Arusha halisi ilivyo na watu wake

hasason

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
1,648
1,539
Habari zenu wadau.

Kwanza naomba niseme huu uzi hauna lengo la kuilinganisha Arusha na mkoa wowote Tanzania pia nataka huu uzi utumike kama reference kwa threads zote zitakazouongelea mji wa Arusha.

Dhumuni la kuuanzisha uzi huu ni kutokana na wimbi kubwa la members huku kuusema mji wa Arusha kwa namana tofauti ambazo pengine kutokana na kuwa sio wakazi wa Arusha wanaweza wasiwe sahihi sana.

MAMBO YA KIPEKEE KUHUSU MKOA WA ARUSHA.

1. Hati rasmi za uhuru wa Tanganyika zilitiwa sahihi hapa na Uingereza mwaka 1961.

2. Azimio la Arusha la kujitegemea lilipitshwa mjini hapa karibu na maeneo ya mnara wa saa.

3. Makubaliano ya Arusha accords ya kusitisha vita nchini Rwanda yalipitishwa mjini Arusha mwaka 1993.

4. Wameru kwa kupitia organisation yao waliyoiunda ndio watanzania wakwanza kudai uhuru wao UN muda mrefu kabla ya Nyerere.
Unamfahamu Japhet Kiliro ?? Pitia historia ya Tanzania! Utakuta habari hii Alienda kuomba uhuru wa Wameru UNO... Lingine ni kuwa Wameru walifungua kesi Queens Bench kudai ardhi yao kesi hii maarufu inaitwa "Meru Land case"

5. Una mbuga nyingi barani Africa, Hali ya hewa ni nzuri sana. Mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro, Ziwa Manyara, Olduvai Gorge, Arusha National Park,Tarangire na mlima Kilimanjaro zipo ndani\karibu na mji huu.

6. Arusha imechezwa movie ya Hollywood maarufu kama HATARI mwaka 1962.....Hatari! (pronounced [hɑtɑri], Swahili for "Danger!") is a 1962 Americanaction/adventure romantic drama film directed by Howard Hawks and starringJohn Wayne. It portrays a group of professional wildlife catchers in Africa.[2]The film includes dramatic wildlife chases and the scenic backdrop of Mount Meru, Arusha a dormant volcano.

7. Wakati mikoa yote inahangaika na madawati likiwemo jiji kuu la Dar, Jiji la Arusha halikuwahi kuwa na upungufu wa dawati hata moja na kila secondary school inayo maabara hata kabla ya agizo la Rais. (shule nyingi za serikali za Arusha zina computer labs)

8. Arusha ndio mkoa wenye matumizi makubwa ya Internet kuliko Mkoa wowote Tanzania and East Africa.

9. Arusha ni mkoa wa kwanza kwa Social Development Index (Huduma Bora za Kijamii kama maji, life expetancy, Health services, Education) By UNDP

10. Arusha ndio mkoa unaofatia ukitoka Dar kwa wingi wa viwanda na kuchangia katika pato la Taifa.

11. Arusha ndio mkoa wenye gharama za juu za maisha kuliko mkoa wowote Tanzania, kama unataka kuanzia maisha Arusha na una uhakika hauna kipato cha kujitosheleza nakushauri ujaribu Mwanza.

12. Arusha kuna plate number za rangi ya blue au kijani ambazo matrafic police ambao ngeli haipandi hazipigi mkono pia watu hudable bei kama wamekuja kwenye business zao wanawachukuliwa class fulani (wakazi wa Arusha wananielewa)

CHANGAMOTO ZA JIJI LA ARUSHA

1. Roads Roads Roads, Barabara Arusha zipo nyingi ila ni nyembamba kutokana na mji huu kuwa na masterplan ambayo ni ya muda mrefu, Maeneo ambayo yanatakiwa kuwekewa mkazo ni pamoja na Olasiti, Olasiver, Englesheraton, USARiver, Moshono, Kisongo, Ngaramtoni ambapo ndipo mji unaelekea.

Mimi kama kama mzaliwa Arusha na nimetembea mikoa yote sio kupita kwa bus wala kukaa siku 2 bali nimeishi mikoa mingi kwa kweli, nimekuja koconclude Arusha ni ya kipekee sana kuanzia tabia za watu wa Arusha ni tofauti 100% na watanzania wote, Maisha ya watu wa Arusha ni tofauti na mikoa mingine na hata wa mikoani wakija Arusha wanakiri maisha ya Arusha na watu wake ni wa tofauti.


#Arusha #GenevaOfAfrica #SafariCity #UN #A-Town #Machalii #Mamong'oo #Arachugga #Mabillionare #Meli #Mafogo #MjiWaMabilionea #HalfLondon #TheOnly #MjiWaWajanja #Tanzanite #HeadQuaters #EastAfricaCommunity #Zurich #TanzaniteInTheSky #Wakakamavu #ChaliAraa #Jombii #Ungalelo #Lakuchumpa #Matejoo #Ungalimii #Arifu #Makamanda #USARiver #Watengwa #Weusi #Nako2Nako #USARiverSatelliteCity
 
4404237782_6b3f620485_b.jpg



05ArushatorchInn.jpg
 
Wee ni muongo sana ,unasifia kwenu mpaka unapitiliza na vya wenzenu unafanya vya kwenu hapo namba 4 umeitaja mbuga ya serengeti kwamba ipo Arusha ni uongo, Serengeti haipo Arusha, Serengeti ipo mkoa wa Mara,sema tu watalii wengi hupenda kuanzia safari ya kwenda huko kwa kutokea Arusha.
 
Wee ni muongo sana ,unasifia kwenu mpaka unapitiliza na vya wenzenu unafanya vya kwenu hapo namba 4 umeitaja mbuga ya serengeti kwamba ipo Arusha ni uongo, Serengeti haipo Arusha, Serengeti ipo mkoa wa Mara,sema tu watalii wengi hupenda kuanzia safari ya kwenda huko kwa kutokea Arusha.
Hatutaki ligi soma uelewe...amesema zipo ndani ama karibu na mji wa arusha sasa Serengeti inaangukia upande wa karibu na mji wa arusha
 
kwenye namba tisa hapo..katika kuchangia pato la taifa umedanganya mzee.....mkoa unaofuatia kwa kuchangia pato la Taifa ni Mwanza then Mbeya na mingine ila Arusha kwenye top 5 haipo..ila top 10 ipo....Rejea ripot ya banki kuu mwaka 2015 kuonesha mikoa inayochangia zaidi pato la Taifa

Tuwekee hiyo report hapa ikitoka kwenye websites za BOT ama yenye alama ya BOT iliyosainiwa na Ndulu 2015 inayoyasema hayo unayosema
 
Back
Top Bottom