Arsenal (The Gunners) | Special Thread

YEs, alikuwa anamkataa partey..
Zubi ajiongeze, kwanza awe na confidenve kisha afanyie sana mazoezi bàadhi ya vitu, ubora mwingine sio wa kuzaliwa nao ni mazoezi tu.

Ishu ya saka na martinelli kiukweli martinelli ni bora awe ST kuliko winger,
Saka kwake ni 50 50, yaank sijawahi kumuamini ni kama anabahatisha tu
 
Wanigeria wamecharuka wanamdiss Odegaard kuna jamaa kambatiza jina anamuita 'King of Looking Busy'

Kwenye game dhidi ya Kairat Odegaard anapokea mpira akiwa nyuma robo tatu ya 18. Eze yupo mbele yake karibu na dimba.



Hoja ni kwamba kwa mchezaji anayejali kwamba tunatakiwa kushambulia haraka ilibidi ampe pasi Eze hapa huku yeye akiwa anasogea mbele. Ila Odegaard hakutoa pasi akaanza kudribble kuja hapa dimbani.

Alivyofika dimbani kulia kwake kukawa na wachezaji wawili ambao angeweza kuwapa mpira.



Badala ya kutoa pasi kule kulia Odegaard akampa mpira Eze aliyekua kushoto kwake kwenye hii picha.

Yaani amempa mpira mchezaji ambaye angeweza kumpa sekunde 6 nyuma ila akadribble mpaka dimbani halafu akaacha kuendeleza shambulizi kwa kumpa mpira mchezaji yupo pembeni yake.

Goli la pili dhidi ya Fulham ni Ben kampa mpira Saka, Saka akaachia fasta kumpa Ben, Ben hakukaa nao akamuachia Eze.

By this time wachezaji wa Fulham wakawa wanakuja kwa presha juu wakiamini pale wanaondoka na mpira.

MPira unafika tu kwa Eze. Arteta akasogea pembeni ya Eze.


Hapo Arteta anamuonyesha Eze ishara ya "Tulia" maoni yanasema uzuri Eze hakumsikiliza kwakua kumsikiliza ilimaanisha kuondoa presha ambapo angekua Odegaard angetoa back pass kwa mchezaji aliye nyuma yake.

Ila Eze akatoa through ball kwa Gyokeres, ambapo watu wawili wakasogea kuufuata mpira. Wakaacha gap ambalo Saka akalitumia kupokea mpira na kuscore.

Kwa maoni ya wadau ni kwamba Odegaard angekuepo uwanjani tungeishia moja bila, kwakua hiyo pasi ya Eze asingepiga.
 
Kwa msimamo ulipo sasa mtu wa 13 anaweza pia kushuka daraja lakini ili iwe hivyo inabidi mtu wa 18 ashinde mechi zake tatu alizobakisha.

Timu ya nafasi ya 18, Westham, imebakisha mechi dhidi ya Arsenal, Newcastle na Leeds. Timu ya 13 ikishinda games zake zilizobaki anaweza kwenda Europa.

Nimekuta baadhi ya mashabiki wa Arsenal wanasema dhid ya Westham itakua easy pia game dhidi ya Burnley itakua easy kwavile Burnley ameshashuka daraja.

Nimekuonyesha kwanini game dhidi ya Westham haitakua nyepesi halafu nakukumbusha kwamba West Bromwich walimpiga Chelsea 5 huku West Bromwich ikiwa imejihakikishia kushuka daraja.

Kama unamkumbuka Maitland Niles alikua kwa mkopo WestBrom wakati wanawanyoosha tano. Notice kwamba hiyo timu itacheza kwa kurelax kuzidi wewe, inaweza kuamua kwamba inapaki basi tu wala hawana haja ya kuvuka hata dimba na hauna unachoweza kuwafanya.

Westham hawatokua relaxed ila wanapambanis uhai, sielewi ni kivipi hii mechi watu wanaona itakua nyepesi.

Kwa sasa kwetu kila game ni final. Hua tunashinda magoli matano games za mwisho wa mwaka halafu hua naandika "Haina haja kwa tulipofikia kuscore magoli mengi" maajabu yake msimu huu yale magoli mengi hatufungi tena.

Arsenal to death
 
Huyu Heaven anayechezea Utd nasikia mlimuuza kwa £1m ,? Bonge moja la mistake, nimemuangalia mechi hizi mbili, anacheza vizuri, ana vision pia haogopi .... . Still ana mature , huyo mtu wenu aliyefinalize hili dili anatakiwa anyongwe mbele ya halaiki !

Same mistake kwa Chelsea kumuuza dogo Rhio Ngumoha kwenda Liverpool...ana potential sana..atakuja kuwa mchezaji mzuri



Utd waliwahi fanya makosa ya kumuachia PoGba wakaja kumrudisha kwa pesa ndefu sana ....



Hii ndio football.....inatokeaga
KdB Chelsea walimtema
Salah Chelsea walimtema

Kuna dogo yupo pale Everton utd walimuachia, nadhan watajuta, ameanzA kuonyesha potential..... Tuchel anamuita WC ! James Garner
 
Ukitaka kujua Arteta ni mpumbavu anaamini kuanza na Ode anamuacha Eze.

Kafungwa na city game 2 kwa upumbavu wake.

Ode ametoka mejeruhi anamuanzisha game ya city yaani ni kama jinga lile kocha.
 
Tottenham ameshinda jana hii nimeipenda sana, mechi ijayo Westham watalazimika kushinda tu na sio vinginevyo na apo ndipo watakapocheza mpira wa kufunguka na sisi ndio kitu tunataka kwenye hiyo game wasikae nyuma.
 
Arsenal tumewauzia United Chido pia. Massive potential yule dogo ila akawa anataka aanzishwe first eleven na mpunga upande. Arsenal tukagoma, United wakakubali akaenda pale.

Akacheza games kadhaa, akaonekana bado akashushwa kule kule ambako alipakataa huku.

Sasa mfano wewe ndiyo Heaven, upo academy. Timu ya wakubwa nafasi unayocheza anacheza Gabriel Magalhaes na William Saliba, na hao watu wana miaka mitano mbele ya kucheza kutokana na umri wao wa sasa.

Wewe ndiyo Heaven ungebaki? Na wakati United una uhakika wa kupata namba kwakua defense yao ni ya hovyo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…