Arusha halisi ilivyo na watu wake

Arusha halisi ilivyo na watu wake

Arusha in next few days to come, jiji linaenda kumeremeta

Arusha.jpg


Barabara.jpg


road06.jpg
 
mtu akianziasha vithread vyake vya kisorosoro sijui anafananisha Geneva na uchafu gani mlete huku kwenye huu uzi akatwe ngebe... hahahahaaaaa
 
Hii ndio Hotel ambayo kila mtu inamuacha hoi.....

Ngurdoto Mountain Lodge ...........

ngurdoto-mountain-lodge-back.jpg


ngurdotomountainlodge1.jpg


ngurdoto-mountain-lodge2.jpg



The-Ngurdoto-Mountain-Lodge-Tanzania.jpg


ngurdoto-lodge-12.jpg


50270209.jpg


ngurdotomountainlodge5.jpg
Hotel hii in jiran na nyumbani kwangu hapa USA RIVER....na huku ndani kabla hujavuka gate LA kuingilia arusha national park kuna hotel za maana sana...
 
Ni fahar sana kuwa mzaliwa wa Arusha au kuishi Arusha, wala haihitaji degree kutambua hilo ndio sababu kila siku mada zinazohusu Arusha haziishi humu jamvini.

Umemaliza
 
Mbona watu wanaupita kama hawauoni statistics zinaonyesha unasomwa sana ila comment noma sababu hawana la kuongea. Huwezi kuja Arusha siku mbili alafu na wewe eti unauongelea mji wa Arusha never.

Mleta mada upo njema.
MTU yuko ileje nae anadai anaijua arusha
 
Hotel hii in jiran na nyumbani kwangu hapa USA RIVER....na huku ndani kabla hujavuka gate LA kuingilia arusha national park kuna hotel za maana sana...
Master nilishafika huko Momela majumba ni ya hatari alafu watu wanasema Arusha palipojengwa ni njiro. USA River imejengwa sana nyumba zimeachiana nafasi kuubwa sio mbanano kama watu wanavyozoea

Na Arusha watu hawapendi kubanana kabisa alafu wanapenda garden hatari hasa Meru. Kuna jamaa tulikua tunasoma nae chuo kila weekend lazima aende home kwao ukimuuliza kufanyaje anasema kukatia fance na garden hahahahaa
 
Master nilishafika huko Momela majumba ni ya hatari alafu watu wanasema Arusha palipojengwa ni njiro. USA River imejengwa sana nyumba zimeachiana nafasi kuubwa sio mbanano kama watu wanavyozoea

Na Arusha watu hawapendi kubanana kabisa alafu wanapenda garden hatari hasa Meru. Kuna jamaa tulikua tunasoma nae chuo kila weekend lazima aende home kwao ukimuuliza kufanyaje anasema kukatia fance na garden hahahahaa
Hiloa garden nami nimewakubari wameru..wanapenda sana kutunza mazingira...huku mji ndo unakua kwa kasi sana...maeneo yote ya arusha university kupo poa sana mandhari mazuri sana...huku ngurdoto kuna makasri ya hatari watu wametulia,vijana wanapiga kazi na kujipatia kipato halali...
 
Hiloa garden nami nimewakubari wameru..wanapenda sana kutunza mazingira...huku mji ndo unakua kwa kasi sana...maeneo yote ya arusha university kupo poa sana mandhari mazuri sana...huku ngurdoto kuna makasri ya hatari watu wametulia,vijana wanapiga kazi na kujipatia kipato halali...
Huko ndio nataka kuzeekea hamna stress kabisa.
 
Arusha ni shidaaa!nimeishi maeneo ya SAKINA kwa mzee wangu Kavishe.ukweli ni kuwa kama huifahamu Arusha potea kwenye huu uzi.kama unapenda kujifunza kitu kuhusu AR basi salia humu.
 
najua watakupinga tu..

Kwa kiasi kikubwa katoa taarifa chanya sahihi japo ina kasoro chache.Upande wa pili wa Shilingi Arusha ina mambo mengi ya hovyo usiyowezaa kuyapata popote Tanzania.Maeneo kama Unga LTD onyesha ilivyo,Arusha ni baadhi ya maeneo machache yaliyopo Tanzania unayoweza kunyang'anywa chochote mchana kweupe,ukapigwa na kisu risasi na wenyeji wanaona ni jambo la kawaida.Arusha kuna eneo ambalo ukiamua kuwa mzinzi unauliza tu ni wapi napata malaya,unaonyeshwa na kununua kirahisi kuliko unavyoweza kununua nyanya Iringa,Mbeya au Lushoto.

Mapungufu ya Arusha ni mapungufu yetu tuyaondoe.

Ila kwa hali ya hewa na mandhari ni moja kati ya maeneo unayofurahia uumbaji wa MUNGU.Ni moja kati ya maeneo unayoona fahari kuzaliwa Tanzania na kuwashangaa wanaotamani wangezaliwa mbwa Ulaya au Marekani.
 
Habari zenu wadau.

Kwanza naomba niseme huu uzi hauna lengo la kuilinganisha Arusha na mkoa wowote Tanzania pia nataka huu uzi utumike kama reference kwa threads zote zitakazouongelea mji wa Arusha.

Dhumuni la kuuanzisha uzi huu ni kutokana na wimbi kubwa la members huku kuusema mji wa Arusha kwa namana tofauti ambazo pengine kutokana na kuwa sio wakazi wa Arusha wanaweza wasiwe sahihi sana.

MAMBO YA KIPEKEE KUHUSU MKOA WA ARUSHA.

1. Hati rasmi za uhuru wa Tanzania zilitiwa sahihi hapa na Uingereza mwaka 1961.

2. Azimio la Arusha la kujitegemea lilipitshwa mjini hapa karibu na maeneo ya mnara wa saa.

3. Makubaliano ya Arusha accords ya kusitisha vita nchini Rwanda yalipitishwa mjini Arusha mwaka 1993.

4. Una mbuga nyingi barani Africa, Hali ya hewa ni nzuri sana. Mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro, Ziwa Manyara, Olduvai Gorge, Arusha National Park,Tarangire na mlima Kilimanjaro zipo ndani\karibu na mji huu.

5. Arusha imechezwa movie ya Hollywood maarufu kama HATARI mwaka 1962.....Hatari! (pronounced [hɑtɑri], Swahili for "Danger!") is a 1962 Americanaction/adventure romantic drama film directed by Howard Hawks and starringJohn Wayne. It portrays a group of professional wildlife catchers in Africa.[2]The film includes dramatic wildlife chases and the scenic backdrop of Mount Meru, Arusha a dormant volcano.

6. Wakati mikoa yote inahangaika na madawati likiwemo jiji kuu la Dar, Arusha haikuwahi kuwa na upungufu wa dawati hata moja na kila secondary school inayo maabara hata kabla ya agizo la Rais. (shule nyingi za serikali za Arusha zina computer labs)

7. Arusha ndio mkoa wenye matumizi makubwa ya Internet kuliko Mkoa wowote Tanzania and East Africa.

8. Arusha ni mkoa wa kwanza kwa Social Development Index (Huduma Bora za Kijamii kama maji, life expetancy, Health services, Education) By UNDP

9. Arusha ndio mkoa unaofatia ukitoka Dar kwa wingi wa viwanda na kuchangia katika pato la Taifa.

10. Arusha ndio mkoa wenye gharama za juu za maisha kuliko mkoa wowote Tanzania, kama unataka kuanzia maisha Arusha na una uhakika hauna kipato cha kujitosheleza nakushauri ujaribu Mwanza.

CHANGAMOTO ZA JIJI LA ARUSHA

1. Roads Roads Roads, Barabara Arusha zipo nyingi ila ni nyembamba kutokana na mji huu kuwa na masterplan ambayo ni ya muda mrefu, Maeneo ambayo yanatakiwa kuwekewa mkazo ni pamoja na Olasiti, Olasiver, Englesheraton, USARiver, Moshono, Kisongo, Ngaramtoni ambapo ndipo mji unaelekea.

Mimi kama kama mzaliwa Arusha na nimetembea mikoa yote sio kupita kwa bus wala kukaa siku 2 bali nimeishi mikoa mingi kwa kweli, nimekuja koconclude Arusha ni ya kipekee sana kuanzia tabia za watu wa Arusha ni tofauti 100% na watanzania wote, Maisha ya watu wa Arusha ni tofauti na mikoa mingine na hata wa mikoani wakija Arusha wanakiri maisha ya Arusha na watu wake ni wa tofauti.

#Arusha #GenevaOfAfrica #SafariCity #UN #A-Town #Machalii #Mamong'oo #Arachugga #Mabillionare #Meli #Mafogo #MjiWaMabilionea #HalfLondon #TheOnly #MjiWaWajanja #Tanzanite #HeadQuaters #EastAfricaCommunity #Zurich #TanzaniteInTheSky #Wakakamavu #ChaliAraa #Jombii #Ungalelo #Matejoo #Ungalimii #Arifu #Makamanda #USARiver #Watengwa #Weusi #Nako2Nako
MARA.
http://www.wildafrica.com.au/wp-content/uploads/2012/12/Serengeti-National-Park-wide-1024x415.jpg
 
Mkuu mbona mnatumia nguvu sana....si muache tu waje watembee waone na watoe maoni yao....ila bado Arusha itafika tu.
Chuki zako kwa Arusha dhahiri kabisa..

Hivi kwenye huu uzi wewe kimekuchukiza kipi?? Tumekuombeni msifie mji wetu?? Tumesema wapi ni lazima nyie msifie mji wetu?? Ni vibaya sisi kuamua kusifia mji wetu?? Tumeomba wapi validation ya ninyi ku approve mji wetu ni mzuri kama tunavyousifia??

Naomba unijibu hayo maswali...
 
Back
Top Bottom