Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Serikali yetu imechangia kuuwa mji wa Arusha, kwa nini walijenga ukumbi wa Nyerere Dar wakati tayari AICC ipo ? AICC ilikuwa ni chanzo kikubwa sana cha Uchumi wa Arusha City baada ya UN, sasa UN wameondoka, AICC Mikutano hakuna kwa maana yote inafanyikia Dar unajiuliza kwanini waliamua kujenga huu ukumbi wa Mikutano Dar kwangu mimi ni fumbo, unawezaje kujenga uchumi wa Tanzania wakati unabomoa uliopo?
Sasa hivi Arusha Hoteli zinafungwa hakuna kitu, fikiria tu kwa mfano kwa kawaida Mkutano mkubwa kama wa SADC ungefanyikia Arusha City lkn ulifanyikia Dar sababu ya ukumbi wa Nyerere.
Dar tayari ni mji tajiri Tanzania hivyo hakuna haja tena ya kuipora Miji mingine chanzo cha mapato au mnataka Tanzania nzima wahamie Dar au vipi? Nilisafiri ktk Dar -Arusha inasikitsha sana, baada ya kukata kona ya Segera -Moshi-Arusha tu ni kama unaenda kijijini hakuna magari kabisa na ni mpaka Arusha, zamani hii barabara ilikuwa imejaa magari.
Bill Clinton aliita Geneva ya Afrika alipofika Arusha City leo hii hakuna kitu
AICC enzi za uhai wake, RIP ukumbi wetu.