Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Huyu mzee atanipa ugonjwa wa moyo hata mechi za Arsenal naogopa kuangalia huwa nauliza matokeo tu,kafika mwisho wa upeo wake aje yule kocha anaepiga vibao labda vijana watamuelewa.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Bingwa atajulikana 30.4.2011 mechi baina ya man u na wenger boys atakaeshinda ndie atakua anaukaribia ubingwa

...Thanks kwa hiyo PMA, (Positive Mental Atittude!)
humu jamvini Bro Wacha1 ni miongoni mwa walioshikilia msuli Bingwa bado kujulikana!, ...ingawa wengi mara nyingi tushakaribia 'kutupa taulo ulingoni!'
Cartoon-BoxerNegThinking.jpg



...Hii winning mentality ndio inayotakiwa kusiginwa kwenye akili za Arsenal Squad ya miaka hii, Mwenyewe Arsene Wenger kila siku anatuambia Tutashinda, 'wengi hatumuelewi!' ...kwakweli wachezaji na mashabiki ndio wa kulaumiwa...!

Pamoja Boss Mpya yupo radhi kutumwagia kitita cha usajili sikia kauli ya wenger "I don't need to spend" kaniudhi hebu someni hapa Arsene Wenger: I don’t need to spend | The Sun |Sport|Football

...Pamoja na kwamba huyu mzee hata kwenye blog ya Arsenal amezitaja "IF's" mbili tatu, gazeti la The Sun ni anti Arsenal hao, hujawashtukia tu? Gazeti hilo labda kama ni mshabiki wa Page 3 tu :loco::loco::loco:

...huwa sifuatilii articles zao kuhusu Arsenal. Chunguza Articles zao kuhusu Arsenal wakifanya vizuri, ...hukuti kwenye front wala back page. Habari utaitafutia kwenye last but two pages, tena kaji caption kiduuuchu. Hiyo Article weshaipika na kuipakua (taken out of context)

Ni bora ya kusoma Daily Mail/Mail on Sunday, The Mirror au hata METRO!
 
Sawa mkuu,lkn uzalendo umenishinda.

wewe kuwa mwanaume achakuwa mtoto wa kiume hebu jiamin kama unavyokuwa unamdai m2 kesho atakupa usikate tamaa akikwambia hal mbaya hebu jiamini wewe na ARSENAL NI DAMU
bak arsenal wewe ni huku kwanini ukimbie kimbie kama kuku mwenye dege dege hvyo hvyo itakavyokuwa ni nyumba yako 2uu
ARSENAL 4 LIFE ARSENAL IPO JUU
 
Mbwa man ure wamebebwa sana leo walikuwa wafe leo..teja ferdinand kamsukuma anichebe kwenye penalty box refa akauchubua..
 
Wenger kufanya mabadiliko

Kwa mara ya kwanza kabisa kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa kweli anahitaji kufanya mabadiliko ya kikosi cha klabu yake.


Wenger ameyasema hayo siku ambapo Sir Alex Ferguson amesema kuwa kitisho kinayoikabili klabu yake ya Manchester united ni kutoka Chelsea iliyopiga hatua.

Wenger amesema kuwa klabu ya Arsenal ina msimamo mzuri kifedha na ikibidi tunaweza kufanya mabadiliko makubwa.

Aliongezea kuwa, katika ulimwengu wetu kila mmoja analia hana fedha, lakini mtu asiyetumia pesa atakuwa ni mjinga.

Wenger amesema kuwa nia yao ilikuwa kujenga uwanja mpya bila kupoteza nafasi kileleni mwa Ligi kuu ingawaje walifahamu kuwa watakuwa na kipindi kigumu cha mda wa miaka minne hadi mitano.

Kwa hiyo tulichukuwa uwamuzi wa jinsi ya kusalia miongoni mwa timu bora tukitegemea mapato duni yaliyopo.

Tumejitahidi, lakini sasa hivi, bila shaka watu wamechoka. Ninaelewa vyema kwa sababu hata mimi nimechoshwa pia.

Ukitizama msimu wetu utaona kuwa hatuhitaji mabadiliko makubwa. Hapo tutakosea tukifanya hivyo.

Ukiwa na biashara ya gazeti lililo katika nafasi ya pili bora kwa mauzo, hufungi biashara yako.

Lakini lazima tuzingatie dunia ya sasa ambapo ukimaliza wa pili kwa tofauti ndogo, kila mmoja atakuona kama taka.

Akizungumza na wandishi wa habari baadaya mechi ya Manchester United dhidi ya Everton, Wenger aliuliza Je hisia zangu zinanisukuma katika soko? Nahisi daima kuna haja ya kuimarisha kikosi.

Shinikizo la kushindwa kupata ufanisi kwa msimu wa sita mfululizo lilionekana kumdhuru Arsene Wenger siku ya jumatano aliposhuhudia vijana wake wakishindwa kuzuia kuporomoka kwa uongozi wa magoli matatu kwa moja.

Mfano wake wakati akifuatilia pambano hilo umetajwa 'kama adhabu' na wadadisi, akiwemo mwandishi wa gazeti la sportsmail Graham Poll.

Alimsimulia mwandishi huyo kuwa ana nia ya kuongezea majina makubwa kwenye kikosi chake, wachezaji kama Leighton Baines na Per Mertesacker, ambao wana uwezo wa kuifanya klabu ya Arsenal ibuni kikosi kilichoimarika zaidi.

Meneja wa Manchester United Ferguson anakubali kuwa kweli Aresenal kuimarisha kikosi chake kwa kuongezea wachezaji walio na uzowefu kuimarisha kikosi chake.

Ferguson aliongezea kusema kuwa ingawa Arsenal ina wachezaji walio bora kuliko Chelsea lakini ratiba inaonesha kuwa Chelsea wana michuano rahisi kuliko ya Arsenal.

Miongoni mwa wachezaji wanaotazamiwa kuondoka, Denilson atakuwa wa kwanza kuondoka baada ya klabu hiyo kumtangaza kwa kuweka bei ya pauni milioni 5 kwa mcheza kiungo huyo.

Wachezaji Gael Clichy na Nicklas Bendtner huenda wakafuata Mbrazil huyo. Mabadiliko haya ya kipindi cha soko bila shaka yatawaridhisha mashabiki wa Arsenal ambao wamejawa na uchungu pamoja na kukerwa na matokeo ya kushindwa mara kwa mara na miaka sita bila mafanikio.

Hata hivyo, Wenger ameonya kuwa sera yao imekuwa kukuza vipaji vyao wenyewe kwa sababu hawana uwezo wa kuwasajili akina Ronaldo.
 
well-noted, mi tangu arsenal tubondwe na birmgham kwenye curling cup...sina hamu nao tena!! Nimechoshwa bt still this is my favourite team!!
 
kwa nini mnajipa presha. Arsenal sio kabila kwamba huwezi kubadili. Hamia club zisizo na presha wala mawazo. Wenger anawazingua magazeti leo yameripot kuwa hatasajiri mtu next season. Wenger amekuwa mwanasiasa.
 
Mabadiliko yanatakiwa yaanze kwa kumuondoa Wenger! Mafanikio aliyoyapata yanatosha! Sasa hiv kashaishiwa mbinu na anaonekana kuipeleka timu pabaya!
Arsenal inahitaji meneja mpya!
 
Heri ya PASAKA kwa Arsenal Fans wote.........

Poleni sana kwa maumivu...........Yaani tumekuwa si GUNNERS tena......Tumekuwa wapiganaji wa VITA VYA MAJIMAJI...........Dah,Inauma sana....
 
Gooners... Tupeni zawadi ya pasaka leo!! Woop bolto`ns ass for the sake of your funs!!
 
Mbwa man ure wamebebwa sana leo walikuwa wafe leo..teja ferdinand kamsukuma anichebe kwenye penalty box refa akauchubua..


Mkuu usiwe na presha ni kawaida kabisa ya huyo mbwa kubebwa hakuna tofauti yoyote the old story ... .... .. khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee wasipobebwa watakuwa wapi pamoja na bahasha nene kila mwezi kwa marefa?

Mabadiliko yanatakiwa yaanze kwa kumuondoa Wenger! Mafanikio aliyoyapata yanatosha! Sasa hiv kashaishiwa mbinu na anaonekana kuipeleka timu pabaya!
Arsenal inahitaji meneja mpya!

Mkuu ulikuwepo wakati wanamwajiri au unabwabwaja pumba tu, msimu ulipoanza hakuna hata moja aliyesema Arsenal watakuwa hapo walipo, we are a strong team and soon we'll be winners. We have quality than most of our competitors and the majority of them are envious of our progress.
 
Happy Easter watani, angalieni hizo Easter eggs zisiwafanye mkakosa mechi kwa kupitiwa na usingizi.
 
Bolton: Jaaskelainen, Steinsson, Cahill, Knight, Robinson, Lee, Elmander, Muamba, Taylor, Sturridge, Kevin Davies. Subs: Bogdan, Petrov, Mark Davies, Klasnic, Moreno, Cohen, Wheater.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Djourou, Koscielny, Clichy, Song, Wilshere, Walcott, Fabregas, Nasri, van Persie. Subs: Lehmann, Ramsey, Squillaci, Arshavin, Eboue, Gibbs, Chamakh.
 
Captain FAB kapoteza nafasi ya wazi kabisa..... then anakuja na statement why hatushindi vikombe.....anasahau chance kama hizi anazopoteza ndo huwa zinaleta ushindi and hence vikombe......
 
Back
Top Bottom