EZE:
Nimesikia:
1. Wamiliki wa Crystal Palace pia ni wamiliki wa Lyon. Lyon ilishushwa kwenda Ligue 2 ila imeshinda appeal yake na kurejeshwa Ligue 1.
2. Lyon ilisema kama itashushwa Ligue 2, basi itaiachia nafasi yake ya kushiriki Europa ila sasa kwa kuwa imerejeshwa Ligue 1, basi itashiriki Europa. Hili huenda likawa tatizo kwa Palace, kwa sababu sheria za UEFA hazitaki kuruhusu timu za mmiliki mmoja kucheza kweye shindano moja.
3. Palace kama mabingwa wa FA Cup, wamefaulu kushiriki Europa, ila ndiyo hivyo sasa sheria hii inawapa changamoto.
Kama Palace ikinyimwa kushiriki Europa, je itakuwa rahisi zaidi kwetu kumpata Eze kwa sababu yeye atatamani kucheza UCL kabla umri haujaenda sana na pia Palace huenda wakahitaji pesa tutakazowapa kuendesha timu yao maana watakosa pesa nyingi kwa kuwa nje ya mashindano ya Ulaya