Mjopho
Member
- Aug 21, 2025
- 68
- 133
Mkuu kwa namna hiyo tuseme na kila msimu alioshika nafasi ya pili au tatu isomeke hakukuwa na hiyo nafasi?Mimi naona pamoja na kutozwa pesa nyingi, wanyang'anywe makombe pia. Hiyo miaka waliyoshinda isomeke kuwa hakukuwa na bingwa. Kwenye FA cup na league cup pia. Zile pesa walizopewa kama washindi watozwe na zigawanywe kwa kila timu iliyoshiriki msimu huo.
Kina Leicester na wengine walioshuka daraja wapelekewe hizo hela huko walips sasa. Historia ni ngumu kurekebisha ndiyo maana sio lazima kuyagawa makombe kwa aliyemaliza nafasi ya pili, bali historia isome kuwa hiyo misimu hakukuwa na bingwa kwa sababu City alifanya maovu. Hata misimu aliyotoka bila ubingwa, pesa alizoshinda kwa nafasi aliyomalizia itozwe igawanywe kwa timu zingine.
Na bado wakaanzishwa non-league huko waanze upya kupanda, kisheria za huko walikoanzia, siyo unakuta ligi mishahara ya wachezaji ni milo mitatu kwa siku na bima ya afya, halafu wao wanalipa mamilioni. Wao pia wawe na wachezaji wa milo mitatu...
Vipi kama alifika fainali ya FA na EFL na kupoteza, isomeke kuwa timu A ilichukua ubingwa wa mezani?.
Na vipj kuhusu pesa walizopata kwa kushika nafasi ya pili au tatu au kufika stage flani na makombe ya ndani nazo wanyang'anywe???