Arusha city Geneva ya Afrika imegeuka Mogadishu ya Tanzania

Sijaelewa mantiki ya hoja yako kujikita kwenye ukumbi pekee, unamaanisha hatukupaswa kujenga ukumbi wowote Nchi nzima sababu upo wa AICC?
Hata kufikiria kuwa mikutano kutofanyika AICC sababu pekee ni kujengwa ukumbi wa JNICC hilo pia ni jambo la kushangaza..

Ndiyo, hatukupaswa kujenga ukumbi mwingine mbali na AICC sana sana kama kulikuwa na uhitaji tungeuboresha zaidi, kwingine kujengwa vitu vingine kuna mambo mengi Mikoa zaidi ya 20 ya Tanzania inaweza kufanya na kila Mkoa ukawa na kitu chake cha kipekee, Arusha ingeachwa uwe Mji wa International conferences tena tungeenda mbali na kuufanyia promotion hata confrences za nchi nyingine ziletwe AICC, ...
 
Hatujui kujenga uchumi, huo ndiyo ukweli ni lazima tujifunze, AICC ilikuwa inasaidia sana uchumi wa huo Mji hata kuufanya tu ujulikane nje ya Tanzania kama Mikutano mikubwa ingefaynikia huko, fikiria enzi za Mandela kama msuluhishi wa Rwanda/Burundi Mzee Mkapa (RIP) alikuwa anafanyia Mikutano AICC Arusha City, Mikutano mikubwa ikienda Arusha Uwanja wa ndege wa KIA unatumika unajaa ndege na wageni hii ingesaidia sana uchumi wa huko, sasa kila kitu wamehamishia Dar, Dar ambayo tayari ina vyanzo vya kutosha vya mapato, ...
Hiv ni wewe au mwingine amecomment kupitia account yako? Kumbe kuna muda akili huwa zinatulia kabisa unaweza kuona haya?! Aiseee
 
Kujengwa kwa ukumbi Dar,haimaniishi kumbi zingine zife,
Uwezi kuzuia watu wasijenge viwanda,kwa sababu vitafanana na viwanda vya mikoa mingine,
Jiulize General tyre ya Arusha ipo wapi?
Mi nashauri hizi kumbi zijengwe nyingi tu,Mwanza,Dodoma,Mbeya.
Sukari ipo Kagera sugar,Kilombelo,Kwenye cement,tupo Tanga cement,Mbeya cement,Dangote Mtwara,na Wazo hill Dar.
Kufa au kukosa mapato kwa AICC,kusiusishwe na Nyerere conference Dar,kuzuia Nyerere conference,isifsnye kazi,Ili kuiokoa AICC,ni akili mfu,zisizo na tija kabisa.
Natoka arusha na ulichokiongea ni sahihi kabisa
Huwezi kuzuia kumbi zisijengwe eti kisa kuna kumbi nyingine
Tens ikiwezekana hata kila kanda kuwe na ukumbi wenye hadhi ya kimataifa
Muhimu ni kuongeza ubunifu lakini si kusema kwamba serikali imeamua kuiua aicc wakati kumbi zote ni za serikali
 
Back
Top Bottom