PESA HIYOOOOO .!
Unalipa Pauni Milioni 105 kwa mchezaji kama huyu , sio wengine mnalipa 100 hovyo hovyo tu .!
Size ya pitch ya uwanja wa Luton ni changamoto aisee hasa kwa passing game

Kwa kiasi kikubwa hasa kipindi cha kwanza Gaby Jesus alikuwa anasaidia sana kwa Arsenal kusogea juu kwa
1: Kushuka chini , kupokea mpira na kusogea nao juu ( carries )
2: Kushambulia space baina ya outside CBs wa Luton na wingbacks wao

Luton wanastahili pongezi kwa mpango wao : walitumia faida ya udogo wa pitch kwa kubana zaidi space na kutumia counter attacks plus mipira iliyokufa kupata chochote kitu .

Kipindi cha pili ni kama vile ilikuwa nani atafunga magoli mengi zaidi ya mwenzake , mmoja anatumia ufundi wa kuweka mali chini ( Arsenal ) mwingine anatumia ufundi wa mipira mirefu na iliyokufa ( Luton ) : mwisho Arsenal wakawapa Luton ladha ya dawa yao wenyewe . Heartbreaking
NOTE
1: Yule Fullback wa kushoto wa Luton : Doughty ana mwaga maji huyo
2: Ross Barkley kama alikamia vile , kaubonda
3: Kai Havertz anakuja bhana , kajipata tayari
4: Bukayo Saka ni hatari , anafanya vitu kwa level ya juu sana
5: Gaby Jesus kuna muda anakuwa Yes kuna muda No
6: David Raya

nafikiri Ramsdale atakuwa na matumaini nafasi yake bado ipo
7: DECLAN RICE , DECLAN UBWABWA ... PESA .! What a player . Tangu atue Arsenal sikumbuki mechi gani alicheza vibaya . Arsenal waongeze zingine £20M kwa West Ham
8; Kafungwa Luton lakini wanachukia wengine .
FT: Luton 3-4 Arsenal
AMBANGILE