Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Nadhani b4 halland city alibeba akiwatumia Bernado kdb na Foden kama false 9 sababu Gabriel Alikuwa gari ya mkaa
 
Nyie Aseno ni zaidi ya mbwa. Mnacheza na kibonde afu mnanichania mkeka? Hamtakuja kushinda kombe lolote lile la maana; nawalaani. Mtaishia tu kushinda makombe ya Emirates cup wapuuzi nyie!
 
Upo sahihi
 
Nadhani b4 halland city alibeba akiwatumia Bernado kdb na Foden kama false 9 sababu Gabriel Alikuwa gari ya mkaa
KUN AGUERO ndo Msimu alikuwa anaingia toka zaidi kwenye timu sababu ya Majeraha. CITY ina Mtaji wa Kikosi kipana, ARSENAL akiumia Jesus kunakuwa na "EXPERIMENT" nyingi za CF/ST.

ARSENAL inahitaji zaidi Ukomavu wa Mwalimu zaidi ya Players! Klopp alishindwa enda jino kwa jino na PEP baada ya Majeraha ya VVD na MANE. ARSENAL ya Leo akiumia kati ya RICE ama SALIBA hali inakuwa tofauti sana.

Arsenal ni Ile basi tu ila walikuwa wanahitaji winga Mtengenezaji zaidi na Speedster kwa wakati Mmoja. Mudryk angewafaaga sana. {Kina Martinelli wamerudi kwenye "Default"}
 
Binafsi sina tatizo na hao mashabiki wa timu zingine wanaoleta karaha humu ndani maana ni haki yao kama ambavyo tunapeleka karaha kwenye majukwaa yao.

Shida yangu ni hao wanaosema ni mashabiki wa Arsenal alafu wanasema haiwezi kuchukua ubingwa bila kutoa sababu za kimpira zaidi utasikia mara Arteta hana uzoefu, mara hatuna wachezaji wa kushindania ubingwa au mara tumu ina wachezaji wawili tu waliokamilika. Yaan ni watu wanaongea ovyo ovyo tu kama walevi. Tulitarajia timu ikifungwa au ikishinda basi tuje na maoni na mitazamo ya kimpira kwamba timu yetu imefungwa kwasababu kadha wa kadha au tumeshinda lkn bado tunatakiwa kurekebisha 1,2

Kwa wale ambao mnaisifia Liverpool nawakumbusha nyuma kidogo, baada ya Liverpool kucheza final ya UCL 2006/2007 timu ilianza kupoteana kidogo kidogo mpaka kufikia kushindwa kufuzu kucheza UCL 2010/2011 na imemchukua liver misimu mitano kurudi UCL.

Liver ilianza kurudi kwenye form chini ya kocha Roggers mpaka alipokuja kuichukua krop 2016/2017 ikiwa tayari imeanza kuwaka lkn bado ilimchukua Krop zaidi ya misimu 4 kuchukua Epl. Cha ajabu ni kwamba Arteta kaichukua Arsenal ikiwa hoi taabani lkn katumia misimu miwili tu kuirudisha timu kwenye form na sasa ni msimu wa pili tangu timu ikae vizuri na kuanza kushindania makombe lkn bado kuna mtu anakwambia hatuna timu ya ushindani wakati mpaka sasa ipo nafasi ya pili kwa point 2 nyuma ya anaeongoza ligi.

Kuna wengine wanakuja na hoja ya kocha kukosa uzoefu, sawa ila tujiulize ili upate uzoefu inatakiwa ufanye nini? Je ni lazima kuwa na uzoefu ndo ufanye vizuri? Unai ni kocha mzoefu, je alifanya vizuri?. Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka wakati Pep anaochukua Barca kutoka Rigkard je alikuwa na uzoefu?? Zidane je???.

Nadhani wana-Arsenal tusijadili kama kwa kukandia kama ambavyo tunawakandia watani zetu wa timu zingine hilo tuwaachie wao kama tunavyowakandia kwenye majukwaa yao
 
Mkuu ni wewe kweli au kuna mtu anachezea simu yako?
Yuko wapi hamis77 Castr na HENRY14
 
Unachosema ni kweli kabisa lkn je hao strikers wanapatikana? Kuna muda inabidi utengeneze ulichonacho ili kikupe ubora nadhani cha muhimu ni kwamba hao tulionao wameshindwa kufikia ubora basi watafutwe wengine ili watengenezwe. Hao unao wasema akina Mane, Sara na Bob wameboreshwa na Krop. Sarah alivyotoka fc Basal kuja Chelsea hakuwa na ubora huo mpaka akaondoka kwenda Roma na alikuja liver baada Cortinho kuondoka sawa na Mane alivyokuwa Soton hakuna na ubora huo ila ameboreshwa na Krop. Kwahiyo siyo lazima ukanunue top striker ila unaweza kuchukua mwenye potential kisha ukamboresha ili akidhi mahitaji yako
 
Nikiwa Arsepimbi orijino toka Kimbiji naeleza ukweli goli la kwanza la West Harm ni la Referee na VAR team maana mpira ulishatoka nnje ya uwanja.
 
Tupige spana tu mwana Gunner mwenzetu
 
Liver ilianza kurudi kwenye form chini ya kocha Roggers mpaka alipokuja kuichukua krop 2016/2017 ikiwa tayari imeanza kuwaka lkn bado ilimchukua Krop zaidi ya misimu 4 kuchukua Epl

Arteta kaichukua Arsenal ikiwa hoi taabani

Kwahiyo siyo lazima ukanunue top striker ila unaweza kuchukua mwenye potential kisha ukamboresha ili akidhi mahitaji yako
LIVERPOOL ipi Imeanza Rudi wakati wa RODGRES? Ni Moja ya Walimu Pekee wa Liverpool ambao hawajawahi shinda taji lolote na Timu.
KLOPP kaitengeneza timu ikiwa dhoofu haswa, Haikuwa inashiriki Michezo yoyote ya Ulaya, kaenda nayo fainali za UEL huku anaijenga mpaka kaja chukua kila Kombe, ikiwemo EPL baada ya Miaka 30!

Unasema ARTETA Kaikuta Arsenal Mbovu!! Timu imemaliza nafasi ya 5 na Fainali ya UEL kwa Mara ya kwanza msimu wa kwanza wa Mwalimu Mpya inaachaje kuwa Msimu bora kwa kuanzia.
ARTETA mnampa sifa zilopitiliza na ndo mana huoni wale Wachangiaji wenu wenye MAONI TURUFU ya kutopingwa HAMISI na Genge lake. Mnaaminishana Ujinga sana, ARSENAL miaka yote imekuwa timu ya Mpira MZURI, ila Mpira wa Pasi kama huna MESSI timu zinazopaki Basi lazima zikutoe Jasho. PEP mwenyewe amehitaji Msaada wa "FFP Breaching" Kushinda Treble. ARTETA Msimu wa 5 Sasa unasema mmefanikiwa na Mna Kombe 1!

Ukiingia Jukwaa la UTD/CHELSEA/LIVER watu wanakuwa na uhalisia Pa kuponda wanaponda, Wanatoa maoni yao kulingana na Uhalisia, Ila hapa unaweza dhani ni AJAX ya LVG, AC MILAN ya SACCHI, BAYERN ya HEYNCKES, ama BARCA ya PEP. KUBALINI UHALISIA NYIE NI PROJECT INAYOENDELEA SIO KITU KILOKAMILIKA.
 
Kitu unachoshindwa kujua ni kwamba arsenal sio bora kuliko city na liverkuku kama mnavyoaminishana humu. Kuwa kwenu juu msimu huu ni kupoteza form kwa city na liverkuku na bahati mbaya kwenu the two giants are awake now. Mnajipa false hopes kuhusu ubora ila nyie na man utd mko level moja tu sema kiasi mmeboreka ukilinganisha na misimu ya nyuma.
 
Hadi dakika hii siamini tumefungwa fungwa vipi, kuubonda kote kule!

Ila Nina uhakika ata tukirudiana nao kesho kutwa jmoss labda tujitahidi tusiruhusu goal
Ila kuwatia goal, naona haiwezekani kabisa

Kuna Muda timu nzima ya westham ilikua ndani ya box lao, odegard mtafuta mashimo Jana alikua hajui afanye Nini Sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…