arusha mwaka 1993.

4. Una mbuga nyingi barani Africa, Hali ya hewa ni nzuri sana. Mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro, Ziwa Manyara, Olduvai Gorge, Arusha National Park,Tarangire na mlima Kilimanjaro zipo ndani\karibu na mji huu.

5. Arusha imechezwa movie ya Hollywood maarufu kama HATARI mwaka 1962.....Hatari! (pronounced [hɑtɑri], Swahili for "Danger!") is a 1962 Americanaction/adventure romantic drama film directed by Howard Hawks and starringJohn Wayne. It portrays a group of professional wildlife catchers in Africa.[2]The film includes dramatic wildlife chases and the scenic backdrop of Mount Meru, Arusha a dormant volcano.

6. Wakati mikoa yote inahangaika na madawati likiwemo jiji kuu la Dar, Arusha haikuwahi kuwa na upungufu wa dawati hata moja na kila secondary school inayo maabara hata kabla ya agizo la Rais. (shule nyingi za serikali za Arusha zina computer labs)

7. Arusha ndio mkoa wenye matumizi makubwa ya Internet kuliko Mkoa wowote Tanzania and East Africa.

8. Arusha ni mkoa wa kwanza kwa Social Development Index (Huduma Bora za Kijamii kama maji, life expetancy, Health services, Education) By UNDP

9. Arusha ndio mkoa unaofatia ukitoka Dar kwa wingi wa viwanda na kuchangia katika pato la Taifa.

10. Arusha ndio mkoa wenye gharama za juu za maisha kuliko mkoa wowote Tanzania, kama unataka kuanzia maisha Arusha na una uhakika hauna kipato cha kujitosheleza nakushauri ujaribu Mwanza.

CHANGAMOTO ZA JIJI LA ARUSHA

1. Roads Roads Roads, Barabara Arusha zipo nyingi ila ni nyembamba kutokana na mji huu kuwa na masterplan ambayo ni ya muda mrefu, Maeneo ambayo yanatakiwa kuwekewa mkazo ni pamoja na Olasiti, Olasiver, Englesheraton, USARiver, Moshono, Kisongo, Ngaramtoni ambapo ndipo mji unaelekea.

Mimi kama kama mzaliwa Arusha na nimetembea mikoa yote sio kupita kwa bus wala kukaa siku 2 bali nimeishi mikoa mingi kwa kweli, nimekuja koconclude Arusha ni ya kipekee sana kuanzia tabia za watu wa Arusha ni tofauti 100% na watanzania wote, Maisha ya watu wa Arusha ni tofauti na mikoa mingine na hata wa mikoani wakija Arusha wanakiri maisha ya Arusha na watu wake ni wa tofauti.

#Arusha #GenevaOfAfrica #SafariCity #UN #A-Town #Machalii #Mamong'oo #Arachugga #Mabillionare #Meli #Mafogo #MjiWaMabilionea #HalfLondon #TheOnly #MjiWaWajanja #Tanzanite #HeadQuaters #EastAfricaCommunity #Zurich #TanzaniteInTheSky #Wakakamavu #ChaliAraa #Jombii #Ungalelo #Matejoo #Ungalimii #Arifu #Makamanda #USARiver #Watengwa #Weusi #Nako2Nako
tumeisha kusamee mkuu
 
Tumeomba mtu yeyote aje ajionee na a prove tunachokisema??

Kitu pekee ambacho Wakenya wanatushinda Watanzania kwenye Utalii ni hicho.. Wenzetu wanajitangaza sana huko duniani sisi tumekaa kama mazoba tukijidanganya watakuja tu... Sisi tunavyosifia na kuweka vitu mbalimbali vya kusifia mkoa wetu utajuaje ndio itakuwa nyenzo ya kushawishi watu waje kutembelea Arusha??
sasa chuki yangu iko wapi? siwezi kuichukia arusha kwasababu uwepo wake hauniathiri sana sana unaninufaisha.
 
sasa chuki yangu iko wapi? siwezi kuichukia arusha kwasababu uwepo wake hauniathiri sana sana unaninufaisha.
Juzi nilikuona tu na ile mention yake ila nikaamua kukupotezea..

Nilikuwa najua dhahiri ulichokuwa unakitaka..
 
Juzi nilikuona tu na ile mention yake ila nikaamua kukupotezea..

Nilikuwa najua dhahiri ulichokuwa unakitaka..
Tafsiri zipo tofauti. Unaweza kuona glass half full au glass half empty.....jibu ulilolitoa ndio jibu sahihi kwa maudhui ya swali langu. Hata leo nimeshangaa kukuona humu ndio maana nikakuquote.
 
Tafsiri zipo tofauti. Unaweza kuona glass half full au glass half empty.....jibu ulilolitoa ndio jibu sahihi kwa maudhui ya swali langu. Hata leo nimeshangaa kukuona humu ndio maana nikakuquote.
Mkuu sitaacha kuusifia mkoa wangu hata siku moja... Wewe humu ikitajwa vibaya Range Rover au Dar lazima ufike kutetea, lakini ajabu hupendi wengine tusifie vyetu...

Mimi kusifia Arusha haiwi ndio kuulinganisha Mkoa wangu na sehemu nyingine..
 
Aise mleta mada emebadilisha mitazamo ya wengi waliokua hawajawahi kufika Arusha alafu wanaichukulia poa.

Arusha ni next level na hizo under construction projects ndio zinaenda kuipaisha Chugga highest.
 
Back
Top Bottom