Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Nketiah ni takataka nyingie, nitakuwa wa mwisho kuamini anahitajika kwenye timu ya kuchallenge ubingwa, huyu ni mchezaji wa kina everton huko, namuona danny welbeck ndani yake.. bora BALOGUN.
Toa hiyo takataka tia hata saka, jesus arudi kati pale.

Kipi kimefanya matheo kova aendelee na game, diogo jota alikula kadi kwa namna hii hii.

Tunapata tabu ya kutoka pale chini, jorginho na declan wakekabwa saana anahitajika kiungo mnyumbulifu, kiungo fundi, tia partey huyo.
Partey ni partey.. kuingia kwa partey ni kama akamtia ndimu declan, declan akachachuka.

Partey jitu saana,
Nketia takataka..
 
Tuna haki ya kupata hata wine leo Kipara ametunyanyasa sana huyu Fala ngoja nikanunue nienjoy na movies zangu leo

IMG_4746.jpg

Hapo umenyanyaswa mzee Battle ilikuwa Even Hii
 
TEMBO YULEEEE .!! TAWI LAKE ANALITAKA

Mechi ilikuwa tight sana ni kama vile hakuna mtu aliyetaka kupoteza kwa muda mrefu mpaka nafikiri dakika 25 za mwisho ndio uliona Arsenal wanazitaka zaidi pointi 3 kuliko City na wamestahili kwa hilo

Kipindi cha kwanza kila mmoja alikuwa na mapungufu hasa wakivuka mstari wa kati

ARSENAL :

Kama ukiwa pressed katikati ya uwanja basi njia nzuri ni pembeni ya uwanja na hapo ndio kipindi cha kwanza walimiss sana huduma ya Saka na Martinelli kwenye 1v1 na fullbacks wa City , ndio maana walikuwa wanatupa sana mipira hasa wakikaribia katikati ya uwanja

MAN CITY

Walikuwa wanaishinda pressing ya Arsenal lakini tatizo lao kubwa ilikuwa mbele wamebana uwanja ( Foden Alvarez na Lewis ) walikuwa karibu karibu sana katikati ya mstari wa ulinzi na kiungo wa Arsenal na matokeo yake pembeni ya uwanja waliwaachia Walker na Gvardiol ambao sio wazuri sana kama attacking fullbacks

Kipindi cha pili baada ya kuingia Martinelli lakini hasa hasa Partey ndio naamini mechi ilianza kuwa ya Arsenal zaidi , kwanini ?

1: Partey mzuri zaidi ya Jorginho dhidi ya Counter attacks maana yake anawapa uhuru fullbacks na viungo wa Arsenal kusogea juu zaidi

2: Partey ana uthubutu wa kupiga pasi za mbele zaidi kuliko Jorginho anayependa pasi salama

3: Hapo ndio Arsenal walipoanza kushambulia kwa idadi kubwa zaidi ya wachezaji maana yake City wanakuwa mbali na lango la Arsenal hata wakipata mpira

NOTE

1: Kovacic kaponaje na kadi nyekundu ?

2: Raya ana bahati sana ameenda mapumziko bila kuruhusu goli alikuwa na mchecheto sana

3: Rice Rice Rice ndio maana City nao walimataka

4: Gvardiol anajua boli

5: Haaland kwani alikuwepo uwanjani ? Saliba roho mbaya sana

6: MARTINELLI MATCH WINNER

FT: Arsenal 1-0 City

AMBANGILE
 
Back
Top Bottom