Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Hakuna magazeti yanayokuaga na stori tamu kama magazeti ya kufungia maandazi au vitumbua..... unasoma unakuta Arsenal inaongoza Premier league.. ukiangalia date, ni May 2004
Kkkkkkk
 
Tumecheza games tatu tukiwa na red.

Games mbili tumepata suluhu moja tumepasuka.

Hii squad haina pumzi wala stamina ya kubaki kumi na kuinflict same damage kwa mpinzani.

Maximo akiwa kocha wa Taifa Stars nimesahau tulikua tunacheza na timu gani ila mchezaji mmoja akapata jeraha akatolewa kisha Maximo hakuingiza sub mpaka dakika zaidi ya 8 zilipoisha.

Baadaye kwenye post interview akaulizwa kwanini ilikua hivyo akajibu alitaka kuona timu itahold vipi wakiwa pungufu uwanjani.

Watu 10 dhidi ya 11 ni fair odds sielewi ni vipi tunashindwa stand our ground. Unaswitch players badala ya mbele kua watatu unaacha wawili au nyuma badala ya kua wanne unawaweka 3. Rahisi mbona? Ila kwakua timu morali inatia huruma ndiyo maana inakua kama tumeonewa.

3 4 3 ya Arsenal inamilikiwaje mpira na 4 4 2 ya Southampton? Only if Arsenal wameamua kutafuta magoli na siyo kupossess. Mentality hii hii tunaenda nayo mbele.
 
arsenal ni bendera inayo pepea nusu mlingoti huku wananchi wake wakiamini wapo huru

arteta hawafai kwa sasa kwani mbinu anazo tumia sio nzuri
 
insta_2465667931825096476.jpeg
 
Finally Auba kafunga
Na Firmino kafunga....

Siku Ile man u anapigwa 6
Sisi tukaja pigwa saba..
 
Mzee umekula Maharage ya wapi?

1 ziyech = 8 Willan + 25 pepe
1 Werner = 40 Lacazette
1 Kante = 10 Partey + 20 Xhaka
1 James = 20 Hector
1 Kovacic = 100 Mo
50 Abraham = 1 Auba
1 Thiago = 20 Luiz + 150 Mustafi
Hivi ni wewe au????
 
Naona sare ya jana imekurudisha mjengoni.
Mimi nipo na nitaendelea kuwepo kwa uwezo wa Allah,

Sijawahi Rudi nyuma,ukiona kimya tu ujue changamoto za kibinadamu hazihusiani kabisa na matokeo ya soka.
Here we go
 
Mimi nipo na nitaendelea kuwepo kwa uwezo wa Allah,

Sijawahi Rudi nyuma,ukiona kimya tu ujue changamoto za kibinadamu hazihusiani kabisa na matokeo ya soka.
Here we go

Mkuu arteta tunamtimua lini?
 
Tumecheza games tatu tukiwa na red.

Games mbili tumepata suluhu moja tumepasuka.

Hii squad haina pumzi wala stamina ya kubaki kumi na kuinflict samw damagw kwa mpinzani.

Maximo akiwa kocha wa Taifa Stars nimesahau tulikua tunacheza na timu gani ila mchezaji mmoja akapata jeraha akatolewa kisha Maximo hakuingiza sub mpaka dakika zaidi ya 8 zilipoisha.

Baadaye kwenye post interview akaulizwa kwanini ilikua hivyo akajibu alitaka kuona timu itahold vipi wakiwa pungufu uwanjani.

Watu 10 dhidi ya 11 ni fair odds sielewi ni vipi tunashindwa stand our ground. Unaswitch players badala ya mbele kua watatu unaacha wawili au nyuma badala ya kua wanne unawaweka 3. Rahisi mbona? Ila kwakua timu morali inatia huruma ndiyo maana inakua kama tumeonewa.

3 4 3 ya Arsenal inamilikiwaje mpira na 4 4 2 ya Southampton? Only if Arsenal wameamua kutafuta magoli na siyo kupossess. Mentality hii hii tunaenda nayo mbele.
I regard Arteta as one of the best promising young couch only with lack of/little managerial experience, despite all the odds against him ningetamani aendelee kuifundisha Arsenal.

Tatizo ni kwamba football sometimes ni moja ya projects ambazo zinakupima kwa matokeo tu, ukiitazama Arsenal for the past decade and a half, utagundua imekuwa na changamoto endelevu na zenye kushika mizizi season after season.

Kuna mdau huko juu aligusia jinsi club ilivyoanza kuporomoka under Wenger toka kuchallenge ubingwa na kuwa regular top 4 club na miaka ya mwisho ya Wenger hata kushiriki Uefa ikawa utata. Ilifikia mahali players wanaforce kuondoka wakiamini pale hakuna nia thabiti za kushinda mataji.

Arteta amepewa kibarua cha kutatua hizi changamoto za muda mrefu na huku akiwa hana experience, ilikuwa hivyo kwa Emery tofauti kidogo yeye alikuwa na managerial experince lakini pia naye angehitaji muda kuzitatua.

Sio kazi rahisi sana hasa kwa kipindi hiki, unazungumza kipindi ambacho Liverpool aliyekuwa 'amelala' yupo on fire, kipindi ambacho Man City anawaburuza kina Madrid, kipindi ambacho Spurs ni title favourite, kipindi ambacho Leicester anapigania top 4, kipindi ambacho Everton inahire kocha wa calibre ya Ancelotti, kipindi ambacho una 'stubborn boys' kama Wolves, Westham na Palace.

Liverpool pia walipitia hizi changamoto na iliwachukua zaidi ya miaka 25 kupata mtatuzi sahihi (Klopp), Man U nao wapo tulipo na so far si Moyes, Van Gaal, even Mourinho na sasa Ole anastruggle pia. Watazame Chelsea pia waliji establish under Mourinho lakini since then wamekuwa na mapito kibao.

Pamoja na yote hayo bado narudi kwa Arteta:
Akiwa kocha 'aliyefundwa' na Guardiola (muumini halisi wa attacking football), nikiitazama Arsenal ikicheza sioni hizo falsafa ndani yake.

Ukiitazama timu ya Pep utaona kuna tofauti kwenye transition, movement na attacking style na ile ya Arteta.

Tofauti ya Arteta ni kuwa hawapi wachezaji freedom ya kumove kwenye open pockets ili wapokee mipira na kuwapa mabeki wa timu pinzani ugumu wa kukaba kutokana na players kuwa kwenye constant motion kutafuta open pockets na hivyo kuwatoa kwenye maeneo yao na kuacha mwanya kupiga mashuti ama penetration passes.

Style anayotumia Arteta inawapa kazi rahisi mabeki kukaba players ambao wako stationary na hivyo kufanya hata washambuliaji wa Arsenal kusaidia kulinda lango pinzani kwa kuwa huwezi piga penetration wala shuti kwenye ule msitu, mbaya zaidi anang'ang'ania kutumia crosses wakati tatizo ni hilo hilo (msongamano) ndio maana tunapiga cross nyingi na zinazofika ni chache na haziwi converted kuwa magoli.

Arteta akibadili hapo trust me, haitaji mechi mbili mbele anaanza kushinda kiulaini tu.

Kuna wadau huko juu wanapiga kelele arejeshwe Ozil, maoni yangu ni kuwa hata aje Messi kwa attacking style yetu mtamtukana pia.

Yees, we need an attacking midfielder but not Ozil. Ozil alikuwepo years back na kila tukibanwa yeye ndio namba moja alikuwa flop kwenye mechi husika, kwa mtu anayejua kuanalyse game Ozil ni very poor tactical player. He has got great talent, but it's very unfortunate that his talent has blinded himself, labda tu anahusishwa kwa kuwa yuko bench pale na analipwa rundo la mshahara ila Ozil is even part of the problem with his bench warming status.
 
Back
Top Bottom